Mahimbo kafunga ndoa na Josephine Kanisa la KKKT Kijitonyama ni ndoa ya Kikirsto mkuu, sio ndoa ya kislam usiyoipenda.
Ritz,
Unakumbuka jana nilikuambia usikurupuke kuhusu mambo ya Kanisa Katoliki? Sijui utaacha lini kuaibika na hili.
Kanisa Katoliki halitambui ndoa zilizofungwa kwenye makanisa ya waprotestant kama hili la KKKT na wengine.
ndoa inayoweza kutambulika na inahitaji marekebisho kidogo ni zile zilizofungwa kwenye Makanisa tunayoita Eastern Catholics.
Kwa mfano, pale D'Slaam, ukienda Barabara ya Ali Hassan Mwinyi opposite to Red Cross, kuna Kanisa liitwalo Greek Orthodox Church. Hili pia unalikuta pale Musoma unpoingia mjini unapovuka kituo cha Musoma Bus.
Angekuwa amefungia ndoa huo basi wakatoliki tungesema kuwa ndoa hiyo ni ya Wilbrod Slaa itakuwa ni batili (invalid) na asingepewa kwani hayo makanisa tunasema tunatofautiana lakini yana sakrament kwa sababu ya kitu kigumu sana kwako kiitwacho apostolic succession.
KKKT ni Walutheri na Luther alikuja na theory yake. Aliijua hii apostolic succession lakini akaipuuza na hivyo wakatoliki hatuamini kuwemo kwa sakrament kwenye makanisa ya waprotestant.
Vilevile sisi wakatoliki hatuwaiti hawa walutheri yaani KKKT na wenzao kwamba ni makanisa (Church). Hawa sisi tunawaita Christian Communities.
Najua waprotestant humu JF wanaweza kuchukia labda ninakashifu lakini naomba msome website ya Vatican (Clikc
Here) ikifafanua maswali kama haya hivi:
**********
FIFTH QUESTION:
Why do the texts of the Council and those of the Magisterium since the Council not use the title of "Church" with regard to those Christian Communities born out of the Reformation of the sixteenth century?
RESPONSE:
According to Catholic doctrine, these Communities do not enjoy apostolic succession in the sacrament of Orders, and are, therefore, deprived of a constitutive element of the Church. These ecclesial Communities which, specifically because of the absence of the sacramental priesthood, have not preserved the genuine and integral substance of the Eucharistic Mystery cannot, according to Catholic doctrine, be called "Churches" in the proper sense
Kwa ufafanuzi huu kutoka Vatican, makanisa yote ambayo ni protestant sisi wakatoliki hatuyatambui kama ni makanisa bali ni vikundi vya wakristo.
Naomba mnaojadili post hii, jihakikishieni wenyewe kwa kusoma website ya Vatican na ninairudia hapa tena(Clikc
Here).
Hivyo, mheshimiwa
Ritz,
Umetusaidia sana kutueleza kwamba
Josephine alifungia ndoa KKKT yaani ndoa ya Kiluteri basi umefunga mjadala huu na kwa maana hiyo bila kujijua umemhalalishia Dr. Slaa na
Josephine kufunga ndoa katika kanisa katoliki.
Namalizia kwa kukushauri mara ya tatu. SOma kwanza mambo ya Kanisa Katoliki ili usiumbuke unapojadili mambo ya Kanisa hilo.
BInafsi nilikuwa na mashaka kuhusu ndoa ya kwanza ya Josephine lakini kwa sababu umetaja mwenyewe kuwa alifungia kwenye mkusanyiko ambao nyinyi mnauita Kanisa la KKKT wakati sisi wakatoliki tunafundishwa na Vatican kwamba huo tuuite tu mkusanyiko wa KKKT wala si Kanisa, basi sasa nina uhakika ndoa ya Dr. Slaa na Josephine imo katika ratiba yangu yaani July 21.
Japo sijajua watafungia parokia gani ya Jimbo gani hapa duniani.