92% ya Wanafunzi nchini wanatembea kwa Miguu kwenda Shule

92% ya Wanafunzi nchini wanatembea kwa Miguu kwenda Shule

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1674731696429.png

Jiji la Dar es salaam linaongoza kwa kuwa na Wanafunzi wengi wanaotumia Mabasi ya Shule kulinganisha na sehemu nyingine yoyote Tanzania.

Wanaotembea mpaka Shule - 92.6%
Wanaotumia Usafiri wa Umma - 3.7%
Wanaotumia Basi la shule - 1.5%
Wanaotumia Baiskeli - 1.1%
Wanaotumia Magari binafsi - 0.6%
Wanaotumia Pikipiki - 0.4%

NBS/ THE CHANZO
 
....720,000,000M,tunatumia kuwahamisha ma DC's,wanafunzi hao wasubiri kwanza, tuna mpango wa kununua school buses kwa kata za nchi nzima!!
 
Kuna maeneo gari inaingia once in a year,Kuna watoto wakakaa bweni
 
Naona wachangiaji mnawahoji hao waliotoa matokeo ya utafiti. Na mimi nawatetea hawana kosa kutoa matokeo tafiti. Hivi ni kweli Watanzania hatujui umuhimu wa utafiti?

Watafiti kazi yao ni kufanya utafiti na kutoa matokeo ili mamlaka husika zichukue hatua ili kuboresha changamoto zilizobainishwa. Ila kwa kuwa sisi Watanzania ni wa hivi hivi, tunabaki tunawashangaa waliofanya utafiti.

Tunavyoona ni kama vile huo utafiti hauna cha maana, wakati ni jukumu la serikali kuangalia namna ya kuwasaidia wanafunzi wanaoishi mbali na shule kwani wengine wanatembea umbali mrefu hivyo kuchelewa kufika shuleni.

Msianze kusema eti mbona zamani walikuwa wanatembea umbali mrefu. Jiulize, miaka hiyo ubakaji na wizi ulikuwa umekithiri kama leo hii? Leo hii mtoto wa kike ataanzaje safari saa kumi na moja asubuhi kukatisha mapori ili awahi shule?

Mambo yamebadilika. Wanafunzi waboreshewe usafiri ili wawahi shuleni!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom