polisi walianza na huyu==>>>
MWANDISHI wa safu ya
Kalamu ya Mwigamba (36)
inayochapishwa kila
Jumatano na gazeti la
Tanzania Daima, Samson
Mwigamba (36), jana alifikishwa katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es
Salaam, kwa kosa la
kuwashawishi askari na
maofisa wa majeshi ya hapa
nchini kuacha kuitii serikali iliyopo madarakani kwa sasa.
Mwigamba ambaye ni
Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) Mkoa wa Arusha
alifikishwa mahakamani hapo
jana saa tatu asubuhi chini ya ulinzi mkali wa makachero wa
Jeshi la Polisi na kisha
kuifadhiwa katika mahabusu
ya mahakama hiyo, kabla ya
kupandishwa kizimbani na
kusomewa shitaka hilo la jinai namba 289, la mwaka huu. Mbele ya Hakimu Mkazi,
Waliarwande Lema, Wakili
Mwandamizi wa Serikali
Elizabeth Kaganda, alidai
mshitakiwa huyo anakabiliwa
na kosa la kuwashawishi askari na maofisa wa Jeshi la
Polisi, Magereza na Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) kutoendelea
kuitii serikali iliyopo
madarakani kwa sasa ambayo inaongozwa na Rais Jakaya
Kikwete, kinyume na kifungu
cha 46(b),55(10(a) na 35 cha
Sheria ya Kanuni ya Adhabu
kama ilivyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002. Wakili Kaganda alidai
Novemba 30 mwaka huu,
gazeti la Tanzania Daima la
siku hiyo toleo Na. 2553
lilichapisha waraka uliokuwa
na kichwa cha habari kisemacho Waraka Maalumu
kwa askari wote ambao
uliandikwa na mshitakiwa
huyo kupitia safu yake
ijulikanayo kwa jina la
Kalamu ya Mwigamba.
Hata hivyo mshitakiwa huyo
ambaye alikuwa amevalia
magwanda ya chama hicho
alikana kosa hilo na wakili
Kaganda alidai upande wa
Jamhuri hauna pingamizi la mshitakiwa kupewa dhamana
kwasababu kosa linalomkabili
lina dhamana kwa mujibu wa
sheria na kuongeza kuwa
upelelezi wa kesi hiyo bado
haujakamilika. Kwa upande wake, Hakimu
Waliarwande Lema alikubali
mshitakiwa apate dhamana
kwa sharti la kuwa na
wadhamini wawili wa
kuaminika ambao kila mmoja atatakiwa asaini bondi ya sh
5,000,000, na kati yao
awasilishe hati ya mali
isiyoamishika yenye thamani
ya sh 5,000,000. Hakimu Lema alisema sharti
jingine ni kwamba
mshitakiwa huyo atatakiwa
kila mwisho wa mwezi aripoti
katika kituo Kikuu cha Polisi
na asalimishe hati yake ya kusafiria mahakamani hapo. Hata hivyo, Wakili wa
mshitakiwa Edson Mbogoro
alieleza kuwa wapo
wadhamini wawili ambao ni
madiwani wa wilaya ya Ilala
ambao wamekuja na barua zinazowatambulisha,
isipokuwa hawakuwa na hati
ya mali isiyohamishika na
kuiomba mahakama impatie
dhamana mteja wake.
Hakimu alikataa ombi hilo na
kuamuru mshitakiwa
apelekwe gerezani hadi
Desemba 20 mwaka huu, kesi
itakapokuja kwa ajili ya
kutajwa. Hii ni mara ya pili kwa serikali
kumfungulia kesi ya jinai
Mwigamba tangu mwaka huu
ulipoanza. Mwigamba pia ni miongoni
mwa viongozi na wanachama
wengine wa CHADEMA
wanaokabiliwa na kesi ya
mkusanyiko na maandamano
haramu ya Januari 5, mwaka huu, katika Jiji la Arusha na
kesi hiyo ipo katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Arusha na
imefikia hatua ya kuanza
kusikilizwa.