A shock of my life, furaha yageuka shubiri. Be good to people on your way up, you might meet them on your way down, mwenzenu leo yamenikuta!


Hili jamaa ni jitu la hovyo, bado linaendelea kumzalilisha Mama wa watu!

Paschal is selfish with no wisdom, kwa nini asingemtafuta wakaongea Lina kuja huku!

Can you imagine? Pascal anataka kusema kama akikosa Hii Kazi, then ni chuki za huyo Mama!

Huwezi kujiamini kwa kiwango hiki but una mblackmail Mama wa watu, na kwa maelezo haya, kufahamika ni jambo rahisi.

I have advice for you Pascal, live a low profile now and struggle kujijenga, uache kuropoka ropoka! It will not help you!!
 
Ni vema umeomba msamaha.Naishia hapo.
 
Paskali jifunze kuwa na subira, si busara kuanza kumtilia shaka hadharani refa wakati wa mechi, umemuweka hadharani huku yeye huenda hana baya lolote kwako, nakushauri habari hii ungeitoa baada ya yote kufanyika na kuhitimishwa.
Mtazamo wangu naomba uuheshimu: Haufai kuwa kiongozi. Hii inatokana na jinsi ulivyojiandika na kujipambanua binafsi.
 
Hii ni mind game, unataka kutuaminisha kuwa ikitokea umekosa basi si kwamba umepungukiwa sifa bali ni revenge. Kwani wewe unafikiri sifa ni zipi? Hiyo pia ni sifa mojawapo maana inakuelezea wewe ni mtu wa aina gani.

Lakini kitendo cha kuandika haya wakati huu ambapo mchakato bado unaendelea pia inakupunguzia sifa.
 
Bwana Paskali,
Niruhusu nami nikupe kisa cha kweli ambacho kidogo kimefanana na chako.

Nilikuwa kijana kama wewe mjanja na ukipenda shule pia ipo ndani na nje na dunia naijua vyema na nina kazi nzuri.

Alhamdulilah.
Nafanyakazi Tanga.

Kitu ambacho kinaweza kukufanya unitazame tukipishana barabarani ni gari yangu kali sana nimeinunua Dubai.

Ikiwa tutapisha kwa miguu na wewe unazijua ''pamba,'' utageuza shingo kuangalia Yve Saint Laurent, Gucci juu kati na chini utatazama pia utakutana na Roland Cartier.

Tanga aina ya gari hizo zilikuwa mbili ya Bohora mmoja mfanya biashara tajiri na gari yangu.

Mashaallah nikipendeza na wakinipenda.
Lakini binadamu unatakiwa uwe binadamu ili ukamllishe utu wako.

Nilikuwa nimekabidhiwa kiwanda cha Coca Cola Tanga cha mzee wangu kilichokuwa kimefungwa mashine zimetolewa yamebaki majengo.

Kazi yangu ikawa kukiangalia kiwanda hadi majengo yatakapopata mnunuzi.
Ndani ya kiwanja kuna nafasi kubwa sana.

Ili kufidia gharama za kulipa umeme, maji na walinzi uwanja huu nikawapangisha wafanya biashara kutoka Kenya na Eritrea kuweka miti inaitwa mikaratusi inayotumika kama nguzo za umeme.

Miti hii hii ilikuwa inanunuliwa pale pale Tanga inahifadhiwa hapo kiwandani kusubiri mzigo uwe mwingi meli ije usafirishwe kwenda nje.

Ghafla wafanya biashara hawa wakapotea kwa muda mrefu mali iko kiwanjani kwangu inalindwa lakini kodi ya pango hailetwi.

Simu, email havijibiwi kiasi cha miaka miwili hivi.

Majengo tukauza shida iliyobakia ilikuwa kwa mali hii kuondoshwa katika ''premises,'' kwa kuwa mnunuzi mpya alikuwa anataka kufunga mitambo mipya ya kutengezeza soda aendelee na biashara yake.

Kisa kirefu kuwa kifupi.

Mnunuzi wa mali ile akapatikana nikauza mali na fedha nikaweka benki nami nikabaki na nyaraka za ushahidi wenyewe watakapojitokeza nikawabidhi fedha zao.

Siku ya pili tu baada ya kukamilisha mauzo yale na kuanza kuondoa mzigo katika kiwanda nikapigiwa simu kuwa natakiwa Polisi Chumbageni.

Ilikuwa Jumapili.
Nikafika.

Nikakutana na askari wawili na kijana mmoja wa KIsomali.

Nikaelezwa kuwa huyo kijana wa Kisomali amekuja kutoa taarifa Polisi kuwa mali yake iliyokuwa kwenye kiwanda ambacho kilikuwa chini ya usimamizi wangu inahamishwa bila idhini yake.

Nikajieleza.

Nikarudi nyumbani kuchukua vielelezo vyote kuonyesha wenye mali ni nani na huyo anaesema ni yake mimi simtambui.

Ikawa sasa kila baada ya siku mbii tatu askari wananiita kituoni na hakuna la maana wanaloniambia ila neno moja tu, ''Hii kesi nyepesi tunaweza kuimaliza mara moja.''

Jibu langu kwao ilikuwa moja, ''Najua kuwa sina kesi yoyote hapa.''

Kumbe nilichokuwa sijui ni kuwa niliwaonyesha fedha za ile mali niliyouza ambazo zilikuwa benki.

Hazikuwa fedha kidogo.

Nilikuwa nimefanya kosa kubwa sana.

Msomali na Polisi wote kwa pamoja walikuwa wanazitaka zile fedha niwachotee kidogo mambo yaishe.

Hawa askari walikuwa wawili na majina yao ninayo.
Nilipojua upuuzi ule nikawa sitoi ushirikiano waliotegemea kutoka kwangu.

Siku moja jioni kabisa ofisi zimefungwa nikapokea simu kutoka Polisi Chumbagani kutoka kwa wale askari kuwa nahitajika kituoni.

Nilipofika nikaelezwa kuwa kesho nafikishwa mahakamani kwa kosa la wizi wa kuaminiwa.

Nilipigwa na butwaa na kwa hakika nilifadhaika kupita kiasi.
Mimi mwizi.

Nilitakiwa nifike mahakamani siku ya pili asubuhi na wadhamini wawili mmoja awe na mali isiyohamishika na mwingine awe na barua ya mwajiri wake.

Asubuhi nimefika mahakamani wadhamini wangu wamenikuta niko katika benchi na watuhumiwa wengine kutoka Jela ya Maweni tumesimamiwa na askari.

Katika ile benchi tuliyokaa kijana mmoja mtoto mdogo umri wa sekondari akanisemesha akaniuliza kama namkumbuka.

Nikamjibu simkumbuki.
Akanieleza vipi tulikutana.

Ukiingia Chumbageni Polisi Mapokezi kushoto kuna ''lockup'' na kijidirisha kidogo cha mahabusi.

Kijana anasema iko siku naingia polisi kaniona akaniita kupitia kile kidirisha tukatazamana na akaniomba hela.

Nilimkumbuka.

Nilimuuliza askari aliyekuwa kasimama pale nje kama naweza kumpa yule mtoto chochote.

Yule askari akaniambia nimpe tu hakuna tatizo.
Nikatoa fedha nikampa yule mtoto.

Ikawa pale mahakamani tayari nimeshapata ndugu.

Huyu kijana akaniambia, ''Ikiwa watauleta Maweni usiwe na hofu mimi nitakuwa nakuchotea maji ya kuoga na kukufuli nguo zako...'' maneno yakawa yanaingia sikio moja yanatokea sikio la pili.

Nilikuwa nimepigwa na mshtuko mkubwa sana.

Najiuliza nimefikaje hapa na katika hali kama hii?
Nilimkatalia hakimu shitaka la wizi wa kuaminika.

Hakimu akapanga siku ya kusikiliza kesi.

Mdhamini wangu wa kwanza akatoa barua kutoka kwa mwajiri wake kunidhamini.

Muongoza Mashtaka akaikubali.
Mdhamini wa pili akatoka hati ya nyumba iko Ngamiani.

Mwendesha Mashtaka akaikataa kisa majina yaliyoko katika hati ni majina ya baba wa mdhamini kwa hiyo hiyo nyumba si yake.

Mtuhumiwa kashindwa kutimiza masharti ya dhamana kwa hiyo atapelekwa Maweni.

Yakatokea mabishano makubwa kati ya mdhamini wangu na Mwendesha Mashtaka.

Hakimu akaingia kati akasema yeye anatoa dhamana kwa mshtakiwa kwa hiyo barua moja iliyofikishwa mahakamani.

Baada ya mahakama kumalizika nikaenda ofisini kwa Hakimu kukamilisha dhamana yangu nikiwa na Mwendesha Mashtaka.

Naingia ofisini Hakimu ananitolea salamu kwa bashasha na kuniuliza kama namkumbuka.

Akaniambia, ''Nilikuwa natoka Dar es Salaam na dereva wangu tunakuja Tanga, tunafika Wami, gari ikatuharibikia Wami.

Wewe ulisimama ukanichukua na gari yako hadi Tanga.''
Nikakumbuka.

Akanipa pole kwa mkasa ule na akaniuliza nini tatizo.
Nikamueleza kila kitu.

Hakimu akamtazama Mwendesha Mashtaka akasema, ''Angalieni haya mambo msije kuvunja heshima za watu kwa mambo ya kipuuzi.''

Nikapata dhamana.
Kisa kirefu tukomee hapa.

Mwendesha Mashataka tukiwa ndani ya majengo ya Mahakama wakati naondola mtu huru kanifuata kuniomba hongo.

Nilimuuliza anataka kiasi gani.
Nilimuuliza kwa kuwa nilitaka kujua thamani yangu kutoka kwake.

Aliniomba shs: 5,000.00.

Nilisikitika kwa kunishusha kiasi kile na nilimuhurumia sana kupita kiasi kwa kujidhalilisha mwisho wa udhalili.

Siku ile haukupita muda mji mzima wa Tanga taarifa zimeenea kuwa nimefikishwa mahakamani na Msomali kwa ''wizi wa kuaminiwa.''

Watu hawakuamini kuwa mimi naweza kuwa mwizi.

Jamaa wakamfuata na swali moja tu walikuwa wanamuuliza, ''Wewe unamjua vizuri Mohamed Said?''

Msomali aliingia hofu na naamini aliwaambia wale askari washirika wake kuwa mtego wao umekamata chui badala ya swala.

Mtego uliokamata chui unatisha hakuwa wa kuusogelea.

Hawakunipigia simu tena.
Sasa narudi kwako ndugu yangu Paskali.

Nadhani kipo ulichosoma katika stori hii na kukuongezea funzo.
Umelipwa unachostaili.
 
Asipokusamee inakuwa karma over karma,it may reverse back,msngi wa kusamehe ndio msingi mkuu..! Hivi vitu NI vya akili kubwa Sana tena vya kimungu,LABDA POINT MUHIMU ULIYOIRUKA NI KWAMBA ALIPOKUKUMBUSHA ULIPASWA UMWOMBE KWA YOTE ULIYOYAFANYA ,AKIGOMA KARMA INAKUJA M HIT-YEYE ENDAPO ATAFANYA YASIYOSTAHILI.
 
Kwa hiyo umekuja kumlipua tena!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…