A BITTER TRUTH: Kwanini watu weusi walishindwa kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu (Whites) kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

A BITTER TRUTH: Kwanini watu weusi walishindwa kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu (Whites) kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

Tatizo in kua waafrika bado hatuna ukweli juu yetu kunawezekana maingiliano baina ya jamii hizi yalipelekea upotevu Wa taarifa sahihi ju yetu, lakini biashara hizi za utumwa. Zilianzia misri huko ambapo no afrika,,

Ogopa sana watu wanaoweza kwenda nchi za mbali kwa mito mikubwa kama Nile, Amazon au kwa kutumia bahari kuu.

Tungefanikiwa kupata mabaharia wetu watumiao vyombo vilivyotengenezwa na sisi wenyewe enzi hizo kukatiza bahari kuu basi tungekuwa tupo mbali sana sana kimaendeleo.

Who are the Sea Peoples and what role - American Schools of Oriental Research
sea people from www.asor.org

Who are the Sea Peoples and what role did they play in the devastation of civilizations that occurred shortly after 1200 BCE? The simple ...
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu watanzania;

Kwanini watu weusi walishindwa kuwa wa kwanza kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

Kwanini wazungu/waarabu waliweza kuwa wa kwanza kuwaza kuja kuwazoa babu zetu na kuwafanya bidhaa?

Waafrika tulikosa nyenzo gani za kutufanya kuwa wa kwanza kwenda Ughaibuni kisha kuwazoa wazungu kuja kufanya kazi za kitumwa katika mashamba yatu?

Je, hii inadhihirisha ya kuwa wazungu/waarabu wana kitu cha ziada kwenye akili/bongo zao (highly intelligent) tangia zama za kale mpaka wakawaza kuja Afrika kwa mara ya kwanza?

Je, kuna umuhimu wowote wa watu wa bara la Afrika kuendelea kulialia na kulalamikia biashara ya utumwa kama ni janga lililowarudisha nyuma kimaendeleo mpaka sasa?


NINAOMBA KUWASILISHA MADA HII FIKIRISHI. KARIBUNI SANA KWA MICHANGO YENU NDUGU ZANGU

Ninauza Vitabu Vya Kujifunzia Lugha Ya Kijerumani. Ich komme aus der Stadt Dar Es Salaam und verkaufe diese Deutsch-Lernbücher - JamiiForums

KUMBUKA: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TAFADHALI TIMIZA WAJIBU WAKOIPASAVYO.
Uwoga tu.
 
Ogopa sana watu wanaoweza kwenda nchi za mbali kwa mito mikubwa kama Nile, Amazon au kwa kutumia bahari kuu.

Tungefanikiwa kupata mabaharia wetu watumiao vyombo vilivyotengenezwa na sisi wenyewe enzi hizo kukatiza bahari kuu basi tungekuwa tupo mbali sana sana kimaendeleo.

Who are the Sea Peoples and what role - American Schools of Oriental Research
sea people from www.asor.org
Who are the Sea Peoples and what role did they play in the devastation of civilizations that occurred shortly after 1200 BCE? The simple ...
MTU mweusi uwezo anao japo vikwazo anavyopitia in vigumu sana ila we run the worldwide hata wao wanajua ndiyo sababu wanajitahidi kutuletea mentality za unyonge Wa kifikra ila bahati bado IPO kwetu, changamoto in mifumo ya siasa na elimu ya ya MTU mweusi mwenyewe
 
Uwoga wa nini tena mzee baba?
Kila kitu.
Ukiwa mwoga wa kufa utachukuliwa mtumwa miaka 300.
Ukiogopa kutetea haki na utu wako utakuwa mtumwa na kutawaliwa hadi leo.
Ukiogopa kupambana na nchi zinazokunyanyasa kiuchumi utakuwa unaomba misaada hadi siku unakufa.
Ukiogopa kelele na maneno ya watu utaamini mwaafrika hawezi kuvumbua chochote, kubuni elimu yake wala kutengeneza dawa zake.
Ukiogopa kusikiliza fikra zako utaendelea kufuata dini za wakoloni japo hazingii akili.
Waafrika tunaogopa na kuogopa tu.
 
Mkuu tunajibu ki-shabiki lakini swali lako la ki-falsafa sana, natamani nikujibu ila maelezo nimarefu sana.

Imagine phd holder wa kizungu yupo maabara anatafuta dawa ya COVID-19, Phd wa Tanzania yupo msitu wa pande anakata mizizi kujifukiza ili apone!

PHD Mzungu akigundua hiyo dawaa atauza dunia nzima, phd wa Tanzania akipona, hajui ni jani lipi limemponyesha, na hana cha kusaidia wengine!
😃😃
 
Tatizo munasoma history ya darasani tu na kuona inatosha.
Kwanza kufanya mtu mtumwa haimaanishi ndo unaakili
Tumejenga pyramids kabla hata hatujawatumikisha waisrael kutoka Misri. Inamaana kabla ya kizazi cha yakobo.. waafrika tulishaweza kujenga pyramids of egypt.

Wazungu kukutana na waafrika sio suala la karene ya 15 (hii ni historia mbovu ya darasani)

Utawala wa kwanza Afrika ulikua wa mgiriki kabla ya kuzaliwa yesu... utawala uliofuata ulikua wa italy chini ya Kaisari na cleopatra na mwisho akaja mwarabu baadae baada ya yesu kuzaliwa ambapo tunaona watu kama kina Mansa Musa washaanza kukijenga chuo cha Timbuktu (chuo kikuu cha kwanza duniani) chuo ambacho kilianza kama madrasa kwa jengo moja
hadi majengo matatu makubwa.


Kingine... afrika tulishazunguka dunia nzima kama wazungu hawajaanza kutembea majini... Search Mandingo from mali
Mandingo walifika America kabla ya Christopha Columbas... kabla ya vasco dagama.
Mandingo wamefanya operation kwa kutumia misuli ya wanyama kama nyuzi


Rejea kwenye historia... mji wa kwanza na mtawala wa kwanza duniani anaitwa Nimrod.. nimrod alikua mweusi na ndiye mtawala wa kwanza wa sehem iliyoitwa Babeli... nimrod ni mweusi kwakua baba yake alikua ni Kush.. kush means black


kuna mambo mengi sana
ila waafrica au watu weusi tulishastaarabika..tulikua na akili... tulimiliki dunia

Sent using Jamii Forums mobile app
well said
 
Ueledi umepotea kutokana na hila na njama walizofanya kutokana na sisi kuwaamini wakatake advantage na kutukandamiza wakisema kila kitu chetu ni cha kishenzi vyakwao ni bora leo hii mtu ukienda kutambika ktk mizimu yako unaonekana mshirikina ila ukienda kutambika israel au saudia kwenye mizimu yao unaitwa mtakatifu wake up bro..wake up and live
😃😃😃 inashangaza sana..eti ukienda kuzunguka mti aliokuwa anazunguka marehemu babu yako unaitwa mshirikina..ila kuna watu wanaona fahari kwenda maka kulizunguka jiwe😃😃
 
Najua umenitega
lakini potelea mbali narekebisha kidoogo uoni wako.
Kuna vitu vingine vya kwetu ni kweli ni vibaya ,na havina tija yoyote na vinakwaza maendeleo yetu,hasa kwa vile vinatumika kimakosa.
Wazungu leo duniani wamefungua vyuo vya kujifunzia uchawi ,na wanautumia kwa maslahi kama ya kiuchumi,biashara,kivita na kiupelelezi. Hapa ndipo sisi tulipo miss point. Huku kwetu tunatumia uchawi kuulia watu tusio wapenda,au kuwaadhibu watu innocent na kujijengea jina kwa watu ili wakuogope.
Unaona tofauti ,sio kutambik tuu,bali kuwepo na halisia wa manufaa makubwa.

Sasa ile habari ya Kule Jerusalem na Makka ,hii si mizimu wala matambiko, Yale ni maaeneo aliyoyachagua Mungu mwenyewe ili wale wanaotaka matambiko ya ukweli na uhakika waende pale kwa Mungu na kumsemeza shida zao.

Na kwa vile Mungu ana wivu amewakatezeni kutambika mitaani kwenye vinyamkela,kwani huko kuna shetani,labda uniambie wewe kuwa umefanya shirika naye huyo shetani.Pole sana.

Si kila chetu ni cha kishenzi, kweli wali 'take advantage' lakini kutokana na kulala kwetu na ujinga wetu, hadi leo bado tuko USINGIZINI?
LINI TUTAAMKA NA KUJITAMBUA?
😃😃 eti alipo pachagua mungu... hichondio ambacho walichokifanya watu wa middle east wame wa_brainwash ili muweze kuamini kuwa matambiko yao ni chaguo sahihi la mungu na yakwetu hayafai ili iwe rahisi kwa wao kuweza kuwatawala nakatika hilo wamefanikiwa
 
mzunguko huo

kingine binadam wanaamini sisi wa kizazi hiki ndio tunaakili[emoji38][emoji38][emoji38] watu walikua na akili wakajenga pyramids
kwenye pyramids kuna michoro ya viti vinafanana na helicopter... michoro ipo kabla yesu hajazaliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
yeaahh huwa wana amini hivyo.... sijui nani aliyewalisha matango pori hayo 😃😃
 
Mkuu wewe ndio umetoa jibu la kueleweka watu wanawakuza sana wazungu.

Wakumbushe pia General Hannibal yule black wa Numidia, aliitawala mpaka hispania na aliteka mpka Alps kwa kudefeat majeshi ya Roman Empire akitokea ilipo Tunisia ya leo.

Pia anasahau Moors wa Algeria waliwahi chukua watumwa kutoka uturuki na kuwapekeka huko kufanyishwa kazi. Wanawake walichukuliwa for sex slavery!!

Hta wanasahau 25th dynasty ile ya weusi wa Nubia/ sudan ya leo iliotawala misri chini ya kina pharaoh Thutmose ilistretch utawala ma kuchukua watumwa mpka Asia minor.

Mifano ni mingi sana ila watu wanarejea ya historia ya mzungu tunaofundishwa Form 3B!!

Niwakumbushe tu hta hao wazungu wamewahi kuwa koloni kwa Waarabu wa Ottoman empire na Mongolian Empire. Waliwakuta wazungu wengi tu huko eastern europe washamba hta wanajisaidia kokote tu!! Wakawateka kiulaini na kuwatawala. Na kama sio kifo cha Suleiman ama Genghis Khan historia ingekua tofauti sana.

Naomba kuwasilisha

Cc Infantry Soldier
watu sijui hawasomi. mbona kuna mabandiko mengi tu humu yanayo eleza history ya mtu mweusi... hao the moors uliowataja wamewahi kuitawala mpaka ufaransa tena walikuwa na tech ya hali ya juu
 
😃😃😃
Egypt iliyowapokea na kuwatumikisha wayahudi haikuwa ya weusi.
Inventions nyingi zilizofanywa Afrika hazikufanywa na weusi, hata hizi unazosikia geometry na algebra kugunduliwa north Africa, hawakuwa weusi wale! Ni waarabu hawahawa tunaowaona leo wa Egypt, Morocco, Tunisia, Algeria, na hawa wa Egypt walisonga wakasogea hapo Sudan ambako hawaivi na weusi, unaona hata sasa nchi imegawanywa weusi wakabakia kusini. Ethiopians hawajikubali kama waafrika, actually wako Afrika kijiografia tu lakini hawapendi unasaba na weusi, na hiki ndicho chanzo cha mapinduzi ya Ethiopia yaliyomwondoa Mfalme Haile Selassie, ambapo Col Mengistu Haile Mariam alitoka jamii ya watu weusi waliokuwa wananyanyaswa Ethiopia na ndio waliokuwa wanapewa kazi za ulinzi, akatumia fursa hiyo kumpindua mfalme. Chanzo cha Eritrea kujitenga na Ethiopia ni hichohicho, kila anayejiona mweupe zaidi anajihesabia haki zaidi dhidi ya anayeonekana mweusi zaidi. Wasomali wanapenda kujitambulisha kama wasomali, hawapendi uafrika! Kwahiyo waafrika weusi ndio wanaotengwa, na sifa yoyote nzuri inayozungumzwa kwa jambo lililofanikiwa Afrika siyo ya hawa weusi!
wewe jamaa acha mambo yako 😃😃😃 kwahiyo wataka kusema kwamba kina pharao ramisese walikuwa ni watu weupe?
 
unajua mwarabu ameingia egypt mwaka gan??.. [emoji4]
unazungumzia historia ya mtu kama haile wa karne ya 20
me nakupa data za misri iliyoongozwa na Black khemets (kushite)... miaka elfu 3 kabla ya kuzaliwa yesu... means huu ni mwaka 2020 toka azaliwe yesu
urudi miaka elfu tatu kabla
ambapo hata nabii mussa alikua hajazaliwa.
Misri ambayo iliishi kwa kuamini miungu kama Amun-ra... osirs.. horus ... Anubis ... sobek

Bro.... [emoji38]

Sent from my SM-J5007 using JamiiForums mobile app
😃😃😃 hawajui hao...wanadhani kwamba history ya ulimwengu huu imeanza juzi...laiti wangekuwa wanambua kuwa sehemu zote hizi tunazoishi waliishi watu hapo kabla na nyumba zetu na misikiti namakanisa yetu tumejenga juu ya makaburi yawatu wakale wasingekuwa nahizo fikira
 
Source wikipedia? Leta credible evidence mkuu
Haya nmetaja hapo Thutmose 3 naye mweupe? 25th dynasty ilikuwa weupe? Haya Kush Empire iliotawala Ethiopia mpaka Middle East nayo weupe?

Kingine nmekuonyesha hao wazungu walishatawaliwa na race zingine mfano nmetoa Mongolia, Ottoman, Caliphate ya Baghdad n.k

Tukitaka kubalance mjadala mtueleze kwanini mnaanzia historia ya 15th century kuonyesha utumwa ni watu weusi tu
😃😃👏👏👏 paragraph ya mwisho umemalizia kwa kuuliza swali murua sana
 
Back
Top Bottom