Abdulrahman Kinana amempongeza Rais Samia kwa kuvunja rekodi za Mapato

Abdulrahman Kinana amempongeza Rais Samia kwa kuvunja rekodi za Mapato

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2020
Posts
2,823
Reaction score
2,466
IMG-20240418-WA0047.jpg

Na Mwandishi Wetu, Musoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Makamu Mwenyekiti wake Tanzania Bara, Abdulurahman Kinana amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anafanya mambo makubwa ya maendeleo kwa Watanzania ikiwamo kuongeza mapato ya Serikali bila ya wananchi kushurutishwa au kuporwa fedha zao.

Akizungumza leo Aprili 17, 2024 katika kikao kazi cha wanachama wa CCM Wilaya ya Musoma Mjini mkoani Mara, Kinana amesema chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia nchi imepiga hatua kubwa ya maendeleo kuliko awamu nyingine zilizopita.

"Kwanini tusitoe pongezi kwa Rais Samia?. Amefanya kazi nzuri, anajitoa, anajituma na kubwa amekuwa kiongozi wa mfano anaongoza nchi yetu vizuri na maendeleo yanapatikana kila mahali na Musoma hapa ni mashahidi.

"Hata katika ukusanyaji wa mapato hakuna mwaka tumepata mapato makubwa bila kufunga watu, bila kupora watu kama mwaka huu. Huu ndio ukweli, Watanzania tumuunge mkono, kuna usemi unasema ukitaka jambo lisemwe mpe mwanaume ukitaka jambo lifanyike kwa uhodari mpe mwanamke.

"Kazi ya kusema ni ya mwanaume na kazi ya kutenda ni wanawake, akina mama ni waaminifu...Kwa hiyo Rais Samia amefanya kazi nzuri lakini na Chama Cha Mapinduzi kinafanya mengi mazuri zaidi.

"Chama hiki ni kizuri, ukiona hakiendi ujue wakubwa huku juu wanakivuruga, sio wanachama," amesema Kinana na kufafanunua kuwa maendeleo yanayopatikana chini ya uongozi wa awamu ya sita yamefika hadi Musoma na Mkoa wa Mara kwa ujumla.

"Musoma hapo nyuma nikiwa Katibu Mkuu nilikuja kufanya ziara kulikuwa hakuna maendeleo kama ilivyo sasa. Mbunge wa Musoma Mjini (Vedastus Mataulo) ameeleza kuwa Musoma hamna shida ya barabara za lami, maana zipo.

"Shule ziko nyingi, maji yapo ya kutosha, hospitali ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere inaendelea vizuri, Rais amefanya mambo makubwa ya maendeleo.

== ==
 
Let me get this Straight....

Kavunja rekodi ya mapato lakini value for money kwa mdau kitaa haipo !!! Hizo pesa zinakwenda wapi ?!!

Sasa si bora tusivunje rekodi / pesa zisikusanywe sababu hata zikikusanywa kitaa hakuna tofauti...., Huku ndio kuweka punda mbele ya mkokoteni...; Cha kufanya tuhakikishe matumizi ya pesa yanakwenda vizuri nina uhakika kwa theluthi ya kinachokusanywa wala bila Tozo au kutembeza Bakuli tunaweza kufanya marafudufu ya ambacho kinapaswa kufanyika...
 
Sasa kitakusanywa kisichokuwepo?
 
Ndio maana nasemaga Magufuli ni zero brain, Hongera Samia
 
Sasa kitakusanywa kisichokuwepo?
Hivi kweli unafuata mtiririko wa mawazo yako au kila ukiweka nukta unaanza upya kwa kusahau kilichopita ?

Statement: Amevunja rekodi za Makusanyo
Swali : Haya Makusanyo yanakusanywa yanakwenda wapi mbona hakuna value for money kitaa
Statement: sasa kitakusanywa kisichokuwepo ?

Kwahio kavunja rekodi ya kukusanya kisichokuwepo ?
 
Value for money kwenye jambo gani specifically?
 
Chairman anaipiga teke legacy. Jiwe jiiiii!!!
 
Back
Top Bottom