Pre GE2025 Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia

Pre GE2025 Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Yeyote aliyewahi kuwa mwandani wa Kikwete ana ubinafsi na hana mapenzi ya dhati na taifa hili; mapenzi yake yako kwenye maslahi yake binafsi na familia yake.
 
View attachment 3056347
Abdulrahman Kinana

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amemwandikia barua ya kuomba kupumzika.

Katika majibu yake Mwenyekiti wa CCM amesema "Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako".

Pia Mwenyekiti wa CCM amesisitiza kuwa Chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Ndugu Kinana kila vitakapohitajika.

Chama Cha Mapinduzi kinamshukuru Ndugu Abdulrahman Kinana kwa mchango wake mkubwa kwa Chama chetu.

PIA SOMA
- Matokeo CCM: Abdul Kinana Makamu Mwenyekiti Bara, Hussein Mwinyi Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Samia Hassan Suluhu Mwenyekiti Taifa

Ukweli usemwe ,naona hali sio shwari ndani ya ccm.
 
Hawa mawaziri wakuu wastaafu,kuna mmoja atachaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
 
Nice Speculation,but she's there to stay,she's there to lead us up to 2030 Inshallah...
Nimeipenda hii, na huu ndio ni ukweli.
Ile milenium iliyosemwa kuja na maajabu, wakati wake ni sasa. Wengi walidhani kuwa tar 1.1.2000 ndio kutatokea mambo. Vitu kama hivi huchukua muda mpaka vitokee toka point iliyoainishwa.

Ipo hivi- Afrika ina chance ya pili baada ya ile ya kwanza ya kupata UHURU. Kwa maneno mengine Era ya kuzungumzia habari za UHURU ziliishia milenium "2000". Matukio mengi yatatokea kila nchi Afrika na yana maana kubwa.
Kwa Tanzania Era hiyo ilianzia na UJIO WA MAGU.Hakuna aliyemtegemea kwa Heavy weight zilizokuwepo. Na baadae ni UJIO WA MAMA SAMIA- Huu ndio wa ajabu zaidi. Yote haya ni mpango wa nguvu kubwa sana usizozijua** na nia (ishara) ni kuikomboa Tanzania.
Kinachoendelea nyakati hizi ni Mapambano ya nguvu mbili. Ile asilia ya mazoea (ukipenda mafisadi) na nguvu ya pili ni ya mabadiliko (inayoangalia wananchi/walala hoi). Amini usiamini hii nguvu ya MABADILIKO ndio itashinda bila kujali chama kwa sababu ina wananchi. Tuna uchaguzi: Tuunge mkono KIZA au NURU. Kwa wasio ona nawashauri....Tuipiganie NURU kwa nguvu zote itatuvusha.
Na hapa ndio maneno haya yanahitimisha......she's there to stay,she's there to lead us up to 2030...and beyond.
Alamsik!
 
Mzee anasema anaumwa yupo kitandani, sasa barua ya kujiachisha kazi kaandika muda gani?
May be kaandikiwa,na kwani Kuna ubaya Gani akiomba kupumzika?

So to say hakuna namna kabisa CCM inaweza kwenda bila ya Makamu Kinana?

After all Kwa upinzani Gani Sasa hivi wa kuwahofia kiasi Cha kuogopa eti Kinana akipumzika?
 
Hii si bure bali kuna jambo.

Huenda ule utenguzi wa wale jamaa unahusika.

CCM kimwili wako pamoja, ila kiroho wana makundi tena yanayotafunana kuelekea 2025.

Uzanzibari na uzanzibara ni petrol katika moto unaofukuta.

Wanamchekea Bi. Mkubwa ila sidhani kama wanampenda na wanapenda 2025 arudi ofisini.

Kwa madaraka makubwa ya kikatiba na yale ya ndani ya chama, akikomaa atavuka, ila watu wanaweza ku-defect dakika za mwisho na kumuweka katika mazingira magumu unless akumbatie kundi linalotajwa kumpinga na kutaka kiti chake.

Amkumbatie sana JK walau anaeweza kumsaidia kutuliza hali ya mtambo iwapo yatatokea ya kutokea.

Jinsia nayo ni tatizo lingine, na ukiongeza na tuhuma za kutapanya maliasili za watanganyika, naiona hatari kubwa sana mbele yake.

Muda utaongea.
Ipo hivi bi mkubwa alipewa ashike kwa muda baada ya jamm kuuangusha mbuyu, sasa mama kanogewa anawageuka wazee kwa kushikilia kiti baada ya kunogewa
 
Hii si bure bali kuna jambo.

Huenda ule utenguzi wa wale jamaa unahusika.

CCM kimwili wako pamoja, ila kiroho wana makundi tena yanayotafunana kuelekea 2025.

Uzanzibari na uzanzibara ni petrol katika moto unaofukuta.

Wanamchekea Bi. Mkubwa ila sidhani kama wanampenda na wanapenda 2025 arudi ofisini.

Kwa madaraka makubwa ya kikatiba na yale ya ndani ya chama, akikomaa atavuka, ila watu wanaweza ku-defect dakika za mwisho na kumuweka katika mazingira magumu unless akumbatie kundi linalotajwa kumpinga na kutaka kiti chake.

Amkumbatie sana JK walau anaeweza kumsaidia kutuliza hali ya mtambo iwapo yatatokea ya kutokea.

Jinsia nayo ni tatizo lingine, na ukiongeza na tuhuma za kutapanya maliasili za watanganyika, naiona hatari kubwa sana mbele yake.

Muda utaongea.

Watumbuliwa wawili na mjiuzulu wote wapo team moja na JK, na bibie tayari alimkorofisha mentor wake (JK) kwa hali ilivyo kuna game linasukwa na bibie nae ameamua liwalo na liwe na anajiwekeza kwa kasi sana, maana anajua kuna mfumuko wa bomu unasukwa naye ameshaamua liwalo na liwe tu.

Mungu ikomboe Tz kupitia wateule wako waaminifu.
 
View attachment 3056347
Abdulrahman Kinana

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amemwandikia barua ya kuomba kupumzika.

Katika majibu yake Mwenyekiti wa CCM amesema "Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako".

Pia Mwenyekiti wa CCM amesisitiza kuwa Chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Ndugu Kinana kila vitakapohitajika.

Chama Cha Mapinduzi kinamshukuru Ndugu Abdulrahman Kinana kwa mchango wake mkubwa kwa Chama chetu.

PIA SOMA
- Matokeo CCM: Abdul Kinana Makamu Mwenyekiti Bara, Hussein Mwinyi Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Samia Hassan Suluhu Mwenyekiti Taifa

Attachments

  • 5919930-954df270905012ee1220d2072789d42b.mp4
    6.9 MB
Back
Top Bottom