Abiria wanene walipe nauli kubwa zaidi

Abiria wanene walipe nauli kubwa zaidi

Under-cover

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2023
Posts
1,834
Reaction score
3,042
1740305619584.jpg

Kampuni za ndege huenda hivi karibuni zikaanza kuwalipisha kiwango kikubwa cha pesa cha bei ya tiketi abiria wanene wenye uzito mkubwa ukilinganisha na ile watakayolipa Watu wenye uzito mdogo hii ikiwa ni sehemu ya maboresho yanayochangiwa na mambo mbalimbali ikiwemo kilichoelezwa kitaalamu kuwa itasaidia kupunguza gharama za mafuta, FOX News wameripoti.

Fox News imesema mwaka 2008 Mashirika ya ndege ya Marekani yalikuwa ya kwanza kuanza kulipisha pesa kwa mabegi ya mizigo (checked bags) wakianzia na USD 15 na baadaye Mashirika mengine ya ndege yakaiga na gharama ikaendelea kupanda, sasa mjadala mpya ni kuhusu abiria waanze kutozwa fedha kutokana na uzito wao ili kupunguza ulaji wa mafuta na kupunguza hewa chafu ili kutunza mazingira.

Mwaka 2013 kampuni ya ndege ya Samoa Air ilianzisha 'kodi ya unene' na ikawataka abiria kulipia tiketi kulingana na uzito wao lakini haikufanikiwa na wengi waliikataa lakini sasa kampuni kadhaa za ndege ikiwemo Finnair wameanzisha utaratibu wa kuwataka abiria kupima uzito kwa hiyari wakiwa na mizigo yao wafikapo Helsinki Airport ikiwa ni sehemu ya ukusanyaji data kwa miezi mitatu, utafiti ambao utakuja na majibu yatakayoamua kama Watu wanene walipie zaidi ama laah!.

Utafiti wa hivi karibuni kuhusu kama ni sawa kuwatoza Watu wanene pesa zaidi wakitaka kusafiri kwa ndege uliwahoji Wamarekani 1012 ambapo majibu yameonesha kuwa Watu wembamba na wasio na uzito mkubwa wamesema ni sawa tu Watu Watu wanene walipishwe zaidi huku Watu wanene wakitaka utaratibu ubaki kama kawaida na abiria wote walipe sawa, kwa upande wa Vijana wadogo na abiria wanaosafiri mara kwa mara kwenye ndege wameonekana kuunga mkono zaidi utaratibu wa abiria Wanene kulipishwa pesa nyingi zaidi.
 
Ukiwaambia wanajibu kwani we ulikatazwa kunenepa?
 
Huko ni kwanyanyapaa tu, wawaongezee size za siti ili wakae kwa raha.
 
Kwamba watu wanene wanasababisha mafuta kutumika mengi kwenye vyombo vya moto??
😅😅😅 ama kweli unene ni tusi sasa
 
Ni sahihi kabisa! Kusafirisha kgs50 ni tofauti na kusafirisha kgs 120.
Serikali iwe serious na hili jambo
 
Back
Top Bottom