Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu watanzania;
Kwanini watu weusi walishindwa kuwa wa kwanza kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?
Kwanini wazungu/waarabu waliweza kuwa wa kwanza kuwaza kuja kuwazoa babu zetu na kuwafanya bidhaa?
Waafrika tulikosa nyenzo gani za kutufanya kuwa wa kwanza kwenda Ughaibuni kisha kuwazoa wazungu kuja kufanya kazi za kitumwa katika mashamba yatu?
Je, hii inadhihirisha ya kuwa wazungu/waarabu wana kitu cha ziada kwenye akili/bongo zao (highly intelligent) tangia zama za kale mpaka wakawaza kuja Afrika kwa mara ya kwanza?
HILI SWALI WADAU WENGI WANALIKWEPA
Je, kuna umuhimu wowote wa watu wa bara la Afrika kuendelea kulialia na kulalamikia biashara ya utumwa kama ni janga lililowarudisha nyuma kimaendeleo mpaka sasa?
NINAOMBA KUWASILISHA MADA HII FIKIRISHI. KARIBUNI SANA KWA MICHANGO YENU NDUGU ZANGU
KUMBUKA: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TAFADHALI TIMIZA WAJIBU WAKOIPASAVYO.