Abbasia ya Ndanda umeme wake 24hrs

Abbasia ya Ndanda umeme wake 24hrs

Gpaghy

Member
Joined
Sep 25, 2021
Posts
47
Reaction score
138
Wakuu habari,

Najiuliza serikali Yetu inashindwa wapi?, Abbasia ya ndanda nyenye wakazi wengi tu!! Wana umeme wao wa maji, umeme ni masaa 24, haukatiki, maji yao pia ni safi sana na ni 24hrs hayakatiki!

Serikali tunashindwa wapi kuwahudumia wananchi wetu

Mimi nafikiri Ifike hatua tufikie nchi kama Korea Kusini, sio kutumia trillions of money kwa vitu ambavyo havimugusi mwananchi moja kwa moja! Ni mda sasa CCM ikae pembeni ipishe mawazo mengine
 
Mbinu mbadala husaidia nyakati kama hizi

Tusibweteke na tulichonacho maana hatujui siku wala saa hali itakapobadilika

Tunaposema ajira hakuna wataalamu walitakiwa wawe wanakuna vichwa kutafuta vyanzo vya nishati mbadala kama thermal, wind, jua, taka, mawimbi ya bahari nk tuwekeze tuzalishe mfumo uwe umeshiba muda wote

Kipau mbele siasa tutafika?
 
Wakuu habari, najiuliza serikali Yetu inashindwa wapi?, abbasia ya ndanda nyenye wakazi wengi tu!! Wana umeme wao wa maji, umeme ni masaa 24, haukatiki, maji yao pia ni safi sana na ni 24hrs hayakatiki...
Niliwahi leta hoja humu 3 weeks ago kwamba miradi iliyosimamiwa na taasisi za dini ni bora na endelevu

Nikashauri serikali Iwe inateua watumishi toka huko

Miradi mingi ya serikali nikichefuchefu
 
Mbinu mbadala husaidia nyakati kama hizi.
Tusibweteke na tulichonacho maana hatujui siku wala saa hali itakapobadilika...
Bahati mbaya huwa tunakaa tu tukitegemea mambo yatajisort yenyewe, tuna hilo tatizo.
 
18 November 2021
Mwanza, Tanzania

Rais Samia S. Hassan : Uvamizi wa vyanzo vya maji, kukata miti na kuchepusha maji ni janga kubwa Tanzania



Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani amesema uvamizi wa vyanzo vya maji, kukata miti na kuchepusha maji kwa ajili ya matumizi ikiwemo kilimo na mifugo ni chanzo cha upungufu wa maji katika maeneo mengi nchini.

Source : Millard Ayo
 
Wakuu habari,

Najiuliza serikali Yetu inashindwa wapi?, Abbasia ya ndanda nyenye wakazi wengi tu!! Wana umeme wao wa maji, umeme ni masaa 24, haukatiki, maji yao pia ni safi sana na ni 24hrs hayakatiki!

Serikali tunashindwa wapi kuwahudumia wananchi wetu

Mimi nafikiri Ifike hatua tufikie nchi kama Korea Kusini, sio kutumia trillions of money kwa vitu ambavyo havimugusi mwananchi moja kwa moja! Ni mda sasa CCM ikae pembeni ipishe mawazo mengine


Ndanda, Mtwara
Tanzania

Teknolojia ya umeme wa maji waokoa watu wengi mjini Ndanda mkoani Mtwara, kusini mwa Tanzania.



Source : DW KiSwahili
 
Ndanda, Mtwara
Tanzania

Teknolojia ya umeme wa maji waokoa watu wengi mjini Ndanda mkoani Mtwara, kusini mwa Tanzania.



Source : DW KiSwahili

Sio ndanda tu hata pale chipole songea, kuna mission ya ma sister wana umeme wao wa maji wanazalisha kujisimamia wenyewe
 
Sio ndanda tu hata pale chipole songea, kuna mission ya ma sister wana umeme wao wa maji wanazalisha kujisimamia wenyewe

UJUE MRADI WA UMEME WA MAJI TULILA - RUVUMA TANZANIA



Mtazame mtawa wa Shirika la Mtakatifu Agnesi Chipole Jimbo Kuu la Songea Sr.Veritas Ndumbili OSB akielezea mradi wa umeme wa maji wa Tulila ambao upo kwenye maporomoko ya maji ya mto Ruvuma ambao unamilikiwa na watawa hao.Mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati tano ndiyo uliomaliza tatizo la mgawo wa umeme katika mji wa Songea

Source : Songea TV



Chipole, Songea

DARAJA LA CHIPOLE SONGEA


Hatimaye Watawa wa Shirika la Chipole wilayani Songea wameridhia maombi ya muda mrefu ya wananchi kuruhusiwa kulitumia daraja lililokuwa limefungwa kwa zaidi ya miaka mitatu kutokana na kile kilichoelezwa na watawa hao kwamba baadhi ya wananchi walikuwa wakilitumia vibaya daraja hilo na kuhatarisha maisha yao

Source : Azam TV
 
Pesa ya kununulia ndege ingetumika kununua mitambo ya kuzalisha umeme kupitia gesi. Pia kutumia jua kuzalisha umeme. Hili jua linalotuivisha na kutuletea joto pesa ingetumika kujenga solar farms kuzalisha umeme.
Nimeona mahala eti ndege nyingine nne (4) ziko njiani zinakuja Dar. Hivyo viwanja vya ndege viko wapi?
 
TULILA : CHANZO CHA UMEME WA MAJI ULIOMALIZA MGAO WA UMEME MJINI SONGEA
Na Albano Midelo

Kwa miaka mingi mji wa Songea umekuwa unakabiliwa na mgawo mkali wa umeme hali ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika mji huo ambao ndiyo kioo cha Mkoa wa Ruvuma.

Mchawi mkubwa wa tatizo la umeme katika mji wa Songea ilikuwa kuendelea kutumia Jenereta chakavu ambazo zilikuwa zinatumia vipuli chakavu na changamoto ya mafuta ambayo yalikuwa yanakwisha mara kwa mara.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Agosti 2009 alifanya ziara katika Mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuangalia shughuli za kimaendeleo na changamoto zinazowakabili wananchi wa mkoa huo.

Siku ya kwanza ya ziara yake Rais Mstaafu Kikwete wakati anapita barabarani akitokea uwanja wa ndege wa Songea alishuhudia wananchi wakipiga kelele na kudai umeme huku wamewasha taa mchana kutokana na hali halisi ya tatizo sugu la umeme wa kutoaminika katika mji wa Songea ambalo lilikwamisha shughuli za kijamii na kiuchumi.

Rais Mstaafu Kikwete alisikitishwa na kasi ndogo ya kushughulikia ufumbuzi wa tatizo la vipuri vya mashine za kufulia umeme katika mji wa Songea hali liyosababisha kumwagiza Meneja wa TANESCO mkoa wa Ruvuma wakati huo injinia Monica Kebara kufuatilia ili kujua vipuri vya mashine hizo vipo wapi na alitaka kupata ripoti ya vipuri hivyo na mwenendo mzima wa matengenezo ili wananchi wafahamu kila hatua.

Rais Kikwete hakuishia hapo, badala yake aliahidi kuileta mashine mpya ya kufua umeme ambayo aliamini ingeweza kumaliza tatizo la mgawo mkali wa umeme katika mji wa Songea hivyo mgawo mkali wa umeme kubakia kuwa historia.

Baada ya kufungwa mashine mpya ya Rais Kikwete aina ya ABC yenye uwezo wa kuzalisha megawati 1.6 angalau tatizo la mgawo mkali katika mji wa Songea lilipungua kwa miaka takribani mitatu, ingawa matatizo ya mafuta na vipuri yaliendelea na kuathiri umeme katika mji wa Songea.

Hata hivyo baada ya miaka hiyo tatizo la mgawo mkali wa umeme liliongezeka kutokana na kile ambacho kilitajwa na TANESCO kuwa ni kuharibika kwa mashine kutokana na vipuri kuharibika.

Tangu mwaka 2016 tatizo la mgawo wa umeme katika mji wa Songea limebakia kuwa historia mara baada ya TANESCO Ruvuma kuanza kununua umeme wa maji kutoka Tulila mto Ruvuma.

Chanzo hicho kinamilikiwa na watawa wabenediktine wa Mtakatifu Agnes Chipole Jimbo Kuu Katoliki la Songea ambapo sasa tatizo la umeme katika mji wa Songea limebakia kuwa historia.

Akizungumza kwa niaba ya Mama Mkuu wa Shirika hilo, Sr.Richards Chiwinga(OSB) anasema wana mashine mbili ambazo zina uwezo wa kuzalisha megawatts tano ambapo TANESCO Ruvuma ndiyo wateja wao wakuu ambao wanawauzia umeme huo.

“Mji wa Songea unahitaji megawatts kati ya 3.5 hadi 4.5 hivyo tunabakiwa na ziada ya umeme, TANESCO wamezima majenereta yao chakavu ambayo yalikuwa yanasababisha mgawo wa umeme, hivi sasa wanatumia umeme wetu wa maji unaozalishwa toka hapa’’,anasisitiza Sr.Chiwinga.

Soma zaidi : source : Tulila:chanzo cha umeme wa maji kilichomaliza mgawo wa umeme mjini Songea
 
Nimeona mahala eti ndege nyingine nne (4) ziko njiani zinakuja Dar. Hivyo viwanja vya ndege viko wapi?
Asipo nunua, watu wata sema siunaona hata kununua ndege hawezi ...so waacha azinunue tu
 
Njoo ABASIA YA PERAMIHO

happy napo umeme n 24hrs wana bwawa la la kuzalisha umeme toka enzi

Mashirika ya dini yanafanya vizuri kushinda serikali
 
Njoo ABASIA YA PERAMIHO

happy napo umeme n 24hrs wana bwawa la la kuzalisha umeme toka enzi

Mashirika ya dini yanafanya vizuri kushinda serikali
Hata hao wamisionari wapigaji tu,ila huwa wanahakikisha mradi unafanyiwa service.
 
Back
Top Bottom