Aache upotoshaji: Universal Health Care haimaanishi Bima ya Afya. 'Universal Health Care Coverage' kwa Tanzania tuko 100% tangia enzi za Mwl. Nyerere

Kapewa ujinga alete humu halafu waliomtuma hawakumsaidia kuutetea.
 
Yeye anataja upumbavu aliofanya kama kujenga uwanja Chato! Hivi kama kweli wewe ni mtanzania mwenye akili unaweza kuona alichofanya Magufuli siyo ujinga? Kama unaona alichofanya ni sahihi basi pole sana! Nasema pole sana!
Magufuli sio malaika, yapo mazuri na mabaya. Na mazuri yamezidi ubaya, ni mgombea bora ukilinganisha na wengine. Nitampa kura yangu kwa kipindi kingine na atashinda kwa kushindo kama kawaida. Pole wewe uliyeishi miaka mitano ya hasira na gubu na utaendelea hivyo hivyo miaka mitano ijayo. Jipangeni upya 2025...this time tunasonga mbele na Magufuli...
 
Kuna baadhi ya hospitali za serikali zimeanza kuwalipisha watoto chini ya umri wa miaka 5, wanawake wajawazito, wazee na watu wenye magonjwa Sugu, hili unalisemaje mkuu?
Yaani ukiwa muumini wa chama lile afu ukaenda mbinguni, basi hakika jehanamu hatoenda mtu.

Majitu yanaona tunavyonyanyaswa na watawala hawa lakini yanapiga kelele kuwafagilia...
 
Lissu mwenyewe kutwa kumtaja magufuli. Sera hana au?
Anazo nyingi tu.

Magufuli ni kiongozi mkuu wa Serikali ya sasa, katika hali ya kawaida tu kama una akili timamu utaonwa lazima wapinzani wamtaje kwa sababu wanatakiwa waseme watafanya nini tofauti na serikali ya magufuli
 
Umekaa kishabiki zaidi hivyo huwezi kuona mbele! Yani mtu anafanya mambo ya kijinga halafu unakuja na utetezi eti siyo malaika!
 
Wewe ulistahili kuitwa Dr. Hakili! Umekikorogs were mpaka basi. Ukweli ni kwamba kwa Lissu huyu nyie na mwenyekiti wenu mpaka mtajamba cheche mwaka huu! Na waliokupa "likes" kwenye huo upupu ni mapopoma!
 
Kwa iyo ulivyo kilaza unamaanisha kila Mtanzania ana bima ya afya????

😂😂😂😂😂 kweli CCM mmeishiwa hoja sasa mnakuja na vichekesho!!!
 
mmeshikwa matako tayari!
 
Unapotosha, kuhakikishiwa UHC ni tofauti na kuwa na UHC. Bado UHC ipo kinadharia zaidi kuliko kiuhalisia, hata hospitali za rufaa tu ni changamoto, achilia mbali huduma bora.
 
LISSU NI MROPOKAJI TU KAMA WENDAWAZIMU WENGINE HANA WATAALAMU WAKUMSHAURI TATIZO ANAJIONA YEYE ANAAKILI KULIKO WATANZANIA WOTE MAPAKA ANASEMA HAKUNA MTANZANIA ANAYEJUWA ENGLISH HATA MIMI NAJUA ENGISH BANA ASITUDHARIRISHE
 
Usimpangie mgombea chochote Cha kuongea ,kwa iyo mkuu wewe unaona una akili nyingi kuliko lissu,tulia tz Kila kitu kinawezekana Kama wanafunzi wanalipa bima ya NHF ya Kama sh elfu 55 why ishindikane kwa watanzania wote
Hata hivyo watu wakiwa huru,wakawa na mazingira mazuri ya kufanya biashara na mzunguko mzuri wa pesa ukawepo watu watalipa iyo bima hata Kama ni sh ngapi
 
Ufafanuzi nzuri. Tanzania kama nchi miundombinu na mfumo mzima bado haujawa tayari kutoa huduma hiyo ya afya.

Kunahitaji kuimarika kiuchumi kwanza na taratibu kuanza kutoa huduma hiyo ya afya. Hivyo basi, ni budi kuimarisha baadhi ya huduma muhimu za kijamii kama vile elimu, maji na nishati, ambazo kimsingi husaidia kuongeza kinga kiafya na kupunguza mahitaji ya matibabu.

Hadi sasa Serikali iliyoko madarakani (ya CCM) inafanya vizuri na ina mipango thabiti kuelekea kwenye "Universal Health Care" (Rejea Ukurasa wa 131-138 wa Ilani ya CCM, 2020 - kiambatanisho)
√ Hongera Dr Akili kwa mada yako ilichochea mjadala. Tuliokuelewa tunaweka nyongeza ya ufafanuzi wako;
√ Quinine, CCM ina Sera, soma ilani, ila CHADEMA sijui, labda iko kichwani kwa mgombea Urais asiye na HOJA ila VIOJA;
√ Anonymeous, Lissu anajisumbua mwenyewe kwa kutokutambua ya kwamba "hajui kuwa hajui". Anajidai na siasa majitaka zinazoendeshwa na chama chake kilicho na viongozi wasiojua maana ya maendeleo. Maendeleo ya watu (km Universal Health Care) hayapatikani pasipokuwa na uchumi imara (maendeleo ya vitu);
√ Pakawa, je, unazijua "health care" za Sweden na Canada kulinganisha na Tanzania, nchi ambayo ndio kwanza inaingia uchumi wakati? Tungenje uchumi wetu kwanza ili ndoto za kuwa na huduma bora kabisa za kijamii kuliko nchi yoyote duniani, ziwe kweli. Incredible na Bila Bika yawahusu;
√ Sky Eclat, tambua tu kwamba huduma ya afya ubora wake unaelekea huko. Kwa mfano, hakuna aliyetarajia Tanzania ingekuwa na miundombinu imara kwa kipindi kifupi kama sasa. Waliokuwa wakienda Mikoa ya Kanda ya Ziwa, walikuwa wakipita Kenya;
√ BAK, ebu onesha kitu kipi hao wanacho copy kwa Lissu. Soma Ilani ya CCM iliyoambatanishwa nawe weka ya CHADEMA kama anayoyasema Lissu yamo. Yawezekana CHADEMA ndio kwanza wanachapisha Ilani yao kuingiza ya Lissu bila ufafanuzi, kwa maana hakuna walichokifanya kitaifa kuhusu huduma ya afya hata kwenye Halmashauri walizoongoza. Kumbuka ofisi ya chama haijajengwa pia, sembuse kujua maana ya maendeleo?;
√ G Sam dharau ya Lissu dhidi ya Rais aliyeko madarakani ni utovu mkubwa nidhamu ambao ni dalili dhahiri ya tabia ya udikteta. Akipata madaraka ya Urais, hiyo "Universal Health Care" yake itabaki kuwa agenda ya kwenye jukwaa la kampeni;
√BLACK MOVEMENT, tambua kwamba huduma za jamii, ikiwemo afya, zinaboreshwa na Serikali kwa kutumia pia pesa ya mifuko ya hifadhi kuelekea "Universal Health Care". Wanufaikaji pia ni hao hao wachangiaji.

Kutokujua jambo ni kama usiku wa giza.View attachment ILANI YA CCM 2020.pdf
 
Naona Bashiru alivyo waambia UVCCM mjibu hoja za upinzani mkakurupuka. Baba 'enu Meko kashindwa kuzijibu nyie ndio mtaweza?

Kama hiyo UHC ipo na inatekelezwa, ukiachana na maelezo uliyotoa ambayo sitayajibu kwa kuwa wewe mwenyewe unaonekana huyaelewi, kamuulize Meko kwa nini wameanza kuzungumzia issue ya bima ya afya kwa wakulima tena?
 
MWISHO WA YOOTE TUNDU LISSU KWA HAKIKA NI CHAGUO LA WANANCHI...hata kama figisufigisu zitatokea...AMANI ichukuwe nafasi yake na HAKI itafutwe.
Mwenyezimungu ndiye mjuzi.
 
Kweli msomi Dr. unaweza kusema hamna mTanzania anakufa au anakosa huduma ya afya kwa sababu hana pesa? Huduma inayojumuisha pia dawa? Unasema haya with a straight face bila chembe la aibu! Kweli wasomi mna shida.

Amandla...
 
Mkuu wewe ndiye uliyemtafsiri katika namna ya upotoshaji, kisha na wewe ukaamua kupotosha kivyako! Unasema kwake yeye anamaanisha hivyo, Je ulimuuliza akakwambia anamaanisha hivyo au wewe ndiye umemaanisha hivyo?
Kwa hiyo migawanyiko ya utitiri wa bima za afya na mashirika yanayofanya hiyo biashara ndipo shida kubwa ipo hapo! Kwanini zisifumuliwe zote tukawa na mfumo mmoja tu wa bima ya afya kwa wote? Binadamu wote tunapopata marfadhi tunadhurika katika namna inayofanana, wewe hapo ukiugua tumbo utahara vilvile itakavyokuwa kwangu, Je kwanini sasa tuwe na standard tofauti za huduma zetu wakati matatizo yetu yanafanana efect zake?
Mie nafkiri kama kweli taifa letu linazingatia haki na usawa, basi wote tuwe na fursa sawa katika suala afya sio wengine hata akiumwa mafua anapelekwa India wakati wengine anakuwa na tatizo kubwa kabisa la kiafya lakini anbakia kuhangaika huku na kule akiomba wasamalia wema kumsaidia hii haijakaa sawa! Binafsi naikubali sana hii sera ya Lissu itasaidia wananchi wengi sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…