KERO Abiria wa Mwendokasi tuliotakiwa kutoka Kivukoni kwenda Kimara, Dereva katupeleka Morocco kisha akaturudisha Kivukoni

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
kwa mwendokasi ya kimara kama serikali wanashindwa ivyo kuhudumia watu ,sipati picha siku itakapoanza safari ruti ya mwendokasi ya Mbagara nawasihi tu hao madereva wawe na nidhamu ya hali ya juu,abiria wa mbagara hawawezagi ujingaujinga huo
 
Kwa hali ilivyo mwendokasi (Kivukoni - Kimara) Bora mwingereza angebami kututawala tuu. Labda tungefika mbali. Hali ni mbaya kuliko
Hicho ni kipimo kwa watawala. Manake hapo ni karibu na Ikulu kwa watu wa kivukoni.

Hakukuwa na haja ya kuagiza ndege wakati huku chini makabwela wengi wanateseka kwa usafiri wa mwendokasi. Hesabu za wapi hizo?
.
Ambao hao makabwela kesho unategemea wakupe kura
 
Hawana hasara hao mshaharA wao mwisho wa mwezi
 
mara ya mwisho kupanda
nilikua msimbazi nmekaa wee nkaona niunge unge usafiri likaja la morocco nikapanda nikajua nashukia mapipa. La haulaa! Naona kitu kinachoma muhimbili nililaani sana
 
Shida hizi kazi wanazipata kwa connection
 
TUNAMSHUKURU SANA MAMA, KWA KITENDO CHA MZEE KUPIGA SIMU KWA WAZIRI.
 
Sie wa mikoani mwanzoni tulikua tukisikia mwendo kasi tulikua tunatamani sana,nakumbuka siku moja nashuka pale magufuli bus stand..nikasema ngoja leo nijaribu nione yaliyomo yamo..dah nilijuta! Ni usafiri wa hovyo sana!
 
Madereva wa mwendokasi ni wababe sana,majuzi abiria walisema tumejaa tunaumia usipandishe wengine,dereva akaona akisimama wengine watapanda akawa hasimami vituoni na hakuwarudisha abiria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…