DOKEZO Abiria wa Basi la Shabiby tulalamikia huduma mbovu za hoteli Morogoro tunaomba mbadilishe haraka hoteli

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Akili imejaa nyama ya mbuzi
 
Ongezea na kuharibu vifaa kwenye vyombo vya usafiri.. Nilienda Kigoma na Bus mpya tuu inaitwa AIFOLA nikakuta charging system karibia zote zimekufa.. Mimi nasubiri nione hizo treni za mwendo kasi kama zitadumu...
Wataharibu tu na kupiga chata za maandishi ya hovyo hovyo

Hatuna asili ya ustaarabu.
 
Kwa kweli hii issue inakera sana. Especially kuna sehemu moja hivi barabara ya Iringa vyoo ni vidogo utadhani vya watoto wadogo halafu sidhani kama huwa wanavisafisha
 
Basi iko hio moja tu? Watanzania wengi ni mazezeta sana sijui nani aliwaroga, fullu uzezeta, yaani ujinga,
 
Aisee Moro to Dodoma bado sijaona sehemu ya kueleweka Kula msosi, When it comes to best Motels, Arusha to dar has the best
Ondoka na chakula chako, ninua hata kuku na ndizi za kuchoma, na soda au maji, mnapenda kulalamika lalamika , mnataka Samia awasaidie?
 
Panda ABC ukale HOTEL sio sehemu ya kuchimba dawa
 
Naunga mkono kabisa choo kichafu kisawasawa, sijui Bwana Afya wa Morogoro alikufa na hajateuliwa mwingine au yuko kwenye payroll ya hoteli hiyo. Chakula pia kibovu, ingekuwa abiria wa Arusha - Moshi wasingepanda hilo gari kabisa. Shabiby jiangalie au Mbunge Shabiby pitia pale ukija Dar toka Dodoma, usipande ndege
 
Pumbavu mnapanda bure au? Mabasi yote haya?
 
Kapandeni BM au ABC kama unataka raha......shabiby hawawezi kuacha kusimama pale maana abiria sio priority yao
 
Umegonga penyewe. Tanzania kuna institutional failure ya hali ya juu sana. Sijui tumefikaje hapa. Mbaya ni kuwa watu wote, siyo viongozi, siyo wananchi, wameshakubaliana na hali. Kwa mfano hili lalamiko la mwenye thread chanzo chake ni kuruhusu watu kujenga hoteli maporini na kulazimisha wale kwenye hizo sehemu. Mbona zamani utaratibu ulikuwa ni kusimama stendi za umma ambako kulikuwa na hoteli zenye ushindani na huduma nzuri?
 
ABC ni the best, na mimi nilikuwa abiria mtiifu wa kampuni moja kutoka Njombe -Dar, juzi nikashauriwa kupanda ABC na baba yangu aisee sikujutia na rasmi nimehamia huko. Nilisafiri na mtoto na alikuwa comfotable. Vyoo visafi, customer care nzuri ndani ya basi abiria unasafiri kw a raha. Mtoa mada jaribu ABC utaona experience yake pia Cate Hotel utafurahia huduma zao.
 
Dar Dom mabasi yapo mengi sana
 
Hii pia nimewahi kuona
Basi zuri huduma nzuri ila Mheshimiwa Shabiby hawa madreva wako wanapeleka basi kusimama kwenye hoteli chafu chafu za hovyo zisizoendana na heshima ya gari zako pale msamvu kwa nyuma kwenye magesti .Okoa jahazi!
Ni hatari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…