Abdul Nondo: Maisha yetu ni siasa, huwezi kujitenganisha na siasa

Abdul Nondo: Maisha yetu ni siasa, huwezi kujitenganisha na siasa

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079


"Vijana kukosa ajira ni serikali kutokuamua kuchukua hatua. Uwepo wa ufisadi na ubadhirifu ni serikali kutokuamua kuwajibisha, wameamua kujilinda na kukaa kimya. Maisha yetu ni siasa, kila siku huwezi kujitenga na siasa.

Aristotle, mwanafalsafa mashuhuri anasema mwanadamu ni kiumbe cha kisiasa, anasema 'political animal'. Na anasema kama hutaki kujihusisha na siasa, nenda kakae msituni, porini kusiwe na jamii inayofanya maamuzi kwa niaba yako, utakuwa umejitenga na siasa na jambo hilo haliwezekani.

Wanafunzi mnakosa mikopo ni siasa kwa sababu serikali imeshindwa kuamua vilivyo ili mwezi kupata mikopo mingi zaidi."- Amesema Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa Chama cha ACT-Wazalendo, Abdul Nondo
 
Back
Top Bottom