py thon
JF-Expert Member
- Sep 11, 2016
- 2,476
- 4,448
Mshambuliaji wa Ruvu shooting na mfungaji bora wa ligi ya Tanzania bara 2016/2017 Abdulrahman Mussa amemjibu kocha wa Taifa stars kuwa hayupo sahihi kama alivyosema Jana kwenye utetezi wake dhidi ya kashfa ya upendeleo anaoufanya kwenye kuita na kuchagua kikosi.Kocha Mayanga alisema jana kuwa Abdulrahman Musa alikuwa mgonjwa hivyo alikuwa hamtumii lakini taarifa hizo zimemstua mshambuliaji huyo wa Ruvu shooting nakusema hizo taarifa ni za uongo na labda Mayanga angetoa sababu zingine kama hafai kwenye mfumo wake au sababu zingine lakini sio kumsingizia kuwa alikuwa mgonjwa.
Hivi karibuni kocha wa Taifa stars amekuwa akilalamikiwa kuwa na upendeleo katika kuita wachezaji na upangaji wa kikosi wengi wanadai mwalimu huyu anapendelea kuwatumia wachezaji wa klabu moja kongwe hapa nchini licha baadhi ya wachezaji hao kuonekana hawana sifa au uwezo wa kuanza.