Hapa nimeandika machache tu kwenye maisha ya chuoni ambapo ndio ilikuwa kama chanzo cha kuingia kwenye kujifunza elimu ya upande wa pili kwenye hii dunia
Ukizama sana kwenye haya mambo na ukasafiri na kufika hizo sehemu zao wewe mwenyewe bila kuhadithiwa na ukaona kwa macho yako yale yanayotokea na kutendeka pale purely practice n sometimes supernatural powers unaweza kufika mahali pa kukufuru kuwa Mungu
Nakumbuka mwaka 2000 tulienda Malaysia kwenye mji mmoja mzuri sana unaitwa Johor bahru, lakini hatukukaa mjini sisi ilikuwa ni watu wa milimani misituni au sehemu za kimya
Basi tulipanda milima huko mpaka sehemu ambayo si gari pikipiki wa baiskeli inaweza kupanda, halafu baada ya hapo mnapanda kwa miguu almost three hours
Huko ndani juu kabisa ni nyie na miti umande na mawingu ni dunia nyingine kabisa hakuna chochote bali temple moja kubwa sana ambalo material yake ya kulijenga sijui yalifikishwaje kule
huko ni dunia nyingine kabisa na kuko kimya hasa...huko ni habari nyingine....hiyo picha ni kizimba cha meditation