Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
ABIRIA WANAOPANDA BODABODA WASIO NA LESENI NAO WATOZWE FAINI. KABLA HUJAPANDA BODABODA, ULIZA LESENI KWANZA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Leseni ni kama kadi tuu.
Inaweza kuwa softcopy kwa wenye simu kubwa, au hardcopy kwa wasio na simu. Sio mzigo mkubwa.
Haya mambo mtu anajifunza boda leo kesho yupo road ni hatari sana.
Jana nimetoka zangu Sinza, nafika ITV pale yule boda akaikwaruza pikipiki nyingine ambayo ilikuwa na mjeshi. Ilikuwa bahati mbaya. Kwa hofu, yule boda aliyenipakiza akatimua
Mbio. Mimi nikamwambia wewe simama hakuna kitakachoharibika.
Kijana haelewi. Anasema nitulie mimi siwajui hao vizuri. Anasema anataka awanyooshe kidogo.
Heee! Uwanyooshe ukiwa umenipakiza nyuma?
Aiseeh! Aiseeh! Nyie! Nyie! Yule dogo Mungu amlaani. Tulitoka pale nduki gari zikiwa bado kwenye foleni.
Dogo anaropoka akiwa hajatulia, anageuka nyuma mara mbele. Anawaambia mnataka eeh mnataka eeh twendeni, sasa yule Mjeshi naye sijui ili kufuta aibu naye akawa anaongeza kasi kutufukuzia.
Tumefika pale Mwenge Mataa, kumbuka upande wetu umepigwa stop gari hacienda. Gari zinatokea Bunju ndio zimeruhusiwa.
Jamani! Jamani jamani! Mbona nilihisi tumbo kuchafuka.
Tumekoswa koswa pale na gari moja hivi hata silikumbuki. Tumechukua barabara ya Ubungo sasa. Yule mjeshi naye yumo.
Ikabidi nijishikilie.
Haohao! Hao! Hao! Huku nyuma namwambia unafanya nini wewe! Nishushe! Dogo kama Amevuta Sigara kali.
Kwa ule mwendo kumzuia na kumsumbua nilikuwa nahatarisha zaidi usalama wangu. Sasa nilianza kuona jinsi nitakavyopata ajali, national nikifariki zangu, jamani jamani! Kama sitakufa nitakatika sijui miguu au mikono, au nitakuwaje.
Tumefika round about ya Mlimani City pale napo kunakuwaga na kifoleni hivi, pale tukakoswa koswa tena, mbele kidogo ilibaki kidogo tugonge mmama mmoja hivi.
Sasa nikasema hapa nikubali tuu leo ni aidha nakufa au napata kilema. Daaah! Nakufa bila kuaga aiseeh! Naiwaza familia yangu. Jamani jamani! Huyu boda huyu.
Haohao! Tumevuka pale kivulini kama kishada.
Tunafika Ubungo flyover hapo ndipo nikajua aliyenipakiza hakuwa mtu. Hata yule mjeshi alituvulia kofia.
Upande wetu ulikuwa haujaruhusiwa. Lakini boda aliingia hivyohivyo. Nikabaki kuwa napiga kelele, aahaa! Hapaaaaana! Huku nimefumba macho, aloooh! Aloooh! Aloooh! Nyie! Yule dogo hakuwa binadamu na kama nisingekuwa na nguvu za Miungu jana mngesikia taarifa Mtibeli amekufa kwa ajali.
Tilapia pale. Bado tukiwa haihai. Sasa nikamwambia mjeshi ameshatuacha, akasema tulia nimwonyeshe, tukafika Kimara pale, akasimama.
Lililivyo lijinga bila aibu linanidai hela. Nikamwambia twende nikakupe hela.
Nikachukua vijana wangu wawili. Tulimbonda yule kijana, tukamnyanganya na Hela zake. Hakuwa na hela nyingi ni kama elfu themanini hivi.
Mshikaji wangu akaondoka na simu yake. Nikamwambia nenda polisi akashtaki kwamba kuna vibaka wamemfanyia uhalifu.
Dogo kaondoka kasema atanionyesha kazi. Nikamwambia tayari alishanionyesha na alichonifanyia ni mateso ya kisaikolojia ambayo ni zaidi ya nilivyomfanyia.
Aiseeh! Hawa vijana wawe na Leseni. Hata kama kwa mwaka ni 50k na wasio na leseni faini, na abiria atakayepanda bodaboda isiyo na leseni apewe faini.
Kwa sababu mbona ajali ikitokea inawakuta wote wawili bila kuangalia nani dereva nani abiria.
Wewe Abiria kazi yako ni kuuliza dereva bodaboda, unaleseni, nionyeshe leseni, kisha unapanda. Hivyo tuu.
Mimi nimemaliza
Leo zingesoma RIP Mtibeli. Na ingekuwa imeishia hapo.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam