Abdulrahman Kinana asamehewa, Bernard Membe afukuzwa rasmi CCM

Pia ana sifa mbaya sana ya ubadhirifu wa mali ya asili hususani magendo ya meno ya tembo. Mwalimu aliwahi sema Mke wa Kaisari aliachwa sababu ya kutuhumia kutokuwa mwaminifu kwa Mumewe!!! Sasa tuache unafiki hapa…..
 
Membe alikuwa anadai Halmashauri kuu pekee ndo ina mamlaka ya kumfukuza uanachama na si kamati kuu,sasa kuweka kumbukumbu sawa hao aliowataka wagonge msumari ndo hao wamehitimisha ili asije kujifaragua baadae!

Akijitahidi sana ku-survive nje ya CCM ni miaka mitano.

Kwanza,atapoteza marafiki wa muda mrefu.

Pili, atapoteza washirika muhimu na wa siku zote.

Tatu,atakosa kilichompeleka huko aendako.

Nne,ata-swallow his pride na kurudi alikotoka.

Imeisha hiyo!!!
 
Kutubu bila kosa nako ni utumwa,ni heshima kufukuzwa kuliko kuomba msamaha kwa kosa ambalo halikuwa kosa ukabaki na heshima yako utahesabika ni shujaa asiyeendekeza njaa.
Kinana nadhani ni maslahi yamekuwa hatarini. Huyu mzee huko CCM amezoea kubebwa na kuheshimiwa sioni namna anavyoweza kuishi bila kupakatwa na Chama Tawala. Na nadhani mambo yake mengi pengine na familia yake yanategemea huruma za CCM. Hawa ndiyo wale ukienda ofisi za serikali utasikia wanasema ''huu ni mzigo wa mheshimiwa Kinana jamani, msiuchanganye na mingine''.
 
Mmiliki wa chama ataki mchezo
Wamiliki wa chama ni Mama Nyerere,Fatuma Karume.Wengine temporary membership kama UNO ya China,UK,Russia,USA,France permanet membership na Tanzania,Canada, Japan n.k temporary membership
 
Kutubu bila kosa nako ni utumwa,ni heshima kufukuzwa kuliko kuomba msamaha kwa kosa ambalo halikuwa kosa ukabaki na heshima yako utahesabika ni shujaa asiyeendekeza njaa.
Mnawadanganya wenzenu hivihivi wanatumbukia shimoni mnawaangalia halafu mnabaki mnawacheka. .
 
Unamfukuza mtu ambaye si mwanachama! Hana kadi ya CCM.
 
Ndugu mwenye ufinyu wa kuelewa historia ya siasa nchini kwetu ni wewe. Kwanza hujui kinana alivyoweza kufika hapa alipifikia. Kinana amelelewa kisiasa na Marehemu Mwalimu Nyerere, yeye ndiye aliyekuwa Mentor wake, na ndiye alifanya juhudi ya Kinana kupewa unaibu waziri awamu ya ya mzee mwinyi, na baadaye akawa waziri wa ulinzi, wakati wote huo Nyerere yuu Hai. Hata aliyemfanya kuwa campigner kwenye uchaguzi wa mkapa alikuwa Nyerere.

Ulizia wamjuaye Kinana alikuwa kipenzi cha nyerere. Hata Makongoro alipokuwa anaishi Arusha alikuwa akimtania kuwa Baba yake anampenda Kinana zaidi ya Makongoro
 
Jifunze kuishi na marafiki wa kweli na si wanafiki wanaokuchekea wakienda kwa bosi wanakugeuka.
Kwenye siasa hakuna rafiki wa kweli.
 
Wanamfukuza mtu ambaye tayari alisharudisha kadi na sio mwanachama wao?
Sio kufukuzwa, ni kuthibitisha adhabu aliyopewa. Kufukuzwa ni siku nyingi na ndio maana Kinana alishaanza kutumikia adhabu ya miezi 18. Huyu anaekuja kwenu anawafanyia usanii tu ila anatambua fika alishatimuliwa na kwa vile anawajua ni nyumbu bado mtadai amejiondoa kisha mtaliwa kichwa.
 
Waliotupigania mpaka tukawa huru wangeangalia hayo mpaka leo tungekuwa bado tuko chini ya watawala wa kikoloni, unapopigania haki unayodhani kuwa pengine umenyimwa ni kujitoa muhanga wa kupata kile unachopigania au kupoteza rasimali zako mwenyewe, pengine na kupoteza maisha kabisa.
 
Membe anajivunia ulinzi wake anauwezo wa kujilinda binfsi huyo mwingine ulinzi wa kulindwa je atakapo aliza muda wake wakikutana chobis itakuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…