Aache upotoshaji: Universal Health Care haimaanishi Bima ya Afya. 'Universal Health Care Coverage' kwa Tanzania tuko 100% tangia enzi za Mwl. Nyerere

Kagame alicopy Tz? Acha utani mkuu. Model ya bima ya Rwanda haifanani kabisa na Tanzania.
Kule michango imegawanywa kwa thresholds 6 na band ya chini kabisa inalipiwa 100% na serikali. Vipi Tz hao waliopo chini ya poverty line wangapi wanalipiwa bima na serikali kma Rwanda?

Kuna vitu vipo wazi kabisa, suala la bima bado sana kwa tabaka zote hapa Tz. Mama ntilie tu na wamachinga/bodaboda hvi wangapi wana hifadhi za jamii/Bima za Afya?? Hiyo 100% inatoka wapi?
 
1. Unasema kiuchumi hatupo tayari je nchi kma Rwanda tuliozidi GPD mara 7 imewezaje? Mbona Lissu kasema tukianzisha sovereign wealth fund kma ya Norway let's say kwa gesi inayochimbwa au mrabaha kwenye madini hatuwezi fund hiyo mifuko? Kwanini wengine waweze sisi tushindwe?

2. Nimesoma hizo kurasa 130-138 sijaona popote CCM wameweka strategy ya kufikia Bima kwa wote. Zaidi ya vague sentence inayosema kupanua wigo wa NHIF na CHF kutoa bima kwa watanzania wote...... Just that sasa ni wapi huko ulitaka tusome kuhusu mipango kabambe ya CCM kuleta bima kwa wote?
 
1. Kwa nini tuwe na mifuko ya bima ya afya mingi hivyo wakati inaserve the same purpose? Yaani kwa sasa ipo mifuko minne, wanataka kuleta watano wa wakulima baadae wa wafugaji kisha utakuja wa wafanya biashara, then uje wa wasanii nk nk. Tutakuwa na mifuko mingapi hadi tumalize makundi yote ya jamii?

2. Unafahamu kama kwa mifuko hii ya bima mnufaika anapata tu baadhi ya tiba na tiba zingine atatakiwa kujigharamia tena? Kwa nini tusiwe na bima (UHC anayoisema Lissu) ambayo ni kwa wote na haichagui ugonjwa wa kutibu? Kwa nini tuwe na mifuko ya bima inayowachagulia wateja wake waugue nini na watibiwe nini?

3. Unafahamu kwamba hata tu hayo matibabu machache tena ya magonjwa ya kawaida bado wanufaika wa bima wanalazimika kununua dawa pia kwa gharama zao kutokana na usanii wa serikali wa kutopeleka dawa kwenye maeneo ya tiba huku wakiwa wamelipia bima pia?

4. Unazungumzia fao la kujitoa, unaelewa maana yake? Yaani kwa akili yako mtu asilipwe fao la kujitoa kisa ataendelea kupata bima ya afya? Yaani kwako bima ya afya na fao la kujitoa ni kitu kimoja? Kawaite mabwana zako waje kujibu wewe ni mweupe sana bado.

5. Unapozungumzia masuala ya asilimia hakikisha unaelewa unacho kiongea kabla hujaja kumwaga pumba zako hapa.

Unaposema watoto na wanafunzi ambao ni 40% ya population yote wanaweza pia kunufaika na NHIF kisha unasema 70% ya rural population inaweza kunufaika na mfuko wa CHF wewe mwenyewe unaelewa unacho kisema? Yaani hiyo 40% haina ndani yake rural population na kwenye hiyo 70% ya wakulima haina watoto ndani yake? Huoni unajichanganya mwenyewe?
 
Canada ni nchi tajiri sana ukiilinganisha na Tanzania. Population ya Canada ni watu million 37 tu. Tanzania tupo watu million 60.

Kama wewe huko Canada unapewa bure hiyo bima ya afya (kwenu mnaiita universal healthcare insurance) maana yake ni kuwa mzigo wote wa huduma za afya kwa raia wa Canada unabebwa na serikali yenu ya Canada kupitia vyanzo vyake vya kawaida vya mapato (general taxations zingine za government revenues).

Canada inaliweza hilo. Nchi zingine nyingi hazina uwezo huo. Amerika ambayo population yake ni millioni 331.4 haina uwezo huo. Utajiri wa Amerika unamilikiwa na idadi ndogo ya mabillionea; kutoa free universal health insurance kwa waamerika wote millioni 331.4 bila kuathiri shughuli zingine za nchi maana yake inabidi hao mabillionea wachache wapandishiwe kodi mara dufu au zaidi, kitu ambacho mabillionea hawa (akiwemo billionea Trump mwenyewe) katu hawawezi kukubali.
Obama alianzisha Obamacare ambayo matajiri hawakuipenda na alipoingia madarakani Trump aliifyekelea mbali.

Ninachosema ni kwamba hata sisi enzi za Mwalimu serikali ilikuwa inatoa huduma hizi bure kwa wote. Ni kweli huduma hizo zilikuwa duni ukilinganisha na zile zilizokuwa zinatotolewa kwenye nchi tajiri lakini hilo haliondoi dhana ya universal health care tuliyokuwa tunaitoa kwa kiwango cha 100% coverage.

Ninachosema ni kwamba hadi sasa asilimia isiyopungua 70% ya gharama za matibabu zinabebwa na serikali na mgonjwa ( direct or kupitia bima yake) anagharimia kiasi kisichozidi 30% unless yeye ameamua huduma ya private service. Serikali inagharimia pia mishahara na posho mbali mbali za watoa huduma wa afya na kwa kiasi kikubwa dawa na vifaa tiba na mambo mengine kupitia bajeti ya wizara ya afya.
 
unasema watu hawafi kwa kukosa huduma za afya? sikiliza Redio Free Afica kila jumapili asubuhi (nadhani saa 4) , usikilize watu wanavyoteseka kwa kushindwa kulipia huduma za afya. Walipa kodi wanaomba misaada kwa wasamaria wema.
 
Swali jingine ninalojiuliza, kama serikali inachangia 50% kwenye mfuko wa NHIF ( ambayo ni kwa ajili ya waajiriwa) kumbuka mchango wa serikali ni kutoka kwa kodi ya wananchi wote. Je kwa mifuko ya kijamii CHF, serikali inachangia nini?
 
Mnateseka sana asee....
 
unasema watu hawafi kwa kukosa huduma za afya? sikiliza Redio Free Afica kila jumapili asubuhi (nadhani saa 4) , usikilize watu wanavyoteseka kwa kushindwa kulipia huduma za afya. Walipa kodi wanaomba misaada kwa wasamaria wema.
Hao aidha hawaujui utaratibu wa kupata msamaha au wana malengo wanayoyajua wenyewe na hao wenye hizo TV stations. Haijatokea hata siku moja tv yetu ya taifa (TBC1) wakatoa matangazo kama hayo.

Ni jukumu letu kuwaelimisha kama hawajui. Halafu kuna dhana potofu kwamba kila ugonjwa unatibika. Ukweli ni kuwa kuna magonjwa mengi tu hayana tiba, hata ukienda nje ya nchi unapoteza pesa na muda bure. Kwa hiyo mtu alishaambiwa na madaktari kuwa ugonjwa wako hauna tiba po pote duniani, kesho yake utamuona startv akiomba achangiwe pesa ya kuenda India.
 
Swali jingine ninalojiuliza, kama serikali inachangia 50% kwenye mfuko wa NHIF ( ambayo ni kwa ajili ya waajiriwa) kumbuka mchango wa serikali ni kutoka kwa kodi ya wananchi wote. Je kwa mifuko ya kijamii CHF, serikali inachangia nini?
Waajiriwa wa serikali hukatwa 3% hadi 6% ya mishahara yao kila mwezi ambazo hupelekwa kwa mfuko wa NIHF. Hivyo wapo watumishi wengi tu wa serikali ambao kila mwaķa wanalipa shs 3 million kwenye mfuko huo. Watake wasitake makato hayo ni ya lazima kwa mjibu wa sheria. Serikali haichangii 50% ya mfuko huo.
 
Tunatoa elimu. Ni kazi yetu kukupa elimu wananchi wote wasiyoyajua mambo haya akiwemo TL. Siyo kwamba tunateseka. Ni kazi.
Hizo porojo hamna elimu yoyote. Serikali ya kilaghai hii mnalipwa kutetea ujinga
 
na band ya chini kabisa inalipiwa 100% na serikali. Vipi Tz hao waliopo chini ya poverty line wangapi wanalipiwa bima na serikali kma Rwanda?
Mbona wewe mgumu kuelewa? Nimekuambia wale wasiyo na uwezo (masikini) wanapewa msamaha wa kutolipa cho chote. Maana yake ni kuwa wanalipiwa na serikali 100%. Au wewe tu unataka neno bima lionekane ndiyo uelewe kuwa umelipiwa hayo matibabu?
 
Wishful thinking. Watu hawaendi hospitali kwa sababu hawana pesa ya kadi itakayowaruhusu kumuona daktari. Hiyo ndio hali ambayo raia wengi wa vijijini wanayo. Raia ambao wakipata 1000 kwa siku wataimudu vipi hiyo Caesarian ya shilingi 150000 ambayo wewe unaona ni bei nafuu? Badala ya kumponda Lissu kwa kutoa mategemeo ya makusanyo ya baadae, kakae na wananchi wa kawaida usikie machungu yao. Hao ndio wanaojaa kumsikiliza Lissu kwa sababu angalau anaonekana kuyaelewa. Watu wanachohitaji ni tiba na madawa kwa gharama watakayoimudu na si taarifa ya kuwa mmefanya mliyofanya bila kuomba mkopo. Kwa maneno mengine haijalishi rangi paka, kinachothaminiwa ni kuwa anakamata panya.

Amandla...
 
Mwambie huyoo msisiemu
 
Kuna baadhi ya hospitali za serikali zimeanza kuwalipisha watoto chini ya umri wa miaka 5, wanawake wajawazito, wazee na watu wenye magonjwa Sugu, hili unalisemaje mkuu?
Ni jukumu la madiwani na wabunge tutakaochagua kudhibiti hali hiyo. Wahusika wanapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Ni kazi ya serikali za mitaa.
 
Hii ndio shida ya ccm wote, walikua wanamuona Magufuli kama Mungu. Kwakua kila amri aliyoitoa kwa kila MTU na kila Taasisi ilitekelezwa kwa haraka na kwa woga. Sasa yuko kwenye kampeni anakosolewa,anapingwa na kupigwa vijembe ..Mnasema anamtukana na kumdharau Magufuli.

Hivi kuna dharau kubwa kama kuwasema vibaya watu waliopatwa na maafa ambako jiwe amefanya mara nyingi?
Dharau kwa wabunge wa upinzani,maneno machafu alokua anawaambia watu hadharani.
Leo kapata MTU wa kumjibu,kumuonya na kumwelekeza mnalalamika.
 
Acha upuuzi.. nenda rwanda hapo kajifunze.. acha kukopi kwenye mitandao.
 
Awamu ya tano imeharibu kabisa mifumo.. wao kujisifia tuu na majengo.
 
Acha upuuzi.. nenda rwanda hapo kajifunze.. acha kukopi kwenye mitandao.
Rwanda yenyewe imekopi kwetu. Sisi tuliunda mfumo huu miaka ya 1991 wakati huo wanyarwanda wakiwa buisy wakitwangana wenyewe kwa wenye na sisi tukiwa wasuluhishi wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…