Abiria wa Tanzania akamatwa Hong Kong na heroin ikiwa ndani ya mashine

Abiria wa Tanzania akamatwa Hong Kong na heroin ikiwa ndani ya mashine

huyu jamaa nae yani unapeleka spare part hong khong lazima udakwe

Hahahaha kweli za mwizi arobaini yani anapeleka spare part kutoka Tanzania kwenda Hong khong? kweli jamaa zilifika siku zake za kukamatwa mwache achezee kibano.
 
Ndugu ebu tuweke wazi mbona hizo mashine ni tofauti? hiyo nzima hailingani na hiyo iliyokatwa inawezekana kuna udanganyifu wa picha ingawa taarifa inaweza kuwa ya kweli.

kweli mkuu...hizi machine tofauti....iliokatwa na kabla haijakatwa zina tofauti kubwa sana....
 
Kwa mara nyingine, maafisa wa Hong Kong katika kiwanja cha ndege wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya zilizokuwa zinasafirishwa kutokea Tanzania safari hii zikiwa zimefichwa katikati ya chuma cha mashine.

Dawa hizo aina ya heroin zilikamatwa katika nyakati mbili tofauti kwa jumla zikiwa na kilo 1.5 na thamani ya dola milioni 1.3 za Marekani.

Maafisa hao wanasema kwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo za wauza dawa na mbinu za kuficha dawa hizo, walilazimika kukikata chuma cha mashine hiyo ili kuziona.

Adhabu ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni faini ya dola milioni 5 za Kimarekani.

Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Serikali ya nchi hiyo na picha zinazoambatana na taarifa hiyo vimepachikwa hapo chini.

6366947_orig.jpg


8940017_orig.jpg


8668822_orig.jpg

haya maajabu kama sio suicide attempt
1.tarehe 2 august walikamata gram 700.......ndani ya metal gear
2.tarehe 15 wakakamata tena gram 800 ndani ya metal gear....hivi kweli mmoja anakamatwa tarehe 2 halafu tarehe 15 mwingine anaenda na metal gear hio hio from tz to china......
 
Mkuu nitajaribu kukueleza kwa kadiri nilivyoelewa:

1. Picha ya kwanza na ya pili ni picha mbili tofauti zioneshazo matukio mawili tofauti ya ukataji chuma.

2. Chuma kinachoandaliwa kukatwa katika picha ya kwanza ni tofauti na kile kilichokwishakatwa katika picha ya pili.(kulikuwa na vyuma viwili tofauti vilivyoshindiliwa dawa).
Jaribu kuvichunguza kwa makini utagundua havifanani.

3. Ukisoma kwa makini yale maelezo yaliyopo katika picha yenye maelezo utaona wamebainisha wazi kabisa utofauti wa tarehe baina ya tukio la kwanza na lile la pili. Ufanano wa matukio hayo mawili upp sehemu moja tu, njia iliyotumika kuyaficha madawa hayo inafanana.

4. Hivyo basi kutokana na maelezo namba 1, 2 na 3, ni wazi utagundua kuwa hakuna udanganyifu wowote kwani hayo ni matukio mawili tofauti. Kwa mantiki hiyo hata mashine za ukataji kuna uwezekano zikawa zaidi ya moja.

Poa nimekupata mkuu.
 
Wewe ulitaka afanye nini?
ni kheriii akae kimya maana wanaishiaga kusema tu lakini hawatendi....they talk a talk and never walk a talk....hata mwakyembe sijui anapigaporojo za nini?? Kazi yako itasikika au onekana kwa matendo tu na kukesha na waandishi wa habari......
 
Uktaka mzgo wako wa unga ufke salama tanya hiv; vunja mfupa wa paja ondoa uroto then tumbukza madawa yako ungansha nyama,hapo mzgo utakuwa tayar kwa kusafrshwa bila kushtukiwa
 
Mtu anataka alale maskini amke tajiri haya ndiyo madhara yake.

Duh ila ni aibu na Tanganyika sasa dunia inaijua kwa biashara ya madawa ya kulevya. tutakaguliwa mpk basi, Tamaa hi ya utajiri wa haraka inaliangamiza taifa
 
Tanzania sasa haina tofauti na columbia!!!

Ooooh! afadhali ya Columbia marehemu Pablo Escobar alirudisha sehemu ya utajiri wake kwa masikini wa huko kwa kuwajengea nyumba za kuishi.Tafiti mateja wote wa bongo wana hali gani?wanatoka udenda tu hawana pa kulala wenye bahati kama.Ray C hatujui pengine Ritz-1 aliingilia kati.
 
haya maajabu kama sio suicide attempt
1.tarehe 2 august walikamata gram 700.......ndani ya metal gear
2.tarehe 15 wakakamata tena gram 800 ndani ya metal gear....hivi kweli mmoja anakamatwa tarehe 2 halafu tarehe 15 mwingine anaenda na metal gear hio hio from tz to china......

Hii filamu ni ndefu sana haiwezi kwisha mpaka stearing wake ambaye ni JK aamue kuimaliza,wana JF hebu nikumbusheni aliyekuwa rais wa Panama Bw.Noriega yuko wapi siku hizi!
 
By KIHEGA, wana JF hebu nikumbusheni aliyekuwa rais wa Panama Bw.Noriega yuko wapi siku hizi!
  • March 18, 2013 Paris, France. By Henry Samuel, Paris
    2:19PM GMT 18 Mar 2013

    The body of Olivier Metzner, who defended Noriega against money laundering charges in France, was found on Sunday floating off a Breton island he owned.

    Other celebrity clients of 63-year-old star of the French bar included the "rogue trader" Jérôme Kerviel and Continental Airlines, accused of causing the catastrophic Concorde crash in 2000.

    In other high-profile cases, he represented the former prime minister Dominique de Villepin in the Clearstream scandal, rock star Bertrand Cantat in the murder trial of his actress girlfriend, and Françoise Bettencourt-Meyers, the daughter of the L'Oréal heiress Liliane Bettencourt, in her bid to have her mother declared a ward of court.

    In a note sent by his eldest daughter, Noriega said he was "surprised" and "deeply hurt" to learn of Mr Metzner's death.

    He also categorically rejected suggestions of suicide, saying the act was "incompatible with (Metzner's) personality." Source: Manuel Noriega questions 'suicide' of French lawyer Olivier Metzner - Telegraph
    Manuel Noriega returns to Panama to serve 20 year jail term

    Manuel Noriega, the drug-running former Panamanian dictator, has been returned home from France to serve 20 years in jail for the murder of political opponents during his bloody rule in the 1980s.
 
Uvivu ndo umetuzidi,
sie tunaolima mnatuona kama tumechangayikiwa
nyie mwataka za haraka,
haya tutaona chama hapa je.
Mamndenyi
Hivi hao jamaa wanaokamatwa huko HK ni wanachama wa CCM? Naona makamanda wanawaka sana bila sababu ya msingi; hili ni tatizo la kitaifa raia wote wanatakiwa kuwa macho kama wakati ule wa sungusungu majambazi yalikimbia mijini na kutokemea hao jamaa wanaokamatwa hata wakinyongwa kwangu ni poa tu tumechoka na hizi adha wanazotuletea!
 
Last edited by a moderator:
CHAMA ni kweli kwamba co vijana wa CCM.Na ni kweli kuwa ni janga la kitaifa.CCM katika hili ndio Chama ambacho kimekua nyuma kukemea hii biashara,Watu wote wanalaani lkn Mwenyekiti wa CCM ana majina ya wauza unga,Binafsi co kwamba naichukia CCM kama Chama NO... Ila kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.makamanda ni sehemu ya Watanzania hawawezi kulinyamazia.kwa ufupi ni kwamba lawama zinakwenda CCM sababu ndio chama kinacho tawala kwa sasa.
 
Nadhani sasa bei za viwanja zitapungua,na zile nyumba za bilioni zitakosa wateja.hawa jamaa walifanya watu washindwe kununua vitu kwa ajili ya jinsi walivyokuwa wana-inflate bei na fedha zao haramu.

ndio yale yale ya Binti mdogo mwenye mshahara usiozidi milioni kukaa kwenye nyumba ya kupanga ya $1000.monkey economics.

am just thinking positively.maana hawa wapuuzi wameshatuhharibia vya kutosha sie tusiotulia kwenye nchi zetu kwa safari.
 
Khaa!! Ndiyo matokeo yake haya. Nyie mali zote za nchi zinaliwa kwenye siasa. mtu analipwa zaidi ya 10m tena zisizo na makato ya kodi kisa anajua kudanganyadanganya majukwaani. mwalimu ameachwa anakufa njaa. Mkulima ametelekezwa hata hiyo ruzuku kiduchu inayosemwa kumfikia ni bahati huku ruzuku nzito ikimwagwa kwenye vyama vya siasa ambavyo havizalishi chochote zaidi ya kuwapotezea watu muda wa kufanya kazi za uzalishaji kwa kushiriki katika mikutano iliyojaa uongouongo na mambo ya kufikirika. Biashara zote zinamilikiwa na wanasiasa au marafiki zao ambao hujiona kama miungu watu huku wakitunyanyasa kwa kutulipa kidogo na tunakosa sehemu ya kulilia kwa sababu ya unyonge wetu na wao ni waheshimiwa. Tukijaribu kufanya biashara ndogondogo basi mnatuwekea mizengwe kupitia vyombo vyenu ili tushindwe na biashara zenu kubwa zinawiri. Pesa mmefanya ndiyo kitambulisho cha ubinadamu. Kuna gap kubwa sana ya kipato katika nchi yetu. Wanyonge tunakufa huku tunajiona. Kila mmoja anataka kuvuka hili gap ili awe upande wa juu. Sasa atafanyaje ili avuke katika haya mazingira haya uliyomuwekea?.....it's one way only ....the only way...Get rich or Die trying :bored:
 
Back
Top Bottom