Kwanza kibanda hapaswi kujiita mwenyekiti wa jukwaa la wahariri, anatakiwa kujiita kibaraka wa lowassa. Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri hawezi kusimama getini na kuchagua waandishi wa habari wa kwenda kuzungumza na lowasa. NI hivi, wakati waandishi na wahariri walipokuwa dodoma kuzungumza na lowasa, huyu bwana alisimama mlangoni na kuanza kuchambua wa kuingia na wa kutoingia kutokana na vyombo vya habari ambavyo wanavipenda. kwa maana hiyo, kujiita mwenyekiti wa jukwaa ni kudhalilisha taaluma ya habari.mwenyekiti gani asiyeweza kutetea waandishi wake na badala yake kuwa kiungo cha ubaguzi kwa sababu tu ya kulamba watu kisiasa? kuna sababu gani za kulilia sheria ya kutambua uhuru wa habari wakati wanaotakiwa kuutumikia uhuru huo wakibagua waandishi wao wenyewe?
pia, tukio la kuteswa kwake, tunawezaje kushindwa kusema pengine alibeba mke wa mtu na jamaa alilipiza kisasi kuliko anavyokimbilia kutuaminisha kwamba kuna mgombea ambaye alitaka kukatisha maisha yake? kwa nini kama ana ushahidi huo asiende kwenye vyombo vya sheria? nachukia sana watu wanajivika ngozi za kondoo kwa umma wakati ni mbwa mwitu tu.