A BITTER TRUTH: Kwanini watu weusi walishindwa kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu (Whites) kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

Kuhusu uhusiano wa jina la kundi la mataifa ya Ulaya Mashariki na "slave = mtumwa" angalia hapa:
"The English term slave derives from the ethnonym Slav. In medieval wars many Slavs were captured and enslaved, which led to the word slav becoming synonym to "enslaved person".[21][22][23] In addition, the English word Slav derives from the Middle English word sclave, which was borrowed from Medieval Latin sclavus or slavus,[22][24][25] itself a borrowing and Byzantine Greek σκλάβος sklábos "slave," which was in turn apparently derived from a misunderstanding of the Slavic autonym (denoting a speaker of their own languages)."
 
Jibu zuri sana hili
 
Inaleta mantiki kwa kiasi fulani
 
Kwahiyo mtu akifanyiwa kitu flan na asipoumia bas hajafanyiwa ubaya
Kuumia maana yake ni nini?

Unaweza kunipa mfano wa ubaya unaoweza kufanywa bila mtu kuumizwa?

Ninapoongelea kuumizwa maana yake si lazima mtu asikie maumivu.

Mtu akiibiwa na kuharibiwa uchumi wake, hata kama hajajua, bado kaumizwa kiuchumi hapo.

Na inawezekana asipojua ndiyo kaumizwa zaidi maana atashindwa hata kujipanga kupambana na hali halisi ambayo haijui.

Kaibiwa mali, lakini pia kakosa na ujuzi wa kujua kaibiwa mali.
 
Kwa sababu hawakuona sababu ya kufanya hivyo.
 
Kuna kitu Mungu alipunguza kwenye akili ya mwafrika, ndio maana tulipokea imani zao ukristu (uzungu) na uislamu (uarabu) bila hata kuhoji. Huenda miakav1000 ijayo Waafrika tutaibuka na Yesu wetu aliyezaliwa kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro na kuwapelekea habari njema huko Ulaya.
 
Jibu zuri ila sidhani kama linatosha
 
Elewa hoja...kwanini watu weusi hatukuweza kuwafanya hivi wao?

Basi niongeze...kwanini tulishindwa kupinga hali hii?
Mtu mweusi anayapa kipaumbele mahusiano kuliko kushinda kiuchumi.

Ndiyo maana kiutamaduni mtu mweusi sehemu nyingi ni mjamaa, yuko radhi kuweka kipaumbele kugawana na wenzake kidogo alichonacho kuliko kujilimbikizia yeye awe nacho kingi huku wenzake hawana kitu.

Ukiwa na mentality hii ni vigumu kumfanya mwingine mtumwa on a massive scale kama walivyofanya wazungu na waarabu.

Kuhusu kupinga.

Tumeshindwa kupinga hili, na pengine moja ya sababu ya kushindwa kufanya wengine watumwa, kwa ajali ya kijiografia.

Watu weusi wa kusini mwa jangwa la Sahara wametengwa na dunia kwa bahari ya maji na na bahari ya mchanga (jangwa la Sahara).

Wakati watu wa Eurasia na North Africa wanabadilishana ujuzi na kufanya biashara kwa miaka mingi, watu wa huku Afrika kusini mwa jangwa la Sahara walijuwa wametengwa na dunia hiyo, na kutengwa huko kuliwafanya wasiendelee kibiashara na kiuchumi, na hivyo kiteknolojia.

Kutoendelea huko ndiko kulifanya hata wasiweze kupinga biashara ya utumwa.

Zaidi, watu weusi hawakujiona kama wamoja, wengi waliuzana kwa kuangalia tofauti za makabika na madaraja katika jamii. Weusi wengi, mfano machifu, waliwauza weusi wenzao.
 
Umenena vema mkuu.
 
Kwahiyo hapa tukubaliane waafrika tulikuwa malastborn wa dunia🤣🤣 tulipendelewa sana na Mungu baba kutugea kila kitu hadi tukajisahau
 
Kwasababu africa tumeubwa na moyo wa ukalimu,utu na upendo hatuwezi mfanyia binadam mwenzetu yale tusiyopenda sisi kufanyiwa
Afrika na ukarim wap na wapii?? Usichanganye ukarimu na ushamba😂😂😂
The truth is, sisi sio wakarimu ila tunapoziona zile rangi nyeupe tunakuwa na kamchecheto fulani cha ushamba..
Sisi kwa sisi tunafanyiana mambo mengi sana ya kutisha na kustahajabisha, hatupendani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…