Kesi za namna hii Hakimu au Jaji anapaswa kuwa mwangalifu sana katika kuzisikiliza au kwenye kuzitolea Uamuzi, kwa sababu huwa zinaambatana na mambo mengi Sana ya visasi, chuki binafsi, masuala ya kubambikiana Kesi, wivu, n.k. Kwa hiyo Jaji au Hakimu anapoziendesha Kesi za namna hiyo kwa kasi ndogo na kwa muda mrefu inaweza kumsaidia Hakimu huyo kupata taarifa za uhakika kupitia vyanzo vya pembeni kuhusiana na ukweli halisi wa kisa chote kabisa kilichosababisha kuibuka kwa Kesi iliyopo mbele yake. Hii kwa upande mwingine inaweza pia kumsaidia Hakimu au Jaji huyo kufanya Uamuzi sahihi na wa haki kuhusu Kesi husika.