Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inategemea mwenyekiti wao ameamkaje siku hiyo.Pale unapofukuzwa kazi ikiwa tayari umeshaacha kazi. Only in Tanzania.
Kinana nadhani ni maslahi yamekuwa hatarini. Huyu mzee huko CCM amezoea kubebwa na kuheshimiwa sioni namna anavyoweza kuishi bila kupakatwa na Chama Tawala. Na nadhani mambo yake mengi pengine na familia yake yanategemea huruma za CCM. Hawa ndiyo wale ukienda ofisi za serikali utasikia wanasema ''huu ni mzigo wa mheshimiwa Kinana jamani, msiuchanganye na mingine''.Kutubu bila kosa nako ni utumwa,ni heshima kufukuzwa kuliko kuomba msamaha kwa kosa ambalo halikuwa kosa ukabaki na heshima yako utahesabika ni shujaa asiyeendekeza njaa.
Wamiliki wa chama ni Mama Nyerere,Fatuma Karume.Wengine temporary membership kama UNO ya China,UK,Russia,USA,France permanet membership na Tanzania,Canada, Japan n.k temporary membershipMmiliki wa chama ataki mchezo
ZilipendwaWamiliki wa chama ni Mama Nyerere,Fatuma Karume.Wengine temporary membership kama UNO ya China,UK,Russia,USA,France permanet membership na Tanzania,Canada, Japan n.k temporary membership
Consultant
Tunaweza waita jina gani litakalowafaa hawa jamaa ya misisiem zaidi ya kuwaita mataahira?
Mnawadanganya wenzenu hivihivi wanatumbukia shimoni mnawaangalia halafu mnabaki mnawacheka. .Kutubu bila kosa nako ni utumwa,ni heshima kufukuzwa kuliko kuomba msamaha kwa kosa ambalo halikuwa kosa ukabaki na heshima yako utahesabika ni shujaa asiyeendekeza njaa.
Unamfukuza mtu ambaye si mwanachama! Hana kadi ya CCM.Halmashauri kuu ya CCM imemsamehe Katibu mkuu mstaafu kanali Kinana ambaye alipewa onyo kali na kuwekwa katika matazamio.
Halmashauri kuu pia imemfukuza kabisa yule mwingine ( Membe) ambaye hakufanya juhudi yoyote ya kuomba msamaha.
Membe alirudisha kadi yake CCM badala ya kutubu.
Maendeleo hayana vyama!
======
Akizungumza wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM cha kumteua mgombea Urais wa Zanzibar, Rais Magufuli amsamehe aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana. Rais Magufuli amesema:
Ilikuwa mwezi wa wa pili Central Committee ilaamua kutoa adhabu kwa baadhi ya wanachama wetu ambao walikiuka maadili na misingi ya chama chetu.
Kikao kile kilitoa mapendekezo ya adhabu kwa baadhi ya wanachama wetu kutokana na misingi na Katinba halali ya chama chetu. Lakini ni hivi karibuni baada ya miezi kama mnne au mitano, mwenzetu mmoja ambaye ni Former Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi alijitokeza hadharani kule Arusha, na nafikiri shahidi ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha – akaomba radhi., akautia kwa kitendo alichokifanya. Na kikubwa zaidi, ndugu yetu huyu aliomba radhi hadharani.
Ni kitendo kigumu sana kwa mtu kukifanya. Kinahitaji nguvu ya Mwenyezi Mungu tu kutubu hadharani. Mimi alinigusa sana. Nina uhakika hata ninyi wajumbe muliguswa sana. Alikuwa amepewa adhabu ya miezi 18. Hakukataa kutumikia adhabu ile.
Sasa niliona Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama tawala, chama chenye huruma. Chama chenye mapenzi mema. Chama dume. Niwaombe kwa huruma yenu kama itawezekana, huyu ndugu yetu ambaye amekubali mpaka sasa kutumikia adhhabu miezi mine, tumsamehe.
Kupitia kikao hiki napenda kusema Abdulrahman Omari Kinana amesamehewa rasmi. Niwashukuru wajumbe wa kikao hiki kwa huruma ya upendo
Yule mwingine ambaye hata jina lake sitaki kulitaja yeye ameshaondoka moja kwa moja. Adhabu yake si mnaikubali?
Ndugu mwenye ufinyu wa kuelewa historia ya siasa nchini kwetu ni wewe. Kwanza hujui kinana alivyoweza kufika hapa alipifikia. Kinana amelelewa kisiasa na Marehemu Mwalimu Nyerere, yeye ndiye aliyekuwa Mentor wake, na ndiye alifanya juhudi ya Kinana kupewa unaibu waziri awamu ya ya mzee mwinyi, na baadaye akawa waziri wa ulinzi, wakati wote huo Nyerere yuu Hai. Hata aliyemfanya kuwa campigner kwenye uchaguzi wa mkapa alikuwa Nyerere.Sababu umeandika baada ya tukio kutokea, hutaonekana hata kidogo una uelewa mpana wa mambo, ujue tukio likishatokea, alafu ukajitungia hadithi, haipati uzito au utamu, sbb ishajulikana event yenyewe, yaani ww unaremba remba tu na urembo ukizidi huonekana ni uchafu. Kinana ana uchafu wake mwingi tu kama binadamu, sio asset kubwa kama ww usemavyo, lakini amefanya mengi tu CCM hilo liko wazi, nikuulize, je ingekuwa enzi za waasisi kama Mwl Nyerere yuko hai, unafikiri angekubali Kinana kupewa cheo kikubwa CCM? Jibu unalo, hivyo yaliyotokea, usianze kuyatungia maneno yako binafsi, yaache ukweli au uongo unajulikana, waswahili husema kwa vitu vinavyojulikana usiwawekee maneno mdomoni mwao. Busara kaa kimya, labda udogo wako ktk uelewa wa mambo sio mkubwa sana. Uamuzi wa awali wa mh. Rais Magufuli kutoa adhabu ulikuwa sahihi sana sana tu, sbb anawajua hawa watu mmoja mmoja. Ila tunyamazee
Alifukuzwa kwanza, kabla hajarudisha kadi.Wamemfukuzaje wakati alishaondoka?
Jifunze kuishi na marafiki wa kweli na si wanafiki wanaokuchekea wakienda kwa bosi wanakugeuka.Membe alikuwa anadai Halmashauri kuu pekee ndo ina mamlaka ya kumfukuza uanachama na si kamati kuu,sasa kuweka kumbukumbu sawa hao aliowataka wagonge msumari ndo hao wamehitimisha ili asije kujifaragua baadae!
Akijitahidi sana ku-survive nje ya CCM ni miaka mitano.
Kwanza,atapoteza marafiki wa muda mrefu.
Pili, atapoteza washirika muhimu na wa siku zote.
Tatu,atakosa kilichompeleka huko aendako.
Nne,ata-swallow his pride na kurudi alikotoka.
Imeisha hiyo!!!
Sio kufukuzwa, ni kuthibitisha adhabu aliyopewa. Kufukuzwa ni siku nyingi na ndio maana Kinana alishaanza kutumikia adhabu ya miezi 18. Huyu anaekuja kwenu anawafanyia usanii tu ila anatambua fika alishatimuliwa na kwa vile anawajua ni nyumbu bado mtadai amejiondoa kisha mtaliwa kichwa.Wanamfukuza mtu ambaye tayari alisharudisha kadi na sio mwanachama wao?
Tunagoogle kujua nani alimpa sumu mangula kule meza kuu[emoji16][emoji16]View attachment 1502858
Wasanganye wakujaMembe alikuwa anasubiri maamuzi ya halmashauri kuu ya CCM kabla hajaamia chama cha upinzani!
Waliotupigania mpaka tukawa huru wangeangalia hayo mpaka leo tungekuwa bado tuko chini ya watawala wa kikoloni, unapopigania haki unayodhani kuwa pengine umenyimwa ni kujitoa muhanga wa kupata kile unachopigania au kupoteza rasimali zako mwenyewe, pengine na kupoteza maisha kabisa.Siyo kila Vita inayokujia ni lazima ushindane, sometimes ni vema uka surrender kwa manufaa ya baadae. Lowassa mwenyewe karudi CCM ila pengine si kwa ajili yake binafsi bali pia kwa kizazi chake maana Siasa za kiafrica huwa hazina mipaka, hata maisha yako binafsi yataingiliwa kukudhoofisha.
MEMBE ujeuri utamponza maana kiuhalisia bado ana kundi lake kubwa CCM AMBALO lingemchagua pengine 2025 ambapo itakuwa ni kama gombania goli kwa watia nia ya Urais Kupitia CCM ila kwa sasa anajisumbua tu.
Ni imani yangu hata kipindi hiki IKITOKEA Kura ya maoni, MEMBE anaweza mpiga chini MAGUFULI maana CCM wengi wanaojifanya kumuunga mkono Rais ni wanafki kwakuwa ndo hao hao waliokuwepo nchi ikitafunwa na wachache.