TANZIA Abbas Mwinyi Mtoto wa mstaafu Marehemu Ali Hassan Mwinyi afariki dunia

TANZIA Abbas Mwinyi Mtoto wa mstaafu Marehemu Ali Hassan Mwinyi afariki dunia

Hiyo ndinga ilikuwapo home ukiingia ndani full AC ni kama upo katika ndege ya chinichini.
Naikumbuka hiyo .AC yake ni full kipupwe cha hatari sana. Hapa mjini zilikuwa zinahesabika.

mara ya kwanza nilipanda hiyo ndinga ilikuwa ya Mzee Ludovic Utouh kipindi hicho alikuwa NBAA kabla hajawa CAG. Vijana wake ni washkaji tumekuwa nao wao wakikaa upanga.

Huyo mzee alikuwa mtata sana watu waliofanya paper za bodi uhasibu kwa ajili ya CPA wanamjua sana Mzee Ludovic Utouh.
 
Apumzike kwa amani, mara ya mwisho namsikia ni 2000s nilijua hayuko Bongo kabisa
 
Alikuwa class mate wa Baba mdg wangu na marafiki sana mpk ukubwani, na alipokuwa msumbufu sana hapa Zanzibar alishapelekwa akasome Ilboru Sec Arusha....hlf akawa analala kwa Benson...katoroka hapo kaenda Moshi kwa pikipiki akagonga Mtu akafungwa Moshi Central Police...hawakujua ni Mtoto wa Rais,ikapigwa simu moja tu...(landline wakati huo) aachiwe ndani ya dakika chache, baadae kikawakuta Polisi

Lastly, akarudishwa hapa Zanzibar,Kisha akatoroka tena kwenda Dsm🤣
 
Abbas was 60 years old.

Alikuwa na Mitsubishi Pajero Intercooler Turbo lake moja. Miaka hiyo Pajero ndiyo zinatamba mjini.

Pajero mtama kwa watoto, matata sana. Akipita mtaani lazima warembo wapige kelele "Abasiiii".

Mitaa ya Oysterbay alijulikana sana kuwa mtu wa matukio ambaye ukimpa nafasi kusema tu lazima inakula kwako kwa sababu mdomo mali yake na Kiswahili kimetoka kwao.
Halafu bado ipo ujue🤣
 
Pole sana wanafamilia wote, ndugu na marafiki. Mungu wa huruma awajalie moyo mkuu ili mpokee msiba huu kwa moyo wa imani na unyenyekevu.

Mungu wa huruma tunaomba umpokee mja wako kama alivyokuamini na kukutegemea. Tunaomba ukayaangalia mema yake kuliko makosa yake, na hasa kama alikutegemea na aliuishi kwa dhamira upendo wa Mungu.

Nasi tuliobakia, kila kitokeapo kifo kwa mwenzetu, tujue tunakumbushwa kuwa Duniani ni sehemu tu ya maandalizi ya maisha ya milele, tujiulize tunaandaaje maisha yetu ya baadaye?

Wale watekaji, wauaji, wabambikiaji kesi, mafisadi, na wadhulumu haki za wanadamu wenzao, mnakumbushwa kuwa sisi tu mavumbi, na mavumbini tutarudi. Ya nini muwaue wenzenu wakati sisi sote kuna siku lazima tukifikie kifo cha mwili.

Mnaoteka na kuua binadamu wenzenu mjue kuwa hiyo mnayofikiria ni adhabu kubwa sana mnawapa hao mnaowaua, ni ndogo sana kuliko adhabu mnayojipa. Hao mnaua miili yao, lakini ni kwa gharama kubwa sana ya kuua roho zenu.

Rais Samia, ingiwa na roho wa Mungu, ingiwa na hekima, hata kama huteki na kuua kwa mikono yako, na pengine siyo kwa amri yako, lakini ufahamu kuwa kila linalotokea chini ya mamlaka yako, usipolikana kwa kauli na vitendo, usipolizuia kwa kutumia mamlaka yako, moja kwa moja unabeba hukumu ya kuiua roho yako.

Tuombe hekima ili tujue namna sahihi ya kuuishi upendo wa Kristo, upendo wa Mungu wetu.
 
Alikuwa class mate wa Baba mdg wangu na marafiki sana mpk ukubwani, na alipokuwa msumbufu sana hapa Zanzibar alishapelekwa akasome Ilboru Sec....hlf akawa analala kwa Benson...kutoka hapo kaenda Moshi kwa pikipiki akagonga Mtu akafungwa Moshi Central Police...hawakujua ni Mtoto wa Rais, baadae kikawakuta Polisi

Lastly, akarudishwa hapa Zanzibar,Kisha akatoroka tena kwenda Dsm🤣
Daa masikini police wakisema wafuate Sheria tabu wasipofuata Sheria tabu.
 
Live fast, die young.

Miaka 60 amevuta si haba.

R I P
 
Back
Top Bottom