A day in the Buddhist college

A day in the Buddhist college

Tulikuwa na test mara mbili au tatu kwa wiki na passmark ilikuwa above 60, ukipata chini ya hapo unaenda Buddha/meditation hall unapiga magoti na kurecite buddha's mara 1000
[emoji22] [emoji22] [emoji22] [emoji22] [emoji22] ilitaka moyo wa ziada
 
Nilikuwa nina uwezo wa kutabiri hatari Neema au chochote, lakini pia niliporudi Tanzania kuna siku nilienda kanisani na wakati naenda kukaa siti za mbele nilikuwa na kitu kama vibration wakati nawapita watu
Lakini pia nimeshasimulia sana hapa JF matukio mengi ya kuibiwa nk na waliofanya hivyo ikala kwao
Naomba jina la uzi huo pls niende nikazisome nami.
 
Kama maswali yameisha nitaendelea na sehemu ya pili

A NIGHT INSIDE BUDDHIST COLLEGE
Binadamu ni mtu anayependa uhuru na ukimchunga atatafuta mbinu ya kuwa huru
Ndani ya kile chuo tulichungwa sana na kama ikitokea umekamatwa umetoroka adhabu yake ilikuwa ni kufukuzwa chuo moja kwa moja
Hatukurusiwa kuvaa nguo zetu za nyumbani kila kitu kilikabidhiwa na kufungiwa store siku tulipowasili na tukapewa hayo manguo ambayo ndio ilikuwa 24/7 tunayavaa popote tulipokuwa (tulikuwa na pair mbili)
Chuo kilikuwa kilometer moja kufika mjini na nusu kilometer kufika barabara kuu
Chuo kilizungushiwa ukuta wa matofali na fence ya umeme na security lights lakini pia mijibwa mikali yenye roho mbaya sana
Wanachuo walilala floor ya chini na ya pili na mamaster floor ya tatu kwahiyo kama ungetaka kutoroka usiku ilibidi ufanye yafuatayo
- utaimu mijibwa ikiwa haiko upande wa mabweninini
- mtu akusaidie kuzima umeme kwenye fence
- ufanikiwe kuruka ukuta wa mita tatu bila kishindo na bila kuyastua makubwa huko yaliko
-ufanikiwe kuvuka security lights bila kuonekana na mamaster ghorofa ya tatu
-kisha utambae kwenye majani umbali wa nusu km mpaka kufika barabara kuu ndio unakuwa salama
Ukikaribia barabara kuu unavua manguo ya kibuddha ndani una T-shirt na jeans na kapelo na raba (nguo hizi zilikuwa zinafichwa mbali sana)
Unaingia mjini unafanya yako halafu wakati wa kurejea hali ni ileile, yani ilikuwa ukirudi bwenini salama unamshukuru Mungu na kujiapiza kuwa hutotoroka tena
[emoji15] [emoji15] [emoji15] ni zaidi ya utumwa aise
 
attachment.php

Hapa ndio chuo nilipoanzia kujifunza mambo ya Buddhism, meditation, chanting nk. Hii ni picha ya mwaka 1997, na hiyo ni sehemu ya wanachuo.

Hiki kilikuwa ni chuo kugumu na chenye sheria kali kuliko jeshi, tulikuwa wanachuo 21 toka Tanzania lakini tulifanikiwa kumaliza chuo tulikuwa kumi tu na mwishoni watano.

Tulipewa kila kitu bure lakini vinavyofanana kuanzia nguo mpaka dawa ya mswaki. Tuliishi maisha ya useja(total celibacy) huku tukiziadhibu hisia kwa kiwango cha juu mno.!

Tulikuwa kwenye self cultivation (bringing back the scattered mind)Na hii ndio ilikuwa ratiba ya siku moja inayojirudia mara sita kwa wiki.

05:40 kuamka kutandika vitanda na kupiga mswaki/kuiga

05:50 parade/rollcall

06:00-0650 chanting/meditation

06:50-07:00 parade/rollcall na kwenda dining hall kimya na kwa mistari bila kuangalia kulia wala kushoto

07:20 chanting n giving offerings kwa milefo,na hungry ghost kisha breakfast

07:20-07:50 usafi

07:50-8:00 parade/roll call na kuingia darasani

Vipindi vilikuwa ni dk 50 mapumziko dk 10 kuanzia saa mbili mpaka saa tano na dk 50

11:50-12:00 parade/ roll call na kumatch kwa mistari iliyonyooka kwenda dining

-Kuchant kutoa offerings kwa Milefo(future buddha?), hungry ghosts na kisha kula

12:00-13:50-lunch, walking meditation na kupumzika

13:50-14:00 parade roll call na darasani mpaka saa 15:50

15:50-16:00 parade roll call na kubadili nguo

16:00-16:50 martial arts, kung fu karate tai chi nk

16:50-17:50 free time hapa ndio sasa mnaweza kupiga soga na kuendelea na martia arts gym library etc

17:50-18:00 parade rollcall na kumatch kwenda dining

18:00-18:50 chanting offerings kwa Buddha na hungry ghost na kupata dinner

18:50-19:00 parade roll call

19:00-20:50 darasani

20:50-21:50 meditation/chanting

21:50-20:00 kurudi vyumbani kwa kumatch kwenye mistari tena kimya, kuingia vyumbani kuzima taa na kulala
Ukionekana nje baada ya hapo ni majanga

Chuo kiliongozwa na sheria kwenye kila kitu, sheria ya kutumia Maji, kutembea, kuongea kukaa kula kugeuka kulala, kutandika kuvaa etc kila kitu kilikuwa ni sheria na ndio maana wengi sana walishindwa maisha yale
Hii picha ni jinsi tulivyokuwa tunakaa mstarini kila mtu na nafasi yake kwahiyo hata kama haupo nafasi yako inabaki wazi.

View attachment 274159

Hv Mkuu ktk upande Wa iman ya mabudda wanaamin binadamu wa kwanza alikuwa ni nan na alitokana na nn? Maana ktk upande wa ukristro na uislam wanaamin binadam Wa kwanza ni adam na hawa na wameubwa. Ningependa kufahamu kwa upande Wa mabudda ipoje
 
Kwenda selo haikuwa ishu sana ishu ni kwamba hatukuwahi na documents zozote kama passport nk kwakuwa kila kitu kilikuwa kinashikiliwa na uongozi wa chuo
Hivyo ikabidi kila mtu afe kivyake asikamatwe, jamaa yetu mmoja walivamia choo akajifanya ni mhudumu wa choo, akalivagaa sink na kinyesi chake mzungu akamuacha wawili waliruka ukuta lakini walikatwa vibaya sana na vioo vile vinavyochomekwa juu ya ukuta lakini wakasalimika, mimi niliingia kwenye pipa la maji lililokuwa na Maji nusu....imagine baridi ya South halafu uzame kwenye pipa la maji baridi
Hali ilipotulia tuliondoka salama lakini nikiwa natetemeka hasa kwa baridi na mwenzangu akiwa ananuka kinyesi tupu, wale wenzetu wawili walifika mapema na wanaingia salama bwenini nasisi pia vilevile, tuliwatibia usiku ule ili damu ikate asubuhi wawe parade bila mabandage..ni kitu kigumu mno lakini walihimili
Watukutu [emoji1] [emoji1]
 
Nilinusurika kifo mara nne
Naweza kukiri kwamba meditation, martial arts na mazingira ya chuo yalinijengea uwezo fulani wa nguvu fulani, nguvu zenye uwezo wa kukuepusha au kujua hatari ijayo
Leo hii ningekuwa marehemu niliyeoza siku nyingi sana lakini kw namna ya ajabu kabisa nikakikwepa kifo mara nne
mara ya kwanza kwanza kwenye chumba fulani mtaani self container nilitorokea dirisha la bafuni/chooni..wakati jamaa, wakivunja mlango ili waingie wanimalize
Mara ya pili ilikuwa ni kama kilometer tatu tu kutoka chuoni wakaniotea niliwazidi maarifa nikatoka nduki mbio ambazo nafikiri nilimzidi Bolt
Mara ya tatu ilikuwa sumu kwenye pombe, nikategesha chupa mdomoni kama sekunde tano, nikaishusha mezani nikasepa

Mara ya nne ilikuwa na mambo mengi sana
Nilitoka chuoni saa nne usiku nikiwa na bastola( nilikuja kununua silaha) na hii yote ilikuwa kwa ajili ya kujilinda, nikafika mpaka Sambonani kwaito likiwa ndio kwanza linakolea
Mtu niliyemfuata akanipa signal kuwa pale hapakuwa penyewe wale wagomvi wangu walikuwepo kwahiyo tukachukua tax kwenda Zithobeni km kama tano hivi toka pale mjini
Tukafika kwenye bar moja kubwa na ukumbi wa disco, sasa ukifika pale unakabidhi silaha mlangoni kisha unasachiwa ndio unaruhusiwa kuindia ndani, mimi silaha niliichomeka chini y kitovu na nikanuia jamaa wasiione kweli haikuonekana nikaingia
Tukiwa tunakunywa kwenye dimlights za ukumbini nikawaona wabaya wangu meza kama ya nne hivi, palepale yakanicheza, lakini wakati huohuo mmoja wao akaenda chooni
Nilikaa tayari kwa lolote, nikiwa nawaangalia jamaa niliona mmoja ananyanyua chupa, na umeme ukakatika nilimrukia mtu wangu tukaanguka chini, kilichofuatia ni kishindo cha chupa ukutani nilisikia upepo wakati inapita juu ya kichwa changu
Kama movie vile
 
Hv Mkuu ktk upande Wa iman ya mabudda wanaamin binadamu wa kwanza alikuwa ni nan na alitokana na nn? Maana ktk upande wa ukristro na uislam wanaamin binadam Wa kwanza ni adam na hawa na wameubwa. Ningependa kufahamu kwa upande Wa mabudda ipoje
Ubudha niliosoma mimi , kwakuwa kuna sects nyingi sana kwenye Buddhism unaamini kuwa origin ya dunia/uumbaji ulitokana na the realm of existence, cause conditions and effect . kwamba hakukuwa na mwanzo wa dunia/uumbaji kwa hiyo hakuna mwisho
Hili swali linajibiwa kwa kukwepwakwepwa kwakuwa Buddhism ilianzishwa na Sidharta Goutama (Sakyamuni Buddha) mwana mfalme ambaye alikuta tayari dunia ipo na maisha yanaendelea
 
tetee kuna maisha watu tumepitia kiasi kwamba hata ukija sehemu kama JF halafu unakutana na mtu ambaye hata hakufahamu na anaanza kukupotomoshea matusi unamwangalia tu....
Tatizo limited experience ya mtu alonayo anafikia hatua ya kukuhukumu. Sio kosa lako it's their loss.
 
Kwa kweli nimejifunza meeengi kwenye huu uzi
Hapa nimeandika machache tu kwenye maisha ya chuoni ambapo ndio ilikuwa kama chanzo cha kuingia kwenye kujifunza elimu ya upande wa pili kwenye hii dunia
Ukizama sana kwenye haya mambo na ukasafiri na kufika hizo sehemu zao wewe mwenyewe bila kuhadithiwa na ukaona kwa macho yako yale yanayotokea na kutendeka pale purely practice n sometimes supernatural powers unaweza kufika mahali pa kukufuru kuwa Mungu
Nakumbuka mwaka 2000 tulienda Malaysia kwenye mji mmoja mzuri sana unaitwa Johor bahru, lakini hatukukaa mjini sisi ilikuwa ni watu wa milimani misituni au sehemu za kimya
Basi tulipanda milima huko mpaka sehemu ambayo si gari pikipiki wa baiskeli inaweza kupanda, halafu baada ya hapo mnapanda kwa miguu almost three hours
Huko ndani juu kabisa ni nyie na miti umande na mawingu ni dunia nyingine kabisa hakuna chochote bali temple moja kubwa sana ambalo material yake ya kulijenga sijui yalifikishwaje kule
13af0955c2a1b3e1c77a7c4b8c9058de.jpg
huko ni dunia nyingine kabisa na kuko kimya hasa...huko ni habari nyingine....hiyo picha ni kizimba cha meditation
 
Yaanii unajua kusimulia kama natizama documentary hapa. Basi ndio maana wengine hujawa na kiburi na kuona Mungu hayupo.
Ila vitabu vinasema itafuteni elimu ijapokua ni nchi za mbali. Na hizo materials za ujenzi huenda zilipandishwa ki supernatural!!!! Lakini mjenzi hasa ni nani?? Vipi majoka huko juu, je huwa watu wanaokaa humo ndani ya hilo temple permanent au wote watalii??
 
Ishu za majoka kule hakuna kule ni pure practice na watu wako serious hasa....kuna watu wanaishi huko tulikuta baadhi wana zaidi ya miaka 3 hawajawahi kufika mjini...! Waende kufanya nini? Wanakwambia kule kuko contaminated na ni full illusions, life there is not real magari nguo za gharama makeups pesa nk nk
Wako huko juu na amani tele na wako powerful mno wanakula natural wanalala natural practice zote ni natural vyombo na vitu vingi humo ndani ni handmade mavyuma ni kidogo sana miti ndio mingi vyombo karibia vyote ni vya udongo
98357808007b99a8323be04bd3de8354.jpg
 
I wish siku moja niende huko nikatembee. Hao kuwapeleka mjini ukawape baga ni kuwatesa aisee.
Wanaishi maisha ya uhalisiaa, hakuna stress za kodi wala kutafuta pesa. Mungu mkubwa
 
I wish siku moja niende huko nikatembee. Hao kuwapeleka mjini ukawape baga ni kuwatesa aisee.
Wanaishi maisha ya uhalisiaa, hakuna stress za kodi wala kutafuta pesa. Mungu mkubwa
Hata wewe ukienda retreat ya wiki moja tu ukirudi mjini hata haya maji ya chupa unaweza usiyanywe ni kemikali tupu, unaingia tetee wewe anatoka tetee mwingine kabisa mwenye tafakuri mwenye subra mwenye kituo na kiasi.....unajiona kabisa uko tofauti uko settled
 
Ninakua kama nimerudi Bustani ya Eden, na nilivyofast learner lazma nibadilike, yaani kama ndani ya wiki napata matokeo chanya mbona nazidi kutamani kwenda!!
ila kwa mjini ni ngumu kuyakwepa maji yenye fluoride ujue, labda kama kuna vyanzo vingine ukitoa ya kisima!
 
Lakini sijui kwann mikoani hakuna sehemu zenye kutoa mafunzo kama Dar
 
Back
Top Bottom