Pre GE2025 Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
View attachment 3056347
Abdulrahman Kinana

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amemwandikia barua ya kuomba kupumzika.

Katika majibu yake Mwenyekiti wa CCM amesema "Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako".

Pia Mwenyekiti wa CCM amesisitiza kuwa Chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Ndugu Kinana kila vitakapohitajika.

Chama Cha Mapinduzi kinamshukuru Ndugu Abdulrahman Kinana kwa mchango wake mkubwa kwa Chama chetu.

PIA SOMA
- Matokeo CCM: Abdul Kinana Makamu Mwenyekiti Bara, Hussein Mwinyi Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Samia Hassan Suluhu Mwenyekiti Taifa

Leteni katiba mpya vinginevyo hatuwaelewi
 
Baada ya uchaguzi wanateuana tena na kuombana misamaha ya kinafki kuwa hadaa Waitwao wanyonge na kuendelea kuzikamua kodi zao kwa anasa na kufruh na familiar zao huku wakiuza rasimali katika nchi ya Waitwao wanyonge ###SiKwaBahatiMbaya,YamepangwaHaya###Wasituone Mazuzu hawa Walafi
 
Huyu Mzee aliomba kupumzika siku nyingi sana.
Acha uongo! Amepatikana hakuna jinsi lazima aondoke lasivyo ilikuwa lazima aondolewe. Tafuta video clips za ziara za mama Katavi utamwona huko akihangaika.... hahahaha...
 
View attachment 3056347
Abdulrahman Kinana

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amemwandikia barua ya kuomba kupumzika.

Katika majibu yake Mwenyekiti wa CCM amesema "Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako".

Pia Mwenyekiti wa CCM amesisitiza kuwa Chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Ndugu Kinana kila vitakapohitajika.

Chama Cha Mapinduzi kinamshukuru Ndugu Abdulrahman Kinana kwa mchango wake mkubwa kwa Chama chetu.

PIA SOMA
- Matokeo CCM: Abdul Kinana Makamu Mwenyekiti Bara, Hussein Mwinyi Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Samia Hassan Suluhu Mwenyekiti Taifa

Baada ya vijana wake wa kushoto na kulia kutemwa amejiona hayuko salama ndio maana anajiondoa kuepuka aibu mbeleni.
 
Hii si bure bali kuna jambo.

Huenda ule utenguzi wa wale jamaa unahusika.

CCM kimwili wako pamoja, ila kiroho wana makundi tena yanayotafunana kuelekea 2025.

Uzanzibari na uzanzibara ni petrol katika moto unaofukuta.

Wanamchekea Bi. Mkubwa ila sidhani kama wanampenda na wanapenda 2025 arudi ofisini.

Kwa madaraka makubwa ya kikatiba na yale ya ndani ya chama, akikomaa atavuka, ila watu wanaweza ku-defect dakika za mwisho na kumuweka katika mazingira magumu unless akumbatie kundi linalotajwa kumpinga na kutaka kiti chake.

Amkumbatie sana JK walau anaeweza kumsaidia kutuliza hali ya mtambo iwapo yatatokea ya kutokea.

Jinsia nayo ni tatizo lingine, na ukiongeza na tuhuma za kutapanya maliasili za watanganyika, naiona hatari kubwa sana mbele yake.

Muda utaongea.
Napata ugumu wa kuamini kuwa uuzaji wa maliasili ni uamuzi wa ntu mmoja.
 
Mkuuu kikwete wanini tena hapa wacha mama apambane mwenyewe ili atakaposhinda kusiwe na fadhila zozote kumrudishia mtu, mama ana kila kitu kashika kwenye mpini, wote ambao wako chini yake wameshika kwenye makali mimi napendekeza aongeze tenguzi kwa wale wote ambao wanamhujumu kwenye hustle zake zote.

Aongeze watu anawaowaamini na watakao msaidia hii nchi ina viongzi wengi wakongwe na waandamizi wengi hakuna kumuogopa mtu et kwa sababu ana background fulani

Mama pambana ukishindwa umeshinda umeshinda umeshinda
 
Mnamkuza sana Kikwete ilhali ni mwepesi kuliko karatasi! Kikwete na mtandao wake ulimalizwa haraka sana na Magufuli akabaki hoi bin taabani.

Mtandao pekee ambao haukufa na Magufuli aliamua kusalimu amri kwao na kuungana nao ni Lowassa na Rostam Aziz ambao kijana wao mtiifu na mpendwa ndo huyo Nchimbi kwa sasa!

Huyo JK hana lolote mnalotaka kuaminisha watu zaidi ya mvizia fadhila tuu.
Samia ni product ya Kikwete. Sasa team Kikwete akawa mgombea mwenza wa Magufuli na ndiye Rais wa sasa.

Katibu mkuu TISS aliyepita ni team Kikwete.

Kinana ni team Kikwete na ndio katoka umakamu mwenyekiti.

January, Nape, Makamba ni team Kikwete na mawaziri watatu wote walikuwa baraza la Rais Samia.

Mtoto wa Kikwete yupo kwenye baraza la Samia.

Haya tutajie mtandao wa Rostam Aziz na Lowassa uliokuwepo madarakani hata wakati wa Magufuli. Nchimbi kitu gani huyu mweupe hafikii hata nusu ya influence ya Makonda. Kwamba Rostam Aziz anamzidi Kikwete influence? Ndoto za mchana
 
Hii si bure bali kuna jambo.

Huenda ule utenguzi wa wale jamaa unahusika.

CCM kimwili wako pamoja, ila kiroho wana makundi tena yanayotafunana kuelekea 2025.

Uzanzibari na uzanzibara ni petrol katika moto unaofukuta.

Wanamchekea Bi. Mkubwa ila sidhani kama wanampenda na wanapenda 2025 arudi ofisini.

Kwa madaraka makubwa ya kikatiba na yale ya ndani ya chama, akikomaa atavuka, ila watu wanaweza ku-defect dakika za mwisho na kumuweka katika mazingira magumu unless akumbatie kundi linalotajwa kumpinga na kutaka kiti chake.

Amkumbatie sana JK walau anaeweza kumsaidia kutuliza hali ya mtambo iwapo yatatokea ya kutokea.

Jinsia nayo ni tatizo lingine, na ukiongeza na tuhuma za kutapanya maliasili za watanganyika, naiona hatari kubwa sana mbele yake.

Muda utaongea.
IMG-20240729-WA0011.jpg
 
Mnamkuza sana Kikwete ilhali ni mwepesi kuliko karatasi! Kikwete na mtandao wake ulimalizwa haraka sana na Magufuli akabaki hoi bin taabani.

Mtandao pekee ambao haukufa na Magufuli aliamua kusalimu amri kwao na kuungana nao ni Lowassa na Rostam Aziz ambao kijana wao mtiifu na mpendwa ndo huyo Nchimbi kwa sasa!

Huyo JK hana lolote mnalotaka kuaminisha watu zaidi ya mvizia fadhila tuu.
Ficha ujinga wako. Labda kama ni mgeni sana wa siasa za nchii ndo unaweza kuandika huu ujinga.
 
Back
Top Bottom