Aache upotoshaji: Universal Health Care haimaanishi Bima ya Afya. 'Universal Health Care Coverage' kwa Tanzania tuko 100% tangia enzi za Mwl. Nyerere

Aache upotoshaji: Universal Health Care haimaanishi Bima ya Afya. 'Universal Health Care Coverage' kwa Tanzania tuko 100% tangia enzi za Mwl. Nyerere

Hata Stiglers gauge ilikaa kwenye makaratasi miaka zaidi ya 30 hadi alipopatikana Ngosha na mambo yakawa reality. Huyo Ngosha akipewa miaka mingine 5 haya yote yaliyomo kwenye makaratasi lakini utekelezaji wake unasuasua yatakuwa reality. Hao wengine hamna kitu.

Kumbuka kuwa Kagame ali copy makaratasi yetu haya akaenda kuyatekeleza kwake Rwanda na sasa Rwanda inasifika kuwa na mfumo bora wa bima ya afya na Universal healthcare.
Kagame alicopy Tz? Acha utani mkuu. Model ya bima ya Rwanda haifanani kabisa na Tanzania.
Kule michango imegawanywa kwa thresholds 6 na band ya chini kabisa inalipiwa 100% na serikali. Vipi Tz hao waliopo chini ya poverty line wangapi wanalipiwa bima na serikali kma Rwanda?

Kuna vitu vipo wazi kabisa, suala la bima bado sana kwa tabaka zote hapa Tz. Mama ntilie tu na wamachinga/bodaboda hvi wangapi wana hifadhi za jamii/Bima za Afya?? Hiyo 100% inatoka wapi?
 
Ufafanuzi nzuri. Tanzania kama nchi miundombinu na mfumo mzima bado haujawa tayari kutoa huduma hiyo ya afya.

Kunahitaji kuimarika kiuchumi kwanza na taratibu kuanza kutoa huduma hiyo ya afya. Hivyo basi, ni budi kuimarisha baadhi ya huduma muhimu za kijamii kama vile elimu, maji na nishati, ambazo kimsingi husaidia kuongeza kinga kiafya na kupunguza mahitaji ya matibabu.

Hadi sasa Serikali iliyoko madarakani (ya CCM) inafanya vizuri na ina mipango thabiti kuelekea kwenye "Universal Health Care" (Rejea Ukurasa wa 131-138 wa Ilani ya CCM, 2020 - kiambatanisho)
1. Unasema kiuchumi hatupo tayari je nchi kma Rwanda tuliozidi GPD mara 7 imewezaje? Mbona Lissu kasema tukianzisha sovereign wealth fund kma ya Norway let's say kwa gesi inayochimbwa au mrabaha kwenye madini hatuwezi fund hiyo mifuko? Kwanini wengine waweze sisi tushindwe?

2. Nimesoma hizo kurasa 130-138 sijaona popote CCM wameweka strategy ya kufikia Bima kwa wote. Zaidi ya vague sentence inayosema kupanua wigo wa NHIF na CHF kutoa bima kwa watanzania wote...... Just that sasa ni wapi huko ulitaka tusome kuhusu mipango kabambe ya CCM kuleta bima kwa wote?
 
1. Kwa nini tuwe na mifuko ya bima ya afya mingi hivyo wakati inaserve the same purpose? Yaani kwa sasa ipo mifuko minne, wanataka kuleta watano wa wakulima baadae wa wafugaji kisha utakuja wa wafanya biashara, then uje wa wasanii nk nk. Tutakuwa na mifuko mingapi hadi tumalize makundi yote ya jamii?

2. Unafahamu kama kwa mifuko hii ya bima mnufaika anapata tu baadhi ya tiba na tiba zingine atatakiwa kujigharamia tena? Kwa nini tusiwe na bima (UHC anayoisema Lissu) ambayo ni kwa wote na haichagui ugonjwa wa kutibu? Kwa nini tuwe na mifuko ya bima inayowachagulia wateja wake waugue nini na watibiwe nini?

3. Unafahamu kwamba hata tu hayo matibabu machache tena ya magonjwa ya kawaida bado wanufaika wa bima wanalazimika kununua dawa pia kwa gharama zao kutokana na usanii wa serikali wa kutopeleka dawa kwenye maeneo ya tiba huku wakiwa wamelipia bima pia?

4. Unazungumzia fao la kujitoa, unaelewa maana yake? Yaani kwa akili yako mtu asilipwe fao la kujitoa kisa ataendelea kupata bima ya afya? Yaani kwako bima ya afya na fao la kujitoa ni kitu kimoja? Kawaite mabwana zako waje kujibu wewe ni mweupe sana bado.

5. Unapozungumzia masuala ya asilimia hakikisha unaelewa unacho kiongea kabla hujaja kumwaga pumba zako hapa.

Unaposema watoto na wanafunzi ambao ni 40% ya population yote wanaweza pia kunufaika na NHIF kisha unasema 70% ya rural population inaweza kunufaika na mfuko wa CHF wewe mwenyewe unaelewa unacho kisema? Yaani hiyo 40% haina ndani yake rural population na kwenye hiyo 70% ya wakulima haina watoto ndani yake? Huoni unajichanganya mwenyewe?
Nimekuambia hizi bima ni kwa ajili ya kumrahisishia mtanzania kulipia hiyo cost share yake atakapokuwa mgonjwa na kulazimika kwenda kutibiwa.

Nimekuambia hadi sasa zipo bima za afya nne zinazomilikiwa na serikali (publically owned) kila moja ikiwa na target population yake kwa ifuatavyo:
1. NIHF - target population yake ni watumishi wa umma na wategemezi wao (compulsory). Mtu mwingine anaruhusiwa kujiunga (voluntary). Bima hii ni comprehensive na gharama ya premium zake ni kubwa - Tsh 1.5 million kwa mwaka lakini serikali imeruhusu watoto na wanafunzi kulipa TSh 50,000 tu kwa mwaka. Kumbuka kuwa watoto na wanafunzi idadi yao ni 40% of the total population of Tanzania.

2. CHF: target population ni rural population households. Ni bima ya hiari. Kila household hulipia Shs 10,000 tu kwa mwaka ambayo huwezesha wote walio kwenye house hold hiyo kupata tiba kwenye ngazi ya zahanati, kituo cha afya na hospitali ya wilaya. Kumbuka kuwa rural population is about 70% of the total population of Tanzania.

3. TIKA: mfumo wake ni sawa na wa CHF ila target population yake ni urban household.

4. SHIB: Target population ni wanachama wote wa mfuko wa pensheni ya NSSF pamoja na wategwmezi wao. Kumbuka kwamba ni takwa la kisheria wote walio kwenye ajira rasimu wanapaswa kukatwa asilimia fulani ya mishahara yao na mwajili kutoa kiasi hicho ambazo hupelekwa kwenye mfuko wa NSSF kama pensheni ya uzeeni. Kiasi fulani cha pesa hiyo NSSF hutumika kama bima yao ya afya pamoja na wategemezi watu. Halafu mijitu mingine inataka fao la kujitoa. Ukijitoa na hiyo ba yako ya afya utakuwa umejitoa.

5. Sasa kuna ubaya gani kuongeza wigo wa bima hizi za afya? Kuna ubaya gani kuwa pia na bima ya afya ya wakulima ambayo target population yake ni wakulima wanaokuja kuuzaazao yao ya biashara kama pamba, kahawa na korosho? Premium ya bima yao inakatwa kwenye gharama ya mazao yao kwa hiari yao? Vivyo hivyo kwa makundi mengine eg bodaboda, wafanyabiashara na wajasiliamali wengine kwa hiari yao?

Hizi ndizo mbinu pekee zitakazowezesha kila mtanzania kuwa na bima ya matibabu. Si zile mbinu za huyu mgombea za kuenda ku copy ubelgiji na ku paste tanzania.
 
Mimi ni Mtanzania ninaye ishi Canada. Universal Health care ni bima ya afya ambayo kila mkazi anapewa na serikali. Kwa miaka ambayo nimeiishi Canada, sijawi lipia matibabu wala familia yangu kulipia matibabu. Kusema ukweli gharama za elimu na matibabu ni cost za serikali. Tena kwa watoto gharama za elimu ni free mpaka school bus za kuwapeleka mashuleni na kuwarudisha. Nakuwekea maelezo hapo chini usome na nakuwekea na link yake.

Healthcare in Canada is delivered through the provincial and territorial systems of publicly funded health care, informally called Medicare.[1][2] It is guided by the provisions of the Canada Health Act of 1984,[3] and is universal.[4] Universal access to publicly funded health services is often considered by Canadians as a "fundamental value that ensures national health care insurance for everyone wherever they live in the country.

link;

Healthcare in Canada - Wikipedia
Canada ni nchi tajiri sana ukiilinganisha na Tanzania. Population ya Canada ni watu million 37 tu. Tanzania tupo watu million 60.

Kama wewe huko Canada unapewa bure hiyo bima ya afya (kwenu mnaiita universal healthcare insurance) maana yake ni kuwa mzigo wote wa huduma za afya kwa raia wa Canada unabebwa na serikali yenu ya Canada kupitia vyanzo vyake vya kawaida vya mapato (general taxations zingine za government revenues).

Canada inaliweza hilo. Nchi zingine nyingi hazina uwezo huo. Amerika ambayo population yake ni millioni 331.4 haina uwezo huo. Utajiri wa Amerika unamilikiwa na idadi ndogo ya mabillionea; kutoa free universal health insurance kwa waamerika wote millioni 331.4 bila kuathiri shughuli zingine za nchi maana yake inabidi hao mabillionea wachache wapandishiwe kodi mara dufu au zaidi, kitu ambacho mabillionea hawa (akiwemo billionea Trump mwenyewe) katu hawawezi kukubali.
Obama alianzisha Obamacare ambayo matajiri hawakuipenda na alipoingia madarakani Trump aliifyekelea mbali.

Ninachosema ni kwamba hata sisi enzi za Mwalimu serikali ilikuwa inatoa huduma hizi bure kwa wote. Ni kweli huduma hizo zilikuwa duni ukilinganisha na zile zilizokuwa zinatotolewa kwenye nchi tajiri lakini hilo haliondoi dhana ya universal health care tuliyokuwa tunaitoa kwa kiwango cha 100% coverage.

Ninachosema ni kwamba hadi sasa asilimia isiyopungua 70% ya gharama za matibabu zinabebwa na serikali na mgonjwa ( direct or kupitia bima yake) anagharimia kiasi kisichozidi 30% unless yeye ameamua huduma ya private service. Serikali inagharimia pia mishahara na posho mbali mbali za watoa huduma wa afya na kwa kiasi kikubwa dawa na vifaa tiba na mambo mengine kupitia bajeti ya wizara ya afya.
 
unasema watu hawafi kwa kukosa huduma za afya? sikiliza Redio Free Afica kila jumapili asubuhi (nadhani saa 4) , usikilize watu wanavyoteseka kwa kushindwa kulipia huduma za afya. Walipa kodi wanaomba misaada kwa wasamaria wema.
 
Swali jingine ninalojiuliza, kama serikali inachangia 50% kwenye mfuko wa NHIF ( ambayo ni kwa ajili ya waajiriwa) kumbuka mchango wa serikali ni kutoka kwa kodi ya wananchi wote. Je kwa mifuko ya kijamii CHF, serikali inachangia nini?
 
Huyu mgombea kila kukicha anawapotosha wananchi kwa kuwaeleza mambo ambayo si sahihi. Anaongea mambo ambayo hayajui na hana utalaamu nayo. Hana wataalamu wa kumshauri ukweli wa kile anachokusudia kuwaeleza wananchi.

Moja ya upotoshaji anasema ni kuwa akichaguliwa atawaletea watanzania wote Universal health care. Ukimsikiliza utagundua kuwa kwake universal health care maana yake ni bima ya taifa ya afya kwa wote. Utagundua kuwa bima ya afya yataifa kwake ni NIHF tu. Hajui kuwa kuna bima zingine za afya za taifa kama CHF, TIKA, SHIB ya NSSF na kadhalika. Hajui kwamba kuna makampuni binafsi zaidi ya saba nchini yanayotoa bima ya afya. Hajui kwamba hadi sasa mzigo mkubwa wa gharama ya matibabu ya watanzania bado unabebwa na serikali kupitia mapato yake ya kodi kwa ujumla (government revenue)

Ukweli ni kwamba:
1.
Universal health care a.k.a universal health coverage (UHC) is a health care system in which all residents of a particular country are assured access to health care. The World Health Organization describes it as a situation where all citizens of a particular country can access health services without incurring financial hardship.

Maana yake ni kwamba UHC ni mfumo wa serikali unaohakikisha raia wake wote wanapata huduma za afya. UHC ni sera ya nchi na mfumo wake unatekelezwa kwa kuundiwa sheria kanuni na taratibu za utekelezaji.

2. Tangia enzi za Mwalimu Nyerere raia wote wa Tanzania walikuwa wanapata huduma za afya bila kulipa chochote. Gharama zote zilibebwa na serikali kupitia mapato yake ya kodi (TRA) na yasiyokuwa ya kodi (government revenues). Sisi tuliyaita matibabu ya bure. Hivyo universal health care coverage ilikuwa 100% kwa gharama ya serikali ya 100% kupitia bajeti yake ya wizara ya afya.

3. Kufikia miaka ya 1990s, kutokana na ongezeko la watu (population) na ongezeko la gharama za tiba kufuatana na teknolojia za kisasa za tiba zenye gharama kubwa, serikali yetu (kama zingine duniani) ilielemewa na mzigo huu wa kutoa huduma bure kwa wote.
Hivyo kwa sababu hizo lakini bila kuathiri universal health care policy, serikali ilibadilisha kidogo mfumo huo kwa kuanzisha utaratibu wa health cost sharing kwa wale wenye kauwezo. Kwa utaratibu huu mgonjwa alitakiwa kuchangia asilimia kidogo ya gharama ya matibabu yake. Gharama kubwa ilibebwa na serikali.

Kwa wale ambao hawana uwezo kabisa wa kuchangia serikali iliweka utaratibu wa kuwasamehe. Makundi yafuatayo hayakusika na utaratibu huu wa cost sharing (hadi sasa): Watoto wote walio chini ya miaka mitano, mama wajawazito, wenye umri unaozidi miaka sitini, wenye magonjwa ya kansa, kifua kikuu, HIV na magonjwa mengine sugu. Hawa bado serikali inabeba gharama zao za matibabu kupitia bajeti yake ya walipa kodi wote nchini. Pia kwa magonjwa ya dharura mtoa huduma analazimishwa kutoa huduma kwanza, masuala ya kiasi gani mgonjwa achangie ataulizwa baada ya kupona na kama hatakuwa na uwezo huo utaratibu wasamaha utafuata baada ya kupona.

Hivyo hata baada ya kuanzisha cost sharing mfumo ulihakikisha universal health care kwa raia wote kwa serikali kubeba most of the cost. Ingawa kiwango cha hii cost sharing ya mgonjwa imekuwa ikiongezwa kidogo kidogo lakini hadi sasa burden kubwa bado inaendelea kubebwa na serikali. Kwa mfano gharama ya operesheni ya Caesarian Section huko Amerika ni USD 18,000 ambayo ni sawa na takribani Tsh 40 million lakini sisi hapa cost anayopaswa kuchangia mgonjwa haizidi Tshs 150,000/ na kama ni ya uzazi ni bure na kama hana uwezo anasamehewa au analipa kidogo ya hiyo. Inayobaki serikali inabeba kuhakikisha hakuna raia wake atakayekufa kwa kukosa uwezo wa kulipia gharama hizo. Hence 100% universal health coverage.

Dhana na chimbuko la bima za afya (Evolution of other health care financing in Tanzania):
Ili kurahisisha na kupunguza buguza/ changamoto ulipwaji wa hizo cost sharing kwa upande wa mgonjwa serikali iliunda bima za afya za taifa (public owned health insurance schemes:

1. The National Insuranse Health Fund (NIHF) ilianzishwa mwaka 1999 (Act of Parliament No. 8 of 199 -CAP 395 RE 2002) kwa ajili kwa waajiriwa wa serikali - government workers. Kila mwajirwa wa serikali alilazimika kukatwa 3% ya mshahara wake kila mwezi na serikali kutoa kiasi hicho hicho kutoka vyanzo vyake vingine vya mapato hivyo kupata 6% ya mshahara na kuuweka kwenye huo mfuko wa bima wa taifa. Mchango huo unamuwezesha mtumishi huyo pamoja na mwenza wake, watoto wao wasiozidi 4 wenye umri usiozidi miaka 18 na wazazi wake wawili - jumla watu sita kupata matibabu kwa gharama ya mfuko huo wa NIHF.

NB: - Waajiri na waajiriwa binafsi hawalazimiki kisheria kwa sasa kujiunga na mfuko huu. Ni wa hiari kwao.
- hulipa Shs 50,000 tu kwa mwaka kuwa wanachama wa mfuko huu.

2. Community Health Fund (CHF): Walengwa hasa wa mfuko huu ni wakazi wa vijijini. Ni mfuko wa hiari. Kila kaya hulipa Sh 10,000 tu kwa mwaka ambayo huwezesha mkuu wa kaya pamoja na watoto wao wote wenye umri chini ya miaka 18 kupata matinabu kwenye ngazi ya zahanati, kituo cha afya hadi hospitali ya wilaya bila mchango mwingine.

3. TIKA (Tiba kwa Kadi): Huu unafanana na ule wa CHF, tofauti hapa ni kaya zilizo mjini.

4. SHIB - ni Social health insurance benefit ulio chini ya National Social Scurity Fund (NSSF).

Ukiacha hizo mifuko aina 4 za bima za afya za kitaifa pia yapo makampuni zaidi ya saba yanayoendesha private health insuranses eg AAR, Strategy etc. Pia bima za maisha zinazotolewa na bima za kawaida huwa zina health insurance.

Mgombea huyo anapaswa kujua basics hizi badala ya kujifanya much know na kuanza kupotosha wananchi kwamba wataletewa UHC kutoka ubelgiji. Hiyo Obamacare haifiki ya kwetu kwa ubora na kwa coverage. UHC coverage ya kwetu bado ni 100%. Hakuna anayekosa matibabu au kufa kwa sababu hana pesa. Nchi zingine haziko hivyo.
Mnateseka sana asee....
 
unasema watu hawafi kwa kukosa huduma za afya? sikiliza Redio Free Afica kila jumapili asubuhi (nadhani saa 4) , usikilize watu wanavyoteseka kwa kushindwa kulipia huduma za afya. Walipa kodi wanaomba misaada kwa wasamaria wema.
Hao aidha hawaujui utaratibu wa kupata msamaha au wana malengo wanayoyajua wenyewe na hao wenye hizo TV stations. Haijatokea hata siku moja tv yetu ya taifa (TBC1) wakatoa matangazo kama hayo.

Ni jukumu letu kuwaelimisha kama hawajui. Halafu kuna dhana potofu kwamba kila ugonjwa unatibika. Ukweli ni kuwa kuna magonjwa mengi tu hayana tiba, hata ukienda nje ya nchi unapoteza pesa na muda bure. Kwa hiyo mtu alishaambiwa na madaktari kuwa ugonjwa wako hauna tiba po pote duniani, kesho yake utamuona startv akiomba achangiwe pesa ya kuenda India.
 
Swali jingine ninalojiuliza, kama serikali inachangia 50% kwenye mfuko wa NHIF ( ambayo ni kwa ajili ya waajiriwa) kumbuka mchango wa serikali ni kutoka kwa kodi ya wananchi wote. Je kwa mifuko ya kijamii CHF, serikali inachangia nini?
Waajiriwa wa serikali hukatwa 3% hadi 6% ya mishahara yao kila mwezi ambazo hupelekwa kwa mfuko wa NIHF. Hivyo wapo watumishi wengi tu wa serikali ambao kila mwaķa wanalipa shs 3 million kwenye mfuko huo. Watake wasitake makato hayo ni ya lazima kwa mjibu wa sheria. Serikali haichangii 50% ya mfuko huo.
 
Tunatoa elimu. Ni kazi yetu kukupa elimu wananchi wote wasiyoyajua mambo haya akiwemo TL. Siyo kwamba tunateseka. Ni kazi.
Hizo porojo hamna elimu yoyote. Serikali ya kilaghai hii mnalipwa kutetea ujinga
 
na band ya chini kabisa inalipiwa 100% na serikali. Vipi Tz hao waliopo chini ya poverty line wangapi wanalipiwa bima na serikali kma Rwanda?
Mbona wewe mgumu kuelewa? Nimekuambia wale wasiyo na uwezo (masikini) wanapewa msamaha wa kutolipa cho chote. Maana yake ni kuwa wanalipiwa na serikali 100%. Au wewe tu unataka neno bima lionekane ndiyo uelewe kuwa umelipiwa hayo matibabu?
 
Acha kuamini majungu. Ni mtanzania yupi aliyeachwa akafa akiwa kwenye hospitali, kituo cha afya au zahanati zetu za serikali kwa sababu hana pesa?

Uhaba wa madawa na vifaa tiba ni suala tofauti. Hili linatokana na mzigo mkubwa ambao serikali inaendelea kuubeba katika hiyo cost sharing kati ya mgonjwa na serikali. Hata hivyo kupitia fedha za mafisadi ambao serikali imewabana pamoja na kuongeza makusanyo ya kodi kutoka Tsh 800 billion kwa mwezi mwaka 2015 hadi Tsh 1.5 trillion kwa mwezi mwaka 2020, uhaba wa dawa na vifaa tiba umepungua kwa kiasi kikubwa sana. Serikali imeweza kuongeza bajeti ya madawa MSD kutoka Tsh 28 billion hadi Tsh 280 billion. Imeongeza wataalamu wa afya kwenye vituo tiba kwa kiasi kikubwa nk. Hata yale magonjwa yaliyohitaji kutibiwa nje ya nchi mengi yake sasa yanatibika hapa hapa. Kwa kasi hii uhaba wa dawa, vifaa tiba na watalaamu wa afya muda si mrefu litakuwa historia. Tumefanya yote haya kwa pesa zetu za ndani. Hakuna cha mikopo wala cha misaada ya wajomba. Lissu haya hayajui. Yeye anadhani haya yanafanywa na bima ya afya. Eti anasema akichaguliwa kuwa rais bima
ya afya itawapandisha mishahara madaktari na manesi mara dufu!
Wishful thinking. Watu hawaendi hospitali kwa sababu hawana pesa ya kadi itakayowaruhusu kumuona daktari. Hiyo ndio hali ambayo raia wengi wa vijijini wanayo. Raia ambao wakipata 1000 kwa siku wataimudu vipi hiyo Caesarian ya shilingi 150000 ambayo wewe unaona ni bei nafuu? Badala ya kumponda Lissu kwa kutoa mategemeo ya makusanyo ya baadae, kakae na wananchi wa kawaida usikie machungu yao. Hao ndio wanaojaa kumsikiliza Lissu kwa sababu angalau anaonekana kuyaelewa. Watu wanachohitaji ni tiba na madawa kwa gharama watakayoimudu na si taarifa ya kuwa mmefanya mliyofanya bila kuomba mkopo. Kwa maneno mengine haijalishi rangi paka, kinachothaminiwa ni kuwa anakamata panya.

Amandla...
 
Mimi ni Mtanzania ninaye ishi Canada. Universal Health care ni bima ya afya ambayo kila mkazi anapewa na serikali. Kwa miaka ambayo nimeiishi Canada, sijawi lipia matibabu wala familia yangu kulipia matibabu. Kusema ukweli gharama za elimu na matibabu ni cost za serikali. Tena kwa watoto gharama za elimu ni free mpaka school bus za kuwapeleka mashuleni na kuwarudisha. Nakuwekea maelezo hapo chini usome na nakuwekea na link yake.

Healthcare in Canada is delivered through the provincial and territorial systems of publicly funded health care, informally called Medicare.[1][2] It is guided by the provisions of the Canada Health Act of 1984,[3] and is universal.[4] Universal access to publicly funded health services is often considered by Canadians as a "fundamental value that ensures national health care insurance for everyone wherever they live in the country.

link;

Healthcare in Canada - Wikipedia
Mwambie huyoo msisiemu
 
Kuna baadhi ya hospitali za serikali zimeanza kuwalipisha watoto chini ya umri wa miaka 5, wanawake wajawazito, wazee na watu wenye magonjwa Sugu, hili unalisemaje mkuu?
Ni jukumu la madiwani na wabunge tutakaochagua kudhibiti hali hiyo. Wahusika wanapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Ni kazi ya serikali za mitaa.
 
Hii ndio shida ya ccm wote, walikua wanamuona Magufuli kama Mungu. Kwakua kila amri aliyoitoa kwa kila MTU na kila Taasisi ilitekelezwa kwa haraka na kwa woga. Sasa yuko kwenye kampeni anakosolewa,anapingwa na kupigwa vijembe ..Mnasema anamtukana na kumdharau Magufuli.

Hivi kuna dharau kubwa kama kuwasema vibaya watu waliopatwa na maafa ambako jiwe amefanya mara nyingi?
Dharau kwa wabunge wa upinzani,maneno machafu alokua anawaambia watu hadharani.
Leo kapata MTU wa kumjibu,kumuonya na kumwelekeza mnalalamika.
 
Acha upuuzi.. nenda rwanda hapo kajifunze.. acha kukopi kwenye mitandao.
Huyu mgombea kila kukicha anawapotosha wananchi kwa kuwaeleza mambo ambayo si sahihi. Anaongea mambo ambayo hayajui na hana utalaamu nayo. Hana wataalamu wa kumshauri ukweli wa kile anachokusudia kuwaeleza wananchi.

Moja ya upotoshaji anasema ni kuwa akichaguliwa atawaletea watanzania wote Universal health care. Ukimsikiliza utagundua kuwa kwake universal health care maana yake ni bima ya taifa ya afya kwa wote. Utagundua kuwa bima ya afya yataifa kwake ni NIHF tu. Hajui kuwa kuna bima zingine za afya za taifa kama CHF, TIKA, SHIB ya NSSF na kadhalika. Hajui kwamba kuna makampuni binafsi zaidi ya saba nchini yanayotoa bima ya afya. Hajui kwamba hadi sasa mzigo mkubwa wa gharama ya matibabu ya watanzania bado unabebwa na serikali kupitia mapato yake ya kodi kwa ujumla (government revenue)

Ukweli ni kwamba:
1.
Universal health care a.k.a universal health coverage (UHC) is a health care system in which all residents of a particular country are assured access to health care. The World Health Organization describes it as a situation where all citizens of a particular country can access health services without incurring financial hardship.

Maana yake ni kwamba UHC ni mfumo wa serikali unaohakikisha raia wake wote wanapata huduma za afya. UHC ni sera ya nchi na mfumo wake unatekelezwa kwa kuundiwa sheria kanuni na taratibu za utekelezaji.

2. Tangia enzi za Mwalimu Nyerere raia wote wa Tanzania walikuwa wanapata huduma za afya bila kulipa chochote. Gharama zote zilibebwa na serikali kupitia mapato yake ya kodi (TRA) na yasiyokuwa ya kodi (government revenues). Sisi tuliyaita matibabu ya bure. Hivyo universal health care coverage ilikuwa 100% kwa gharama ya serikali ya 100% kupitia bajeti yake ya wizara ya afya.

3. Kufikia miaka ya 1990s, kutokana na ongezeko la watu (population) na ongezeko la gharama za tiba kufuatana na teknolojia za kisasa za tiba zenye gharama kubwa, serikali yetu (kama zingine duniani) ilielemewa na mzigo huu wa kutoa huduma bure kwa wote.
Hivyo kwa sababu hizo lakini bila kuathiri universal health care policy, serikali ilibadilisha kidogo mfumo huo kwa kuanzisha utaratibu wa health cost sharing kwa wale wenye kauwezo. Kwa utaratibu huu mgonjwa alitakiwa kuchangia asilimia kidogo ya gharama ya matibabu yake. Gharama kubwa ilibebwa na serikali.

Kwa wale ambao hawana uwezo kabisa wa kuchangia serikali iliweka utaratibu wa kuwasamehe. Makundi yafuatayo hayakusika na utaratibu huu wa cost sharing (hadi sasa): Watoto wote walio chini ya miaka mitano, mama wajawazito, wenye umri unaozidi miaka sitini, wenye magonjwa ya kansa, kifua kikuu, HIV na magonjwa mengine sugu. Hawa bado serikali inabeba gharama zao za matibabu kupitia bajeti yake ya walipa kodi wote nchini. Pia kwa magonjwa ya dharura mtoa huduma analazimishwa kutoa huduma kwanza, masuala ya kiasi gani mgonjwa achangie ataulizwa baada ya kupona na kama hatakuwa na uwezo huo utaratibu wasamaha utafuata baada ya kupona.

Hivyo hata baada ya kuanzisha cost sharing mfumo ulihakikisha universal health care kwa raia wote kwa serikali kubeba most of the cost. Ingawa kiwango cha hii cost sharing ya mgonjwa imekuwa ikiongezwa kidogo kidogo lakini hadi sasa burden kubwa bado inaendelea kubebwa na serikali. Kwa mfano gharama ya operesheni ya Caesarian Section huko Amerika ni USD 18,000 ambayo ni sawa na takribani Tsh 40 million lakini sisi hapa cost anayopaswa kuchangia mgonjwa haizidi Tshs 150,000/ na kama ni ya uzazi ni bure na kama hana uwezo anasamehewa au analipa kidogo ya hiyo. Inayobaki serikali inabeba kuhakikisha hakuna raia wake atakayekufa kwa kukosa uwezo wa kulipia gharama hizo. Hence 100% universal health coverage.

Dhana na chimbuko la bima za afya (Evolution of other health care financing in Tanzania):
Ili kurahisisha na kupunguza buguza/ changamoto ulipwaji wa hizo cost sharing kwa upande wa mgonjwa serikali iliunda bima za afya za taifa (public owned health insurance schemes:

1. The National Insuranse Health Fund (NIHF) ilianzishwa mwaka 1999 (Act of Parliament No. 8 of 199 -CAP 395 RE 2002) kwa ajili kwa waajiriwa wa serikali - government workers. Kila mwajirwa wa serikali alilazimika kukatwa 3% ya mshahara wake kila mwezi na serikali kutoa kiasi hicho hicho kutoka vyanzo vyake vingine vya mapato hivyo kupata 6% ya mshahara na kuuweka kwenye huo mfuko wa bima wa taifa. Mchango huo unamuwezesha mtumishi huyo pamoja na mwenza wake, watoto wao wasiozidi 4 wenye umri usiozidi miaka 18 na wazazi wake wawili - jumla watu sita kupata matibabu kwa gharama ya mfuko huo wa NIHF.

NB: - Waajiri na waajiriwa binafsi hawalazimiki kisheria kwa sasa kujiunga na mfuko huu. Ni wa hiari kwao.
- hulipa Shs 50,000 tu kwa mwaka kuwa wanachama wa mfuko huu.

2. Community Health Fund (CHF): Walengwa hasa wa mfuko huu ni wakazi wa vijijini. Ni mfuko wa hiari. Kila kaya hulipa Sh 10,000 tu kwa mwaka ambayo huwezesha mkuu wa kaya pamoja na watoto wao wote wenye umri chini ya miaka 18 kupata matinabu kwenye ngazi ya zahanati, kituo cha afya hadi hospitali ya wilaya bila mchango mwingine.

3. TIKA (Tiba kwa Kadi): Huu unafanana na ule wa CHF, tofauti hapa ni kaya zilizo mjini.

4. SHIB - ni Social health insurance benefit ulio chini ya National Social Scurity Fund (NSSF).

Ukiacha hizo mifuko aina 4 za bima za afya za kitaifa pia yapo makampuni zaidi ya saba yanayoendesha private health insuranses eg AAR, Strategy etc. Pia bima za maisha zinazotolewa na bima za kawaida huwa zina health insurance.

Mgombea huyo anapaswa kujua basics hizi badala ya kujifanya much know na kuanza kupotosha wananchi kwamba wataletewa UHC kutoka ubelgiji. Hiyo Obamacare haifiki ya kwetu kwa ubora na kwa coverage. UHC coverage ya kwetu bado ni 100%. Hakuna anayekosa matibabu au kufa kwa sababu hana pesa. Nchi zingine haziko hivyo.
 
Awamu ya tano imeharibu kabisa mifumo.. wao kujisifia tuu na majengo.
Hayo makundi yaliyosamehewa kwa kifupi yanaonekana ni mzigo kwa serikali ya CCM. Wazee wengi 75+ wanasema wakiugua wanawahi hospitali, kwenye foleni wanatengwa wanaambiwa wasubiri. Mpaka wale wenye Bima waonwe wote hapo ni saa 8 mchana ndiyo unaandikiwa paracetamol hata kama unaharisha.
 
Acha upuuzi.. nenda rwanda hapo kajifunze.. acha kukopi kwenye mitandao.
Rwanda yenyewe imekopi kwetu. Sisi tuliunda mfumo huu miaka ya 1991 wakati huo wanyarwanda wakiwa buisy wakitwangana wenyewe kwa wenye na sisi tukiwa wasuluhishi wao.
 
Back
Top Bottom