Soma BIblia mwanzo hadi mwisho, mara zote ukiona mwanamke ametajwa ujue kuna jambo maalumu alilifanya; nitafafanua.
- Kama umesoma historia ya Yakobo au Israel yule baba wa wana 12 ambao ndio makabila ya Israel inaonesha alizaa watoto 12 ambao ndio makabila yao but wakati anakwenda Misri imeandikwa kwamba idadi ya wana waliotoka katika viuno vya huyu mzee wa Imani ni 72, maanake ni wa kike pekee yake walikua 60, motto pekee wa kike anae tajwa katika listi ya wana wa Israel ni Dina peke yake and why, because alibakwa na wale wana wa Wahiti.
- Yesu alilisha zaidi ya watu 5000 but Biblia imesema wazi kabisa kwamba idadi hiyo ni wanaume tu, unadhani watoto na wanawake hawakuwepo kwenye mkutano wake ule!?
- Idadi ya waliotoka Misri to Kaanani ni kama watu laki sita but hiyo ni wanaume tu tena wenye uwezo wa kwenda vitani, what about wanawake na watoto bila kujali jinsia zao!?
Kwa ushahidi huo nina hakika Adamu na Hawa walizaa watoto wengi hasa wa kike zaidi ya Kaini, Habili na Seth.