figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Mhariri Mkuu wa Kampuni ya New Habari, ambao ni wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Bingwa na Dimba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ndugu, Absalom Kibanda, amemtupia kombora mgombea Urais wa CCM. Kumbuka Kampuni ya New Habari, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) ni Hussein Bashe ambaye ni Msemaji wa Mgombea urais wa JMT Edward Lowassa.
Hapa nashindwa kuelewa Mhusika ni nani. Sababu siwezi kusema ni Membe sababu Membe alishatoa tamko kukana Kumdhuru Kipanda. Pitia hii thread Membe atoa tamko juu ya kutekwa kwa Kibanda na Waziri Membe akanusha kuhusika tukio la kumdhuru Mhariri Kibanda.
Kumbuka Bashe hawaivi chungu kimoja na Nape Nnauye. Na Nape Nnauye kaachiwa Jimbo la Mtama na Benard Membe. rejea hii Thread Bashe ajibu mashambulizi ya Nape Nnauye.
Akiandika katika ukurasa wake wa twitter kuhusiana na siku yake ya kuzaliwa, amesema, "Huu ni Mwaka ambao, Mgombea mmoja ambaye ni Mtangaza nia hakutamani niuone, Nimemsamehe!" Najiuliza huyo mtangaza nia ambaye hamtakii Mema Kibanda ni yupi?
Absalom Kibanda mwaka 2013, alivamiwa na watu wasiojulikana akiwa ndani ya gari lake wakati akiingia nyumbani kwake huko Mbezi-Beach, jijini Dar es Salaam majira ya saa sita usiku, akatekwa, kupigwa na kujeruhiwa ikiwa na kutobolewa jicho moja.