A day in the Buddhist college

A day in the Buddhist college

Nina tabia ya kumwaga soda chini ama kinywaji chochote kabla ya kukinywa halafu nasema for Ancestors kumbe naabudu nisicho kijua

Knowledge kama hizi ingekua lazima kila mwanadamu azijue dunia sijui ingekuaje

Nimejitahidi sana kusoma hii thread nimefika page ya 23 nikashindwa kuendelea
 
mkuuu mshna nz mihuri tena?
Yeah inaitwa ordination ceremony
Muhuri wa kwanza ni dot tatu kichwani zinawekwa kwa kuunguzwa na vimshumaaa vidogo sana size ya kama njiti za kibiriti ukiziunganisha 2au3 inauma sana
Ya pili hivyo hivyo na ya tatu hivyo hivyo. .Ukikutana na mwenye dot tisa kichwani huyo kaiva hasa kwenye kila sekta
 
Nina tabia ya kumwaga soda chini ama kinywaji chochote kabla ya kukinywa halafu nasema for Ancestors kumbe naabudu nisicho kijua

Knowledge kama hizi ingekua lazima kila mwanadamu azijue dunia sijui ingekuaje

Nimejitahidi sana kusoma hii thread nimefika page ya 23 nikashindwa kuendelea
Tatizo ni nini?
 
Nina tabia ya kumwaga soda chini ama kinywaji chochote kabla ya kukinywa halafu nasema for Ancestors kumbe naabudu nisicho kijua

Knowledge kama hizi ingekua lazima kila mwanadamu azijue dunia sijui ingekuaje

Nimejitahidi sana kusoma hii thread nimefika page ya 23 nikashindwa kuendelea
Malizia mkia
 
#59,
Hii thread nilikuwa naifukuzia kimya kimya/mdogo mdogo style mbio za teja. Dunia ina mengi, na ukitaka kuyajua huwezi kuyamaliza yote.

Heko kwako Mshana Jr.
 
1470552609231.jpg
hili ni temple jipya ambalo tulishiriki kulijenga kwa kufanya fundraising wanachuo wa kitanzania kwenye nchi za Taiwan Singapore na Malaysia
Tulishiriki shughuli za kijamii
Tulifanya maonyesho ya nyimbo za kiafrika na ngoma
Tulifanya maonyesho ya martial arts na nyimbo za kichina na kibuddha
Tulihubiria wachina Buddhism kwa kichina
Tulialikwa kufanya makongamano kwenye vyuo vikuu vya nchi tulizotembelea
Msaada ambao sitausahau ni wa mama mmoja mtaiwan yeye ali pledge usd milioni moja
 
Hapa nimeandika machache tu kwenye maisha ya chuoni ambapo ndio ilikuwa kama chanzo cha kuingia kwenye kujifunza elimu ya upande wa pili kwenye hii dunia
Ukizama sana kwenye haya mambo na ukasafiri na kufika hizo sehemu zao wewe mwenyewe bila kuhadithiwa na ukaona kwa macho yako yale yanayotokea na kutendeka pale purely practice n sometimes supernatural powers unaweza kufika mahali pa kukufuru kuwa Mungu
Nakumbuka mwaka 2000 tulienda Malaysia kwenye mji mmoja mzuri sana unaitwa Johor bahru, lakini hatukukaa mjini sisi ilikuwa ni watu wa milimani misituni au sehemu za kimya
Basi tulipanda milima huko mpaka sehemu ambayo si gari pikipiki wa baiskeli inaweza kupanda, halafu baada ya hapo mnapanda kwa miguu almost three hours
Huko ndani juu kabisa ni nyie na miti umande na mawingu ni dunia nyingine kabisa hakuna chochote bali temple moja kubwa sana ambalo material yake ya kulijenga sijui yalifikishwaje kule
13af0955c2a1b3e1c77a7c4b8c9058de.jpg
huko ni dunia nyingine kabisa na kuko kimya hasa...huko ni habari nyingine....hiyo picha ni kizimba cha meditation
Mkuu mshana tuhabarishe basi na hii habari ya huko maana inaonekana kuna vitu sana huko
 
Ishu za majoka kule hakuna kule ni pure practice na watu wako serious hasa....kuna watu wanaishi huko tulikuta baadhi wana zaidi ya miaka 3 hawajawahi kufika mjini...! Waende kufanya nini? Wanakwambia kule kuko contaminated na ni full illusions, life there is not real magari nguo za gharama makeups pesa nk nk
Wako huko juu na amani tele na wako powerful mno wanakula natural wanalala natural practice zote ni natural vyombo na vitu vingi humo ndani ni handmade mavyuma ni kidogo sana miti ndio mingi vyombo karibia vyote ni vya udongo
98357808007b99a8323be04bd3de8354.jpg
Na vepe kuhusu gharama za kila siku ni nani aliyekuwa anawawezesha ktk kula,mavazi nakadhalika???? Hasa ukizingatia ni sehemu iliyojitenga sana
 
Na vepe kuhusu gharama za kila siku ni nani aliyekuwa anawawezesha ktk kula,mavazi nakadhalika???? Hasa ukizingatia ni sehemu iliyojitenga sana
Waumini ambao wengi walikuwa matajiri sana toka nchi nilizotaja
 
Nifahamishe 'hanyu' ndio nini mkuu?
Han yu ni lugha ya kichina (mandarin chinese)China kuna makabila pia! Hiyo Han yu ni kama lugha ya Taifa kama ilivyo kiswahili
 
attachment.php


Hapa ndio chuo nilipoanzia kujifunza mambo ya Buddhism, meditation, chanting nk. Hii ni picha ya mwaka 1997, na hiyo ni sehemu ya wanachuo.

Hiki kilikuwa ni chuo kugumu na chenye sheria kali kuliko jeshi, tulikuwa wanachuo 21 toka Tanzania lakini tulifanikiwa kumaliza chuo tulikuwa kumi tu na mwishoni watano.

Tulipewa kila kitu bure lakini vinavyofanana kuanzia nguo mpaka dawa ya mswaki. Tuliishi maisha ya useja(total celibacy) huku tukiziadhibu hisia kwa kiwango cha juu mno.!

Tulikuwa kwenye self cultivation (bringing back the scattered mind)Na hii ndio ilikuwa ratiba ya siku moja inayojirudia mara sita kwa wiki.

05:40 kuamka kutandika vitanda na kupiga mswaki/kuiga

05:50 parade/rollcall

06:00-0650 chanting/meditation

06:50-07:00 parade/rollcall na kwenda dining hall kimya na kwa mistari bila kuangalia kulia wala kushoto

07:20 chanting n giving offerings kwa milefo,na hungry ghost kisha breakfast

07:20-07:50 usafi

07:50-8:00 parade/roll call na kuingia darasani

Vipindi vilikuwa ni dk 50 mapumziko dk 10 kuanzia saa mbili mpaka saa tano na dk 50

11:50-12:00 parade/ roll call na kumatch kwa mistari iliyonyooka kwenda dining

-Kuchant kutoa offerings kwa Milefo(future buddha?), hungry ghosts na kisha kula

12:00-13:50-lunch, walking meditation na kupumzika

13:50-14:00 parade roll call na darasani mpaka saa 15:50

15:50-16:00 parade roll call na kubadili nguo

16:00-16:50 martial arts, kung fu karate tai chi nk

16:50-17:50 free time hapa ndio sasa mnaweza kupiga soga na kuendelea na martia arts gym library etc

17:50-18:00 parade rollcall na kumatch kwenda dining

18:00-18:50 chanting offerings kwa Buddha na hungry ghost na kupata dinner

18:50-19:00 parade roll call

19:00-20:50 darasani

20:50-21:50 meditation/chanting

21:50-20:00 kurudi vyumbani kwa kumatch kwenye mistari tena kimya, kuingia vyumbani kuzima taa na kulala
Ukionekana nje baada ya hapo ni majanga

Chuo kiliongozwa na sheria kwenye kila kitu, sheria ya kutumia Maji, kutembea, kuongea kukaa kula kugeuka kulala, kutandika kuvaa etc kila kitu kilikuwa ni sheria na ndio maana wengi sana walishindwa maisha yale
Hii picha ni jinsi tulivyokuwa tunakaa mstarini kila mtu na nafasi yake kwahiyo hata kama haupo nafasi yako inabaki wazi.

View attachment 274159
Mkuu kwa mchanganyiko wa taaluma ulizo nazo...anzisha kitu kama dhehebu lanye mrengo huru la kiafrika zaidi.
Kama kawaida unikumbuke niwe mtunza kapu la sadaq.
 
Back
Top Bottom