Abiria wahimizwa kutoa taarifa za makosa wanayofanya madereva barabarani

Abiria wahimizwa kutoa taarifa za makosa wanayofanya madereva barabarani

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
191
Reaction score
250
Afisa Mnadhimi wa kikosi cha Polisi, Trafiki Makao Makuu ACP Desdery Rugimbana, alisimamia zoezi la utoaji wa elimu ya usalama barabarani kwa watumiaji wote wa barabara wakiwemo madaereva na abiria.

Elimu hii ilitolewa oktoba Oktoba 18, 2026 eneo la Kipalala Morning Tabora. ACP Rugimbana alieleza lengo la utoaji wa elimu hii ni kuwaongezea uelewa wa pamoja kwa watumiaji wote wanaotumia barabara ili kupunguza ajali zinazopelekea Vifo na majeruhi.

Aidha, aliwataka madereva wote nchini kutii alama, michoro na ishara za askari wa polisi wanapokuwa barabarani. Pia, aliwataka abiria kujenga mahusiano mazuri na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za madereva wanaovunja sheria wanapoendesha magari yao barabarani ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi ya madereva wanaofanya makosa wawapo barabarani.
 
Back
Top Bottom