LGE2024 Abdul Nondo: Chini ya ACT Wazalendo hakuna raia atachukuliwa na Uhamiaji bila mwenyekiti kupata taarifa, akumbushia kutekwa kwake

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
"Tunajua mna tatizo kubwa la uhamiaji. Hata mimi walishawahi kunisumbua, wakaniambia mimi si raia wa nchi hii na kunitaka nipeleke vyeti vya babu yangu aliyemzaa babu yangu. Lengo lao lilikuwa kunisumbua tu, lakini chama changu cha ACT kilisimama nami mpaka mwisho. Hivyo kupitia ACT, hakuna raia atakayechukuliwa na Uhamiaji bila Mwenyekiti kupata taarifa."Ameeleza Nondo.

"Hakuna raia atanyakuliwa na Uhamiaji kuambiwa si raia bila Mwenyekiti wa kijiji kusimama na kusema, 'Huyu ni raia. Mzazi wake ninamjua, ni mzee fulani.' Mwenyekiti wa ACT atahakikisha haki na usalama wa raia wake vinaheshimiwa." Amesema Nondo.

"Chagueni viongozi ambao watakuwa watetezi wenu. Hawa mkiwachagua wanakwenda kuwa wakuu wa ulinzi na usalama katika maeneo yenu. Mwenyekiti huyo anakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kijiji. Hakuna raia atapotea bila taarifa kwa Mwenyekiti, na hakuna polisi atakayemchukua raia kiholela bila Mwenyekiti kujua."
 
hiyo sio kazi ya mwenyekiti wa mtaa hawa ndio mana wanafeli kujaza fomu
 
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo Taifa, Abdul Nondo, ameikemea vikali Idara ya Uhamiaji kwa madai ya kuwanyanyasa baadhi ya wananchi, akiahidi kuwa chama hicho kitahakikisha haki na usalama wa raia wa Tanzania vinazingatiwa.

Nondo ameyasema hayo akizungumza katika kampeni za kuwanadi wagombea wa chama hicho katika kijiji cha Mwali, kata ya Nyachenda, Jimbo la Kasulu Vijijini mkoani Kigoma, Ijumaa, Novemba 22, 2024,

Soma pia: Abdul Nondo: ACT sio kama CCM hatuwezi kutoweka baada ya Uchaguzi

Nondo amesisitiza kuwa viongozi wa ACT wakichaguliwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, watakuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za wananchi dhidi ya unyanyasaji wa mamlaka mbalimbali. Aidha, Nondo amewaasa wananchi kuchagua viongozi wanaojali masilahi ya wananchi​

Chanzo: Jambo TV
 
"Tunajua mna tatizo kubwa la uhamiaji. Hata mimi walishawahi kunisumbua, wakaniambia mimi si raia wa nchi hii na kunitaka nipeleke vyeti vya babu yangu aliyemzaa babu yangu. Lengo lao lilikuwa kunisumbua tu, lakini chama changu cha ACT kilisimama nami mpaka mwisho. Hivyo kupitia ACT, hakuna raia atakayechukuliwa na Uhamiaji bila Mwenyekiti kupata taarifa."Ameeleza Nondo.

"Hakuna raia atanyakuliwa na Uhamiaji kuambiwa si raia bila Mwenyekiti wa kijiji kusimama na kusema, 'Huyu ni raia. Mzazi wake ninamjua, ni mzee fulani.' Mwenyekiti wa ACT atahakikisha haki na usalama wa raia wake vinaheshimiwa." Amesema Nondo.

"Chagueni viongozi ambao watakuwa watetezi wenu. Hawa mkiwachagua wanakwenda kuwa wakuu wa ulinzi na usalama katika maeneo yenu. Mwenyekiti huyo anakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kijiji. Hakuna raia atapotea bila taarifa kwa Mwenyekiti, na hakuna polisi atakayemchukua raia kiholela bila Mwenyekiti kujua."
Ana hoja,asikilizwe.
 
pafyumu alipata wapi mpaka akawa ananukia vile kama kweli alitekwa?🐒
 
Back
Top Bottom