Abiria SGR wasota stesheni, Mvua zakwamisha safari za Treni

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema limepata changamoto kwenye mfumo wa umeme karibu na Stesheni ya Ruvu mkoani Pwani, hali iliyosababishwa na mvua inayoendelea kunyesha nchini.

1766920161209.png
Akizungumza na Swahili Times, Afisa Habari wa TRC, Fred Mwanjala amesema kwa sasa mafundi wako eneo la tukio kuhakikisha wanarejesha miundombinu ili huduma za usafiri zirejee kama kawaida.

"Napenda kuwaomba radhi abiria wetu kwa changamoto iliyojitokeza, hilo ni suala ambalo huwezi kuliepuka ni suala la kiufundi," amesema Mwanjala.

Shirika hilo limewashukuru Watanzania kwa kuwa wavumilivu nyakati zote.
 
Duh natoka Moro kurudi Dar at 1925 hii nayo ita delay? Au nikapande bus tu?
 
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema limepata changamoto kwenye mfumo wa umeme karibu na Stesheni ya Ruvu mkoani Pwani, hali iliyosababishwa na mvua inayoendelea kunyesha nchini.

Akizungumza na Swahili Times, Afisa Habari wa TRC, Fred Mwanjala amesema kwa sasa mafundi wako eneo la tukio kuhakikisha wanarejesha miundombinu ili huduma za usafiri zirejee kama kawaida.

"Napenda kuwaomba radhi abiria wetu kwa changamoto iliyojitokeza, hilo ni suala ambalo huwezi kuliepuka ni suala la kiufundi," amesema Mwanjala.

Shirika hilo limewashukuru Watanzania kwa kuwa wavumilivu nyakati zote.
hakuna maji sababu - Hakuna mvua

SGR imegoma kwenda sababu - mvua imenyesha.

sisi ni mafala au malofa?
 
Back
Top Bottom