A-Z yatikisa maonyesho mahala pa kazi Biteko kuzindua kesho rasmi Arusha

A-Z yatikisa maonyesho mahala pa kazi Biteko kuzindua kesho rasmi Arusha

nyamadoke75

Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
93
Reaction score
288
Mwenyekiti wa bodi ya wakala wa usalama na afya mahali pa kazi Adelhelm James Meru ametembelea maonyesho ya mabanda katika viwanja vya General teyre Jijini Arusha kukagua mabanda pamoja na kujionea majukumu ya utekelezaji wa vifaa vinavyo tumika mahala pakazi kwa tahasisi mbali mbali za serikali na zile binafsi.

Akiwa katika viwanja hivyo Mwenyekiti James amefuraishwa na kona uwekezaji mkubwa uliowekwa katika vifaa vya kazi mahala pa kazi kutoka kiwanda cha A- Z ambapo amejionea vifaa mbali mbali vinavyo saidia watumishi katika kutekeleza kazi zao kwa uraisi pia kujikinga na ajali mbali mbali wanapo kua katika majukumu yao ya kila siku viwandani .

Kilele cha Maadhimisho ya kimataifa ya usalama na afya mahala pa kazini ni kesho tarehe 28 mwezi April ambapo mgeni rasmi ni Naibu waziri Mkuu,na waziri wa nishati Doto biteko .

Akitoa ufafanuzi kwa Mwenyekiti wa bodi ya Hosha nchini Eng Harryson Rwehumbiza amesema kwamba kuna tija kubwa katika kuendelea kua na maonyesho hayo kwani yanakutanisha taasisi mbali mbali kujali na kuboresha vifaa vya watumishi mahala pa kazi ambapo ameeleza kwamba pasipo na usalama kwa mtumishi katika eneo la kazi ni vigumu kupata uzalishaji bora wenye soko la ushindani kwa bidhaa zetu na zile zinazo zalishwa nje ya nchi

Kauli mbiu kwa mwaka huu ni ni Athari za mabadiliko ya tabia ya nchi katika usalama na afya kazini Sajili eneo la kazi Osha katika harakati za kupunguza athari hizo .

Mwisho.

20240427_133749.jpg
20240427_133728.jpg
20240427_133711.jpg
20240427_131642.jpg
20240427_133400.jpg
20240427_131444.jpg
20240427_130436.jpg
20240427_130355.jpg
 
Back
Top Bottom