benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Abdulrahman Kinana
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amemwandikia barua ya kuomba kupumzika.
Katika majibu yake Mwenyekiti wa CCM amesema "Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako".
Pia Mwenyekiti wa CCM amesisitiza kuwa Chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Ndugu Kinana kila vitakapohitajika.
Chama Cha Mapinduzi kinamshukuru Ndugu Abdulrahman Kinana kwa mchango wake mkubwa kwa Chama chetu.
PIA SOMA
- Matokeo CCM: Abdul Kinana Makamu Mwenyekiti Bara, Hussein Mwinyi Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Samia Hassan Suluhu Mwenyekiti Taifa