Abasi Mayala: Uchaguzi wetu usitengeneze mpasuko ndani ya chama

Abasi Mayala: Uchaguzi wetu usitengeneze mpasuko ndani ya chama

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa chama cha Mkoa wa Mwanza, Abbas Mayala amewatahadharisha wanachama, wafuasi na wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wa juu katika chama hicho kuepuka kutafuta kura huku wakitumia lugha ya matusi, kejeli na fedhea wakati wa kampeni.

Akizungumza na Jambotv_ leo Januari 4, 2025 jijini Mwanza, Mayala amesema mbali na kuwa uchaguzi huo utakuwa mgumu lakini hatarajii kuona uchaguzi huo una tengeneza mgawangiko na mpasuko ndani ya chama hicho baada ya uchaguzi.

"Nitoe tahadhari kwamba mimi naweza kuwa namuunga mkono mgombea yoyote, lakini ninachokiomba kutoka kwa wanachama na wapiga kura wenzangu tusitafute kura kwa misingi ya kutukana, kuzodoa, kukejeli, kufedhehesha au kumtweza mtu yoyote kwa sababu kila mmoja katika chama hiki ana mchango wake,"

PIA SOMA
- Je, Mpasuko Ndani ya CHADEMA Unaashiria Kuporomoka kwa Chama?
 
Mbona mpasuko upo tayari kabla hata ya uchaguzi? Au unajaribu kuzuia mpasuko ndani ya mpasuko?
 
Back
Top Bottom