Abdulrahman Kinana: CHADEMA wamelipwa ruzuku kiasi cha Billion 2.7

Abdulrahman Kinana: CHADEMA wamelipwa ruzuku kiasi cha Billion 2.7

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Abdulrahman Omari Kinana amedai Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kililipwa Tsh. Bilioni 2.7 ikiwa ni malipo ya ruzuku ya miaka mitatu kutoka Serikalini, mchakato ambao ulifanyika wakati wa mazungumzo ya maridhiano baina ya CCM na CHADEMA.

Amesema “Ruzuku inapitia katika Bajeti ya Serikali na ikishapita haipatikani tena lakini Rais (Samia Suluhu) akaagiza Serikali kutafuta utaratibu wa kuwalipa na wakasema mkitupa hizo hela itakuwa mwanzo mzuri wa kutambuana, wakalipwa lakini hawakuwahi kusema japo madai yao yalikuwa yamepitwa na wakati.”
Malcolm X aliwahi kusema " ukinichoma kisu mgongoni kikaingi inchi 9 halafu ukakitoa kwa inchi 6 sio maendeleo. Hata ukikitoa kabisa sio maendeleo. Maendeleo ni pale utakapotibu jeraha lililosababishwa na kisu ulichonichoma. Lakini mbaya zaidi hautaki hata kukubali kuwa ulinichoma kisu".

Amandla...
 
CCM yaendelea kulia kushindwa kuihadaa CHADEMA, vyama vingine vyote CCM imefanikiwa kuviweka mfukoni ila CHADEMA imeshindikana


View: https://m.youtube.com/watch?v=eH9KwRkB-IQ

Abdulrahman Kinana aelezea jinsi chama dola kongwe CCM chenye kila aina ya hadaa iliyoweza kuandikwa ktk simulizi za hadithi pamoja na rasilimali fedha nyingi vyombo vya dola lakini CCM imeshindwa kukitia mfukoni chama makini CHADEMA

Akizungumza na makada wa CCM walioonekana dhahiri kupigwa na bubuwazi , ambao kwa miaka mingi walidhani chama chao kina ushawishi mkubwa lakini leo wamegundua hizo ni hekaya za Abunuwasi kuwazia kitu wasicho nacho ....

Hadhira nzima ya makada waliojazana wameonekana kutahayari na kuanza kufikiria chama chao kongwe kuonekana dhaifu kupita muda wote wanaoukumbuka katika siasa za Tanzania.

CCM inaonekana imechoka na ipo dhoofu kama alivyowahi kusema Kingungwe Ngombale Mwiru alipoitazama CCM 2015 hadi ikabidi kuokolewa kwa njia haramu za kisiasa 2019 na 2020 chini ya utawala wa kidikteta uchwara wa awamu ya tano ...
 

,04 February 2024​

KINANA ACHAMBUA 'UBORA' WA SHERIA MPYA YA UCHAGUZI​

1707079244737.png

*Awashauri CHADEMA kuacha maandamano

*Asisitiza umoja, mshikamano na maridhiano

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU Makamu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulurhman Kinana, ameshauri vyama vya siasa vya upinzani hususan CHADEMA kuacha kufanya maandamano yasiyo na msingi badala yake wathamini nia njema aliyonayo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuleta maridhiano na kuwatumikia Watanzania.

Aidha, ametumia nafasi hiyo kufafanua kwa kina ubora wa sheria ya uchaguzi ambayo imepitihswa na Bunge hivi karibuni, baada ya wadau mbalimbali nchini kutoa maoni yao ambapo amesisitiza sheria hiyo ni bora kuliko iliyopo sasa.

Kinana aliyasema hayo jana Dar es Salaam alipozungumza na wana CCM na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, ambapo mbali ya kutumia muda mwingi kuzungumzia, maridhiano yaliyoingiwa kati ya CCM na CHADEMA pamoja vyama vingine vya upinzani, alisema kuna mambo mengi mazuri yamefanyika.

Alisema mambo mazuzi yamefanikisha kupata mwafaka ingawa CHADEMA haitaki kueleza ukweli ikiwemo serikali kukipatia chama hicho ruzuku ya Sh.bilioni 2.7 ambayo waliikataa kwa miaka mitatu nyuma.

Akielezea kuhusu sheria mpya, Kinana alisema pamoja na uzuri wake ikiwemo kuzingatia maoni ya wadau wakiwemo CHADEMA wenyewe, lakini bado kinasema haifai.

“Nilifikiri sheria hii mpya wangesema itatufikisha mbali zaidi, lakini wao wanasema hii haifai, basi turudi kule. Sheria ya sasa ni bora kwa muundo, kwa maudhui, kwa malengo, kwa dhamira sijui mnanielewa?. Nitumie nafasi hii kuwasihi ndugu zangu wa CHADEMA waungane na Watanzania waachane na mandamano, waangalie dhamira ya Rais.

“Hivi Rais na baraza lake la mawaziri kama wasingepeleka hii sheria mpya ya uchaguzi nani angemlazimisha? Lakini Rais busara imemuongoza akasema hapana hebu twende pamoja na mimi ndio mtetezi mkubwa wa maridhiano na ustahimilivu. Hebu tupeleke sheria mpya bungeni na kila hoja aliyopelekewa, aliyoambiwa kwamba haya ndio maoni ya wadau Rais akasema sawa, nakubali.

“Sasa niwasihi ndugu zangu Watanzania, tujipange kwa uchaguzi wa serikali za mitaa, tujipange kwa uchaguzi mkuu mwaka 2025. Sheria hii ni nzuri, bora kuliko sheria yoyote iliyopo katika historia ya nchi yetu, inakidhi mahitaji na matakwa ya nchi na jumuiya ya madola, inakidhi mahitaji ya nchi za Umoja wa Afrika (AU), inakidhi vile vile mahitaji ya nchi za Kusini mwa Afrika ambao na sisi ni wanachama,” alisema.

Aliongeza kwamba hakuna tume ya miujiza zaidi itakayokuwepo, huku akifafanua kila jambo ambalo litafanyika lazima litakuwa na kasoro moja au mbili, na kuhoji kwani CHADEMA wao hawana kasoro?.

“Wanazo, sasa nawaambia ninyi chama kikuu cha upinzani kuweni basi na ustahimilivu kidogo, uungwana na kusikiliza wenzenu na kuona nia njema iliyopo katika Chama Cha Mapinduzi, kwa na serikali yake,” alisema.

Akifafanua zaidi Kinana alisema kuwa kushinda uchaguzi kunatokana na sera, mipango ya uchaguzi na kusikiliza watu, kwani unaweza kuwa na tume nzuri ya uchaguzi na matokeo yakawa ni ya hovyo, usiyoyataka.

Alitoa mfano wa moja ya nchi jirani ambayo walipigania sana kuwa na tume huru kwa miaka 20, wakaipata, lakini wamegombea mara nne hawakupata.

“Hawakuingia madarakani, wale waliotengeneza hiyo tume hawakupata, sasa wanasema Katiba hii haina maana waifute, wale walioingizwa na katiba baadae nao wakashindwa wanasema katiba hii haina maana. Kwa hiyo aliyeshinda anasema Katiba haina maana na aliyeshindwa naye anasema Katiba haina maana.

“Sasa kushinda uchaguzi sio Katiba tu, Nigeria baada ya wanajeshi kutoka baradakani walitengeneza Katiba mpya mwaka 1969 na kwa sehemu kubwa walienda kuchukua Katiba ya Marekani, tume ya uchaguzi ya Rais inateuliwa na Rais kwa kushauriana na baraza la ushauri.

“Baraza la ushauri ni nani? Rais ndio Mwenyekiti, makamu mwenyekiti ni makamu wa rais, wajumbe wengine marais wastaafu, hapo vipi? Kuna mtu anatoka nje ya mfumo?

“Hao ndio wanateua, mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa tume, uchaguzi unafanyika na watu wanakubali. Hapa tunatafuta malaika wa kuja kuongoza tume, kila utakachofanya unaambiwa kinakasoro, hivi mnavyoona yote tuliyokubali wanasema hamna kitu.

“Nimesikia wanaandaa maandamano Mwanza, Mbeya na Arusha na mimi nataka niwasaidie kutangaza kama watu wengine hamjasikia. Wanakwenda kueleza haya yaliyopitishwa na CCM na Bungeni hamna kitu.

“Tume si kila kitu, Namibia kamati inatengenezwa baada ya pale anayetua Rais, kuna nchi inaitwa Mauritius na hizi nchi zote ambazo nimezitaja ni za Jumuiya ya Madola, Rais anashauriana na watu wawili tu, anashauriana na waziri mkuu na kiongozi wa upinzani bungeni hakuna mtu mwingine,” alisisitiza.

“India wana mkurugenzi na wana makamishina. Nani anateua? Waziri Mkuu na Baraza lake la Mawaziri kwisha, yaani Rais Samia akae na baraza lake la mawaziri atengeneze orodha ateue, si moto utawaka hapa? Watasema tu maigizo.

“Sasa kuna shida hapa nchini kila unalofanya halina heri ndani yake, lakini vizuri haya mambo tukayaeleza maoni mengine yakatolewa unajua siku hizi kuna watu wanapita bila kupingwa lakini ni vizuri wanaopita bila kupingwa wakapigiwa kura ya ndio au hapana Bunge likasema sawa tumekubali.

“Wanauliza kwa nini? Wanasema kuna watu wengine wanafanya ujanjaujanja wa kupita bila kupingwa, hivyo wapigiwe kura tujue kama wanakubalika Bunge limesema sawa itapigwa kura ya ndio au hapana,” alisema.

KUHUSU MARIDHIANO

Akizungumzia maridhiano ambayo yamefanyika kwa nyakati tofauti, Kinana alisema kuwa wakati Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani kulikuwa na wanachama wa CHADEMA wasiopungua 400 wako mahabusu wakikabiliwa na kesi zilizotokana na sababu mbalimbali za kiuchaguzi, lakini ulitengenezwa utaratibu wa kisheria waakachiwa huru.

Kinana alisema hakuna maridhiano bila ustahimilivu, Rais alialika taasisi za kidini na kiraia ili waelewane kujiuliza nini wanahitaji kwa lengo la kuhakikisha tunakuwa na taifa liwe la watu wenye mshikamano na kupendana.

Alisema Dk. Samia aliunda tume ya kusikiliza makundi ya Watanzania kusikiliza hoja zao ikiwemo Katiba, lakini mwishowe CHADEMA waligomea kwa sababu zao
 
Wanasemaje sasa , tumeshangaa tu mwenyekiti kazindua mjengo wake rosheni la ghrofa kule machame mwezi desemba mwaka jana.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Abdulrahman Omari Kinana amedai Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kililipwa Tsh. Bilioni 2.7 ikiwa ni malipo ya ruzuku ya miaka mitatu kutoka Serikalini, mchakato ambao ulifanyika wakati wa mazungumzo ya maridhiano baina ya CCM na CHADEMA.

Amesema “Ruzuku inapitia katika Bajeti ya Serikali na ikishapita haipatikani tena lakini Rais (Samia Suluhu) akaagiza Serikali kutafuta utaratibu wa kuwalipa na wakasema mkitupa hizo hela itakuwa mwanzo mzuri wa kutambuana, wakalipwa lakini hawakuwahi kusema japo madai yao yalikuwa yamepitwa na wakati.”

Kumbe Kinana ni mpuuzi kiasi hiki?

Hiyo pesa ya ruzuku, yangu wakati wa marehemu Magufuli, CHADEMA waliambiwa waichukue lakini CHADEMA ndio waliokataa. Hivyo kuipata wakati huu siyo jambo la pekee maana Ilihitaji tu CHADEMA kukubali kuchukua, na siyo hisani ya Rais.

Kinana atuambie pia CCM huwa inachukuà bilioni ngapi kila mwezi, na mpaka sasa imechukua bilioni ngapi. Na atuambie ni lini waliwahi kuwaambia wananchi kila wanapoichukua. Vinginevyo, maelezo yote ya Kinana ni ujinga na unafiki wa hali ya juu.
 
Kumbe Kinana ni mpuuzi kiasi hiki?

Hiyo pesa ya ruzuku, yangu wakati wa marehemu Magufuli, CHADEMA waliambiwa waichukue lakini CHADEMA ndio waliokataa. Hivyo kuipata wakati huu siyo jambo la pekee maana Ilihitaji tu CHADEMA kukubali kuchukua, na siyo hisani ya Rais.

Kinana atuambie pia CCM huwa inachukuà bilioni ngapi kila mwezi, na mpaka sasa imechukua bilioni ngapi. Na atuambie ni lini waliwahi kuwaambia wananchi kila wanapoichukua. Vinginevyo, maelezo yote ya Kinana ni ujinga na unafiki wa hali ya juu.
Kinana asingesema tungejua kama Chadema walishabadili maamuzi na kuamua kuchukua ruzuku au tungeendelea kudhani Chadema bado hawachukui ruzuku?
 
Chadema wamelipwa Tsh Bilioni 2.7 kama ruzuku

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Abdulrahman Kinana amedai moja kati ya masharti ambayo waliomba CHADEMA ni kulipwa ruzuku yao ya miaka 3.

Kinana amesema ombi hilo lilikuwa gumu kutokana na ruzuku hutokana na bajeti ya serikali katika mwaka husika.

Kinana amesema ingawa ilikuwa ngumu Rais Samia aliagiza pesa hiyo itafutwe ili walipwe.
Ushahidi
 
Chadema wamelipwa Tsh Bilioni 2.7 kama ruzuku

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Abdulrahman Kinana amedai moja kati ya masharti ambayo waliomba CHADEMA ni kulipwa ruzuku yao ya miaka 3.

Kinana amesema ombi hilo lilikuwa gumu kutokana na ruzuku hutokana na bajeti ya serikali katika mwaka husika.

Kinana amesema ingawa ilikuwa ngumu Rais Samia aliagiza pesa hiyo itafutwe ili walipwe.
Kwanini Kinana hakutaja ruzuku na pesa nyingine inayochotwa na CCM? Chadema ikilipwa ni nogwa lakini CCM ikichota fedha na kuwanunua baadhi ya viongozi toka vyama vya upinzani siyo tatizo.

Watu tusiwe mazuzi, kwenye chaguzi tumeona ambavyo CCM utumia kodi zetu hovyo kuhakikisha inabaki madarakani. Hiyo ruzuku kama kweli imetolewa ni tone tu ukilinganisha na ili inayotumiwa na CCM. Nani ambae hakaona misafara ya Makonda?
 
..ukiona Chadema wamelipwa bilioni basi ujue CCM wamepata trillioni.

..msifikiri ipo siku CCM wataruhusu chama chochote kiwe na fedha au rasilimali kuliko wao.
Ni majambazi
 
Tuache siasa za hovyoo! Kwani sio mbowe aliyekataa ruzuku akisema hautambui uchaguzi?. Mbowe ana makandokando mengi Sana..... Mbona hakusema hili kuwa ni sehemu ya masharti ya maridhiano?. Chadema imefikia pabaya HAKUNA ukweli na uwazi!.
Wewe hutumii akili,
Unajua maana ya muafaka?
 
Tuache siasa za hovyoo! Kwani sio mbowe aliyekataa ruzuku akisema hautambui uchaguzi?. Mbowe ana makandokando mengi Sana..... Mbona hakusema hili kuwa ni sehemu ya masharti ya maridhiano?. Chadema imefikia pabaya HAKUNA ukweli na uwazi!.
Kajinyonge basi tujue umechukia wewe chawa
 
Haya ndio Mambo amabayo mbowe hakutaka kuyaweka wazi wakati wa maridhiano!!, Ona wanavyomuumbua Sasa!, Ni aibu kuwa na kiongozi ambaye sio muwazi katika Mambo ya umma!.
Sema wewe hustahili kuyajua maana huko kwenu ccm huna nafasi
 
Hizi habari wenyewe hawawezi kuziweka public,ni wanafiki balaa.

Zile za kukataa ruzuku wanaita press halafu wakivuta wana-mute.

Ndiyo maana kilichomo kwenye maridhiano ni siri na si ajabu na Chiba keshavuta chake.
Umesahahu kuwa mzee mbowe ndio Mwenye kampuni?
 
Acha upotoshaji wa kijinga, sio mara Moja au 2 cdm wameweka wazi kupatiwa hiyo ruzuku, na viongozi wa cdm wakawa wanatoa ufafanuzi kwa wanachama wake kama sehemu ya kuwaplease kuwa maridhiano yana maana. Ifahamike wafuasi wengi wa cdm hawana imani na hayo maridhiano, Wala hawayataki.
Kama hawatakia mbona Lissu na mzee mbowe wanalalama?
 
Back
Top Bottom