A - Town Gangsters walioitikisa Arusha kwa matukio ya uhalifu

A - Town Gangsters walioitikisa Arusha kwa matukio ya uhalifu

Sabasita Kimaro ambae ni baba yake msanii anaeitwa Tunda anapewaga credit sana kwenye kumaliza haya mambo ya ujambazi na umafia hapa Chugga. Japo wengine wanasema nae alikuwa nyamera tu kama manyamera wengine ila chini ya mwavuli wa upolisi.
 
Sabasita Kimaro ambae ni baba yake msanii anaeitwa Tunda anapewaga credit sana kwenye kumaliza haya mambo ya ujambazi na umafia hapa Chugga. Japo wengine wanasema ane alikuwa nyamera tu kama manyamera wengine ila chini ya mwavuli wa upolisi.
Jamaa amekaa sana moshi then moro,hata issue ya kibiti alikua kwenye mission hiyo
 
Ulimwengu umebadilika utamfanyia ubabe nani zama hizi. Ilikuwa ni wakati KILA mikoa kulikuwa na wababe wako. Tabora Kigoma kulikuwa na mtu hatari sana anaitwa Mussa Chesa miaka ya 90 ameua watu wengi sana kwa ujambazi na uchawi siku hizi ameokoka anatangaza injili anajutia Sana matendo maovu yake. Kaapa kupambana na shetani kwa mda wake wote uliobaki dunia anatoa Siri za uchawi.
Huyu Mussa Chessa yupo wapi kwa sasa?
 
Ngunguli alikuwa na kikosi Kazi enzi hizo chuga umafia tele kwa kifua chake.
Ajabu pamoja na kujulikana kuwa Ngunguli ni jambazi bado akapindishwa cheo na akawa na ukwasi wa kifedha mkubwa, akajenga na misikiti huku kwao mji kasoro bahari hadi sasa hakuna aliyejaribu kumstaki kwa kutumia madaraka vibaya.
 
Miaka ya 80 kuna jambazi aliitwa Nyau, katika mazindiko yake alilishwa moyo wa paka. Akikurukia shingoni alikaba na kurarua kama paka. Huyu jamabazi aliteleza mikononi kwa PGO kama nyoka anavyoteleza mikononi mwa mwanadamu.

Alikua na hirizi hiyo akiivaa risasi zilikua zinapita bila kumdhuru. Alikinukisha Dar na kwenda kujificha Tanga vijijini huko kwa wakwe zake.

Aliuzwa na mke wake, mke wake alikula dili na wajomba kuwa akiwasaidia kumkamata yeye hatakua na hatia. Aliwaambia akiwa amevaa hirizi yake hamuwezi kumkamata.

Basi bwana alikaa ndani muda wote, kuna siku mke wake alimwambia si aende nje akapate fresh air, jamaa alitaka kuvaa hirizi mkewe alimwambia unavaa ya nini si unaemda hapo tu. Kumbe nje wajomba wamezunguka nyumba usawa wa vichaka.

Nyau alikamatwa kizembe sana bila hirizi yake.
Nyau alitokea tabora ingawa alifia tanga
 
Angalau aliwashughulikia wakapotea,kuna moja wasiojulikana walikosea tu timing Tarime, kuna moja Mwanza akalipora bilioni 4 kwenye akaunti yake,jingine lilikimbia sauzi,aliyajua majizi yote kwa sababu alikuwa kwenye system na alijua michezo yao hata alivyodili nao alikuwa na taarifa nao wote. Kuna limoja lilimzulumu mjane nyumba Magu akamsaidia kuirudisha nyumba ikihisiwa alishiriki njama za kumuua mume Ili apate nyumba hii nyumba mme aliikopea, michezo yao siku ya marejesho ya riba yanapotea au kuzima simu Ili yapore nyumba.
Mkwere ndie aliyafuga majizi yakawapiga wageni na wabongo pia, huku yakimwaga pesa kwenye muziki. Mengine yalikufa vifo vibaya. Mengine yanajifanya kujifichia kwenye dini.
Angalau jpm aliyatikisa majizi
Hivi Young Milionea Muzamil Katunzi kaishia wapi nae a;itesa sana enzi za mkwere yeye pamoja na kaka zake mapacha
 
Kwenye simulizi yako umeweka too general ngoja na mimi nielezee kwa ufahamu wangu kuhusu chuga gangsters:
Sadick Mkindi ni legend mtoto wa mzee Mkindi familia maarufu na tajiri Arusha huyo ni mdingi alifanya uhalifu in late 80’s na early 90’s
Majambazi walikuwa kina Chonjo maarufu kwa wizi wa magari, Bob Sambeke, Alex Massawe, Nyari....
Ila kuna hawa magangster wezi na wababe wa mitaani
Alikuwepo Hamis Mtotoo alikuwa anaibia sana wazungu aliuliwa na polisi relini watoto wa Pangani na Bondeni tunamjua vizuri.
Alikuwepo nyokaa alikuwa mwizi hatari katesa sana mianzini, sakina, ilboru na sanawari aliuliwa na polisi sakina
Alikuwepo Tumboniiii alitesa ngulelo, kimandolu kijenge nafkir na yeye aliuliwa na polisi ngulelo
Ngarenaro alikuwepo Mbalulaa alikuwa na mbio hatari akikwapua humshiki
Kuna kundi la wababe hawa hawakuwa wezi ila wababe hatari waliwakosesha raha watu sehemu za starehe kama mawingu club kijenge,roasters garden uzunguni, crystal club, metropole, sabasaba nk miaka ya mwishoni 90 na mwanzoni mwa miaka ya 2000
1. Iddi Mkuluuu (RIP) na kundi lake la Kaloleni gym,huyu bro alikuwa baunsa bonge la mtu mbabe hatari
2. Farijala Athumani(Papaaa) mtoto wa Ngarenaro bdae kijenge alikuwa anapiga kick boxer hatari alikuwa akikupiga kichwa lazima uanguke aliuliwa kwa kuchinjwa pale mtaa wa Jaluo
3.Fredi Jebi na Kabelo walikuwa watoto wa line police fire wababe walikuwa wanapiga gujuruu sio za nchi hii waliwatesa mno watoto wa kishua mjini kina Soican, Yusuph Mirambo, Valee Tango, Alkesh etc. Fredi Jebi alikufa kifo cha ajabu mguu uliota tende na ndio ukawa mwisho wa ubabe wa Kabelo
4.Baba Kisioki “babaaa” alkuwaga bondia na mbabe huko sinoni, lemara, njiro na kijenge ckumbuki nini kilimuua
5.Kingkola alikuwa mbabe hatari alikuwa anchezea timu ya Ngarenaro inaitwa “wayamkali” mpira hauishi kama kingkola hajapiga tiktatka
Wengine ni kina Omary manjiwaa, sele kishugaa pia kulkuwa na dogo aliitwa Regaa au Julius mambwaa alikuwa kapurwa lkn mbabe hatari alikuwa anatembea na mbwa zaidi ya 20.
Makundi maarufu yalikuwepo ka Kossovo chini ya Festo watoto wa Kambi ya fisi, maghoro na makao. Nako2Nako watoto wa kaloleni “Ololoo”, wakudisi watoto wa bongonyoo na Ungaltd kulikuwa na watoto wa blood ring Esso, watoto wa cheka ung’atwe Sombetini. kuna watoto wa Sing’isi walikuwa wanakaa sana tengeru walikuwa ni kwikwi tesa sana watu waliokuwa wnaenda beach party Duluti
Siku hizi haya magenge yamekufa ila waliobaki hatari ni vijana wa “tatu mzuka” wako kokote omba Mungu usikutane nao
Nishawahi kupigwa mabapa party za duluti bila sababu....
***** zao
 
Fred alikuwa my close friend na sikutegemea ule mguu ungemuondoa. Such a brother and good friend. Umenikumbusha mbali sana [emoji22]
 
Ajabu pamoja na kujulikana kuwa Ngunguli ni jambazi bado akapindishwa cheo na akawa na ukwasi wa kifedha mkubwa, akajenga na misikiti huku kwao mji kasoro bahari hadi sasa hakuna aliyejaribu kumstaki kwa kutumia madaraka vibaya.

Kawafanyia ccm Kazi nzuri Sana anakula fadhila kwa sasa.
Aliwajengea waislamu msikiti wakaukataa mikono yake imejaa hatia,machozi ya wajane na yatima yanamlilia.
 
ndio nakwambia hao wotw hapo juu kwa jombi walikua watoto chekechea,ndio nikakwambia badae alikua hata anawapora hao uliowataja na mwisho wakaacha kuiba akaingia front ndio tukio lililommaliza.
Huu ni uongo. Yaani uwapore majambazi wawe wanakuangalia tu several times, wasikuundie hata kamati wakumalize wenyewe. Sentesi hii moja nikii paraphrase "aliwaibia majambazi wa Arusha hadi wakaacha kuiba akaingia front mwenyewe" the the WE NI LIONGO SANA
 
Kuhusu uchunaji ngozi, hizo ni hadithi tu za kuogopesha wasiojua kama hizi zinazosambaa siku hizi kuhusu figo.

Lyimo ni taxidermist na ile nyumba hapo Momela inayovutia hizo hadithi ilikuwa taxidermy workshop yake.
Wasiojua wakiona muda mwingi imefungwa na kusikia harufu ya ngozi za wanyama ndio wakambambikia kuwa ni mchuna ngozi za binadamu.
Na taxidermist ni rare professional hapa nchini unaweza ukasimama na ukawahesabu wenye ujuzi wa aina hii, wengi hawajui taxidermist ni kazi gani well ni ile ya kumrudisha mnyama aliyekufa katika hali ya kama yuko hai huwa kama pambo katika majumba ya watu hasa wenye kipato kikubwa kwa mfano wale wawindaji wanyama pori wakiwauwa hupenda hao wanyama watengenezwa kama walivyokuwa hai na kuuza kwa matajiri kwa mfano utaona wanyama kama simba,chui na wengine wamefanyiwa taxidermy, ni kazi kubwa na inayochukua muda mrefu kwa mfano kumuwamba simba aonekana kama yupo hai na pia madawa yanayotumika ili ngozi istoe wadudu au harufu. Watanzania wengi ni matinoo hujifanya wanajua kumbe hawajui na pia ni wavivu wa kufanya uchunguzi wa kina wa yale tunayoyasikia, tumebaki na uwendawazimu tu wa kusikia udaku wa akina Zuchu anavalishwa pete, misambwanda na ujinga wa akina domo na wenzake wa aina hiyo.
 
Huu ni uongo. Yaani uwapore majambazi wawe wanakuangalia tu several times, wasikuundie hata kamati wakumalize wenyewe. Sentesi hii moja nikii paraphrase "aliwaibia majambazi wa Arusha hadi wakaacha kuiba akaingia front mwenyewe" the the WE NI LIONGO SANA
Umri wako kwanza ndugu,usikute unabishana na babazako hapa.
 
Back
Top Bottom