900 itapendeza, Dr Shika alivyowagaragaza Polisi mahakamani

900 itapendeza, Dr Shika alivyowagaragaza Polisi mahakamani

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
IMG-20260817-WA0015.jpg

Siku zimeenda sana, tarehe 9/11/2017 mwamba kabisa wa nguvu the man himself Dr. Louis Shika alitoa somo kubwa sana la kujiamini kwa wanajamii pale aliponunua majengo ya Bilionea Said Lugumi kwa dau la milioni 900

Mnada ulianza kwa dau la milioni 300 mwana akapanda hadi 400, tajiri mwingine akatia 500 mwamba akaweka 600, kibosile mwingine akaweka 700 mwamba kabisa wa nguvu akatia 900 milioni kwa kauli ya " nadhani 900 itapendeza zaidi" 😆😂 .... akashinda tenda

Sasa utata ukaibuka alipotakiwa kulipia asilimia 25 ya mali inayopigwa mnada, akaanza visingizio kwamba anasubiria kutumiwa pesa zake kupitia Western Union maana alikuwa anaishi nje ya nchi kwa kipindi kiefu.

Baadae kesi ilipokwenda mahakamani mwamba alishinda kesi kirahisi na kuwagaragaza waliomshtaki kirahisi mno yaani mfano wa Daudi kumshinda Goliath, kwani mwamba Shika alidai "ni wapi aliposema atatoa milioni 900? wakati yeye alitamka .... nadhani 900 itapendeza zaidi 😂🤣

Apumzike kwa amani mwamba kabisa wa nguvu Dr. Shika.
 
Back
Top Bottom