Absalom Kibanda (Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri) avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa

Polisi waanze uchunguzi na gazeti la Tanzania Daima na Chadema. kwani hatuelewi ni kwanini alikimbia huko alipokuwa mhariri wa hilo gazeti la mwenyekiti wa chama.

.....

Waanzie kwako, yaelekea una fununu juu ya unyama huu.Vipi Abedi aka Igondhu hajambo?
 
Nilielewa tu hauwezi kunielewa kwa hizo akili zako za pale ''Lumumba''. Hata hivyo nashukuru wenye fikra huru wamenisoma.
Sikushangaa kama nitapata jibu kama hili kwa sababu ujumbe wako ulikuwa unaashilia jinsi kina chako cha uelewa wa mambo yanayohitaji pembuzi pevu kilivyo kidogo.

Kwa kudhihirisha zaidi, bandiko lako hili linachagiza kile ninachokisema kwa vile katika fikra zako hizi fupi, mtu yeyote anayefikiria tofauti kimawazo na hekima zako finyu kwako anatoka Lumumba.
 

Nakubaliana na wewe lazima kuna jambo hapo, haiwezekani awe mhariri aliyekua akifanyia kazi gazeti lilikua mstari wa mbele kukemea ufisadi na hata kutaja mafisadi halafu huyo huyo tena aende kuajiriwa na fisadi, lazima kuna jambo, nakubaliana na wewe kabisa.
 
Kwa sasa kila uhalifu tuliokuwa tukiusikia tu kwa wenzetu au kuangalia mifano yake kweny Movie unafanyika hapa Tanzania- Mauaji ya Albino tunaongoza, Kuingiza na kusambaza madawa ya kulevya tunaongoza, Utekaji na utesaji tunaongoza pia na unyanyasaji kwa kuwafunga Baba na watoto wake jela maisha kwa kubaka na kulawiti mtoto wa Miaka 7 bila kupata maumivu na wazazi kuwachukua muda mrefu kulitambua hilo.
 
hivi unaweza kuwa mwanahabari wa new habari corporation halafu ukawa na uhasama na serikali ya ccm?
 
Msema kweli na yeyote anayeikosoa serikali ya ccm kwanini atekwe na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi? Mbaya zaidi hao majambazi huwa hawakamatwi lakini RPC Mwanza alipouawa wahusika walikamatwa ndani ya wiki moja. Sawa labda kweli ni majambazi kusudi lao nini? Nani kawatuma na kwanini? Mbona hawakamatwi na utawala ulipo madarakani? Pengine wana uhusiano ndiyo maana hawawagusi?
 
Haya mambo yanatokea wazi wazi halafu yule muingereza akiwaandika kwenye vyombo vya habari, eti mnaandaa maandano ya kwenda Ubalozi wa Uingereza. eti mmedhalilishwa. shwaaaaiini kabisa.
 
Mkuu Ng'wamapalala huko sawa kabisa hao sio malaika, ili kuondoa kutokuaminiana kati ya wafanya uchunguzi na wasubiri matokeo naomba iundwe tume.(hapa kidogo tutaamini maana tume inaundwa na MITUME hawa jamaa wako karibu na Malaika) ili kubaini kwanini chunguzi nyingi zinaleta majibu yasiyoaminika/kubalika na walio wengi.
 
Last edited by a moderator:
Ukitaka kuishi kwa amani tanzania nilazima uwe mtu wa kupundisha ukweli na kuubadilisha kuwa uongo. by the way you cat off
 

Mkuu Ng'wamapalala huko sawa kabisa hao sio malaika, ili kuondoa kutokuaminiana kati ya wafanya uchunguzi na wasubiri matokeo naomba iundwe tume.(hapa kidogo tutaamini maana tume inaundwa na MITUME hawa jamaa wako karibu na Malaika) ili kubaini kwanini chunguzi nyingi zinaleta majibu yasiyoaminika/kubalika na walio wengi.

Get Well Soon A. Kibanda.
 
Hili si jambo jema hata kidogo,iwe ametekwa kwa sababu binafsi kati yake na mtu mwingine,au iwe ametekwa na kupigwa kwa sababu ya kazi yake bado nasema kitendo hiki hakikubaliki,lakini tatizo kubwa ninaloliona hapa ni wale wenzangu mimi tunaotofautiana kiitikadi,sisi wa upande mwingine hasa CDM tunaapokosoa utendaji kazi wa serikali hii ya CCM watu wengine wanakuja na hoja za kupinga na kusifia kuwa ni serikali sikivu na inayojali watu,na mbaya zaidi hata sisi wananchi tumeridhika na maisha haya,tumekubali kusubiri zamu zetu za kutekwa na kupigwa hadi kufa au kusalimika kama alivyobahatika Dr Ulimboka,maana kama tungelikuwa tunakataa kwa vitendo ndani na nje hakika hata wanaohusika kulinda usalama wa raia na mali zao wangekuwa wanafanya kazi zao ipasavyo,lakini leo hii tunakataa ndani tu nikimaanisha kupitia mtandao,kwenye laptop na simu,tunaandika sana baada ya siku mbili tatu tunasahau na kudandia jambo jingine.hapa kinachotakiwa ni kukataa kwa vitendo,ni kupinga kwa vitendo,tunapaswa kupaza sauti zetu kwa nguvu mchana na usiku tukipinga vitendo hivi vya kutekwa na watekaji kutojulikana na wala sababu ya kutekwa kwao,sasa tumebaki kusubiri zamu zetu za kutekwa na wote tulioko humu kwenye JF,Twitter,FB na mitandao mingine ni wajanja wa kuandika tu,na imekuwa kama fasion tu,iweje matukio ya kutekwa yanaendelea lakini hatujawahi kusikia watekaji wamekamatwa na sababu za kufanya unyama huo zikabainishwa?hivi hili sio genge la kihalifu kweli,maana baada ya kutekwa Dr Ulimboka nakumbuka kuna mama nae alitekwa na akauwawa huko kwenye msitu wa mabwepande na gari yake ilichomwa moto,nadhani matukio haya yaliendelea tena nadhani mtakumbuka,mwanasheria wa baraza la mazingira nae yalimkuta,nani yule wa bakwata Arusha,mapadri kule ZNZ yote haya ni matukio yanayotudhihirishia kuwa hakuna usalama wa raia wala hakuna Intelijensia isipokuwa pale CDM wanapotaka kufanya mikutano au maandamano ndipo utawasikia hao Intelijensia.
Wandugu,natoa wito kwamba,sasa tukataeni hali hii ya utekwaji kwa vitendo,ndani na njetupazeni sauti zetu kwa maandamano ya amani na tushinikize wahusika wajihuzuru kwani wizara hii imewashinda,Nchimbi aondoke na Mwema nae aondoke,Kova aende na wengine wote wanashughulika na usalama wa raia na mali zao,maana hakuna hata mtekaji mmoja aliewahi kukamatwa na akafikishwa mbele ya sheria.hata kama watekaji hawa ni serikali yenyewe basi tuikataeni,maana ni unyama unaoweza kumpata kila mtu pale ambapo wakijisikia kufanya hivyo.
Mungu na akujalie upone haraka Kibanda.
 
Haya yote ni matokeo ya kuacha kutumia taaluma yetu ya uandishi wa habari inavyotakiwa na badala yake mnaandika ushabiki wa kisiasa!!! Kuna mafia ambao lengo lao si jema hata kidogo!! Imagine leo hii umeandika sanaa wee kuhusu mafisadi kama ambavyo alifanya kupitia Tanzania Daima!! Halafu uniambie eti leo hii Habari Corporation ambayo mmiliki ni miongoni mwa wale mafisadi eti anakupenda na anataka kukuajiri!!! Ili ufanye kazi gani? Mbaya wako ukitaka kummaliza vizuri mlete karibu!!! Na wengi wetu tukichekewa kidogo na hela nyingi juu basi tunajisahau!! Thubutu!! Mafisadi wote ni mafia!! Pole sana Kibanda!! Mungu asaidie upone!!
 
Chadema ni genge hatari sana,polisi angalieni kwa umakini sana kuna mkono wa Chadema hapo
 
our almighyt Lord will cure our hero!long live Kibanda!Prayers are with you!
 
Haya bwana kila anayempa ushauri au anayepingana na mawazo ya bwana mkubwa JK anashughulikiwa na kina Ahmad Msangi .Wafahamu ipo siku watageukiwa wao watalia kilio cha mbwa na kusaga meno. Hizi ni dalili za wazi za kushindwa kuongoza nafikiri tungekuwa na Mkuu wa majeshi mwelewa angeshaliona hilo na kuamua kuchukua nchi kwani sasa hatuna mwelekeo WALA SERIKALI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…