Polisi waanze uchunguzi na gazeti la tanzania daima na chadema. kwani hatuelewi ni kwanini alikimbia huko alipokuwa mhariri wa hilo gazeti la mwenyekiti wa chama.
Mengi yamesemwa kuhusiana na kupigwa hadi kujeruhiwa vibaya kwa Mhariri Kibanda. Swali ambalo wengi wanajiuliza ni chanzo cha tukio hilo la kinyama. Kwa wale wanaofuatilia mambo kwa karibu, kuna uwezekano mkubwa sana chanzo kuwa nafasi aliyopewa New Habari, hatua ambayo ilimfanya binadamu aitwaye Prince Bagenda kujikuta hana kazi. Kwa hiyo inawezekana kabisa Bagenda anafahamu kila kitu, na hata watesaji wa Kibanda si wahuni au majambazi, bali ni watu wa "system" kama alivyo Bagenda. Pia Bagenda kwa zaidi ya wiki inasemekana haonekani ofisini. Pia Bagenda baada ya kuvuliwa madaraka, wapashaji wanasema amewahi kutamba kuwa yeye ni trained soldier and a murderer as well. Tusipuuze hata kidogo dokezo hili. Mungu mponye Kibanda, ili arejee ulingoni.
Fikra fupi kama hizi ndizo zinazo sababisha serikali kufanya unyama itakavyo, tujikumbushe swaga la aliyekua Mbunge wa Tarime:-
Huyu bwana alikua na mgogoro na viongozi wenziye pale CHADEMA, wakati amesimamishwa uongozi kabla hata mwezi haujapita, Chacha Wangwe akakumbwa na umauti (kwa ajali ya gari) watu wengi walipiga sana kelele kwamba uchunguzi makini ufanyike lakini wapi, hakuna kilichofanyika, nadhani mzee mwanakijiji aliandika makala ndefu sana akionesha mashaka yake na kifo kile, lakini bado hakuna aliyetaka ufanyike uchunguzi.
Kumbuka mwenye amri ya kuleta wachunguzi independent ni serikali, hadi leo kimya, watu wenye akili finyu wakasema atakua Mbowe na CDM, sababu ikiwa ya kitoto sana, eti dereva alikua ni Mchaga kama mwenyekiti wa CDM, kesi ilifanyika, yule aliyekua dereva wake akawekwa ndani kwa miaka 3.
Kabla hajamaliza adhabu ile, rais aliyekua madarakani akamfungulia, utafiti binafsi ukaenda mbali zaidi ikaja julikana kwamba dogo yule amewahi kwenda Libya kwa mafunzo maalumu chini ya UVCCM.
Kwenye msiba, Mbowe alitahadhalishwa eti asiende kwani Wakulya wangemuua, wapi bwna, Mbowe alikwenda na akapokelewa na jamii ya watu wa pale kama kiongozi wa marehemu Mbunge wao, uchaguzi ulipo rudiwa wana Tarime walimchagua tena Mbunge toka CDM, hapo ndio ukawa mwanzo wa kitu inayoitwa leo, Opearation Sangara.
Napenda tu nikwambie mkuu serikali hii inaweza kufanya kitu ili tu asingiziwe mwingine, kwani issue ya Daud Mwangosi ilikuaje? si walisema CDM, picha sasa za mnato na za video ndio zikawaumbua, usiwe na akili fupi, ngoja uchunguzi makini ufanyike, you will see.[/SIZE]
Polisi ilishashindwa kuchunguza matukio ya hivyo, Waitwe FBI kuchunguza hilo, tena wapo hapo kisiwani tu.Polisi waanze uchunguzi na gazeti la tanzania daima na chadema. kwani hatuelewi ni kwanini alikimbia huko alipokuwa mhariri wa hilo gazeti la mwenyekiti wa chama.
Mkuu, hili ndiyo tatizo, nchi inapokuwa na taasisi kama polisi ambayo kwa undani ni kama crime syndicate kuna hatari hata ya kuchochea matukio ya uvunjifu wa sheria kuwa ni moja ya day to day work kwa kikundi cha watu wabaya huku watu wengine wakikosa hata imani na utendaji wake na matokeo yake pia ni watu kuanza kujichukulia sheria mikononi.Vyovyote iwavyo.Tatizo zinaundwa tume za (wasio huru) watumia Tumbo badala ya mitume (walio huru) watumia Vichwa. Hivyo huwa wanaenda kuzuga huku wakiwa na majibu toka kwa bosi wao anayewatuma huku wakiwazia POSHO badala ya wajibu wao.Ebu kuwa mwazi
1.Uchunguzi wa Kifo cha mwangosi ulisaidia nini au kuleta majibu gani kwa matatizo yaliyopo kwa wanahabari na wanasiasa?.
2.Uchunguzi wa kutekwa kwa Ulimboka ulieleza sababu ya kutekwa kwake?.
3.Kuvamiwa na Kumwagiwa tindikali S. Kubenea!.
4.Kupakwa sumu viongozi wetu waandamizi.
5.Kuuwawa kwa Barlow.
Kwa uchache tu, Pengine tungefanya vizuri katika chunguzi za hayo matukio tungeweza kuzuia matukio mengine yasitokee.Ndugu Ng'wamapalala polisi wetu wanatuumiwa Kariakoo milioni 150,000,000/=, Lunzewe milioni 300,000,000/=. matukio yote wakitumia silaa na mipango ya siri kubwa.
Kwanini wasiweze kumteka mtu atakayeonekana kuwatafiti katika mambo yao?.
In English they say; Insanity is keep doing the same thing in a same way expecting different results!.Are we all INSANE?. Nooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo!.
..hata mie nimeshangaa kuona anataja mtu..ila huwezi jua mtoa hoja ni nani..?Mkuu una ushahidi ambao unamweka mtu uliyemtaja au umeamua kumtaja tuu
Maana ni bora usingetaja jina la mhusika ila wewe umejiaminisha kabisa kumtaja na jina
Naam na kabla ya sheria mkononi inaanza minung'uniko na hukumu binafsi, ambazo unaziona humu jamvini. Cha ajabu tunabishana badala ya kuona ukweli na kuwalazimiza wale woote wanaosababisha hali hii. Tunawaona tunawafahamu lakini tuko vilevile kila siku.Mkuu, hili ndiyo tatizo, nchi inapokuwa na taasisi kama polisi ambayo kwa undani ni kama crime syndicate kuna hatari hata ya kuchochea matukio ya uvunjifu wa sheria kuwa ni moja ya day to day work kwa kikundi cha watu wabaya huku watu wengine wakikosa hata imani na utendaji wake na matokeo yake pia ni watu kuanza kujichukulia sheria mikononi.
nimeona hivi tu nimekumbuka DR. Ulimboka. Tanzania imefika hapa ilipo? its hard to believe!!!Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari, Abdalom Kibanda, amekimbizwa Muhimbili baada ya kuvamiwa na kisha kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi.
Watu hao walimvamia na kumtoa katika gari kisha wakampiga kabla ya kumtupa na kumtelekeza umbali mdogo na nyumbani kwake.
Aliokotwa na majirani na kukimbizwa hospitalini Muhimbili kwa matibabu ya haraka.
Pamoja na kuumizwa hivyo, hakuna kitu hata kimoja kilichoporwa katika gari lake
Taarifa zaidi baadae...
Kuna shemeji yangu anafanya MOI amesema jamaa yuko kwenye hali mbaya sana. Halafu nikikumbuka kuwa alizaliwa siku moja na Chavez, nashindwa kabisa kujizuia kusikitika.
Unamlazimisha Mungu?
FBI wakichunguza kila kitu kuna haja ya kuwa na kitengo cha intelligencia na Police force kwa ujumla? yaani kama imefikia hatua wananchi tumeanza kuhoji uwepo wa taasisi hizi basi ni Janga lingine hili.Polisi ilishashindwa kuchunguza matukio ya hivyo, Waitwe FBI kuchunguza hilo, tena wapo hapo kisiwani tu.
Hili ulipaswa ulielekeze kwa serikali yako sio kwangu maana Serikali imebuni mtindo mpya wa kusaidiwa na FBI kuchunguza masuala ambayo yapo ndani ya uwezo wa kawaida kabisa wa jeshi la polisi, so hata hili acha tu tuwapelekee FBI.FBI wakichunguza kila kitu kuna haja ya kuwa na kitengo cha intelligencia na Police force kwa ujumla? yaani kama imefikia hatua wananchi tumeanza kuhoji uwepo wa taasisi hizi basi ni Janga lingine hili.
Kama kawaida, kwa kupitia jf, be the first to know, kuwa hivi sasa, juhudi zinafanywa kumhamisha Kibanda kwenda nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi. Juhudi hizi zinaratibiwa na Jukwaa la Wahariri kwa ushirikiano wa karibu na baadhi ya wadau watakao gharimia safari hiyo!.
Japo ni kawaida kwa serikali kupeleka baadhi ya wagonjwa nje ya nchi, preference ya kwanza ya serikali ni kupeleka wagonjwa India kwa sababu its cheaper kuliko Afrika Kusini ambapo gharama ziko juu!.
Hili la Kibanda kupelekwa A. Kusini, linazidi kumshabihianisha Kibanda na Dr. Dr. Ulimboka, wote walivamiwa usiku na watu wasiojulikana, wote walifanyiwa jinai ya kudhuru mwili, wote walihudumiwa kwanza MOI, na baadae kupelekwa nchini Afrika Kusini, juhudi za kwanza ni kusafirishwa kwa michango ya wadau na baadae serikali ikatumbukiza mkono wake.
Mara ya mwisho kukaa na Kibanda ni mwezi Desemba, mara tuu baada ya kuhama Tanzania Daima, tulikutanishwa mahali na mwana jf Omar Ilyas, na miongoni kwa swali kubwa langu kwa Kibanda, nilidadisi ni kwa nini amehama Tanzania Daima kuelekea Mtanzania, alichonijibu nilibaki tuu kushangaa bila kumuamini. Kwa vile jibu lile lilikuwa off the record, lakini maadam haya yamentokea, naanza to connect the dots!.
Kwa sasa, tuendelee kwanza kumtakia uponyaji wa haraka na mengine yatafuatia!.
We keep on wishing him a speedy recovery and get well soon!.
Pasco
Ooh boy.. tunamuombea apone.. ni matumaini yangu kuwa hili halihusiani na kazi yake ya uandishi.
Mambo ya ulimboka yameanza Tena
Tunaelekea wapi...Why Absalom? Anayesimamia anachokiamini,mwanahabari ...Majambazi! Haiingii akilini..kuna dots za kuunganisha hapa..
Kwa nchi yetu ilivyo sasa hivi kuna uwezekano mkubwa kwamba sababu kubwa ya kutekwa kwake inahusiana na kazi zake. Tusubiri tufahamu sababu, lakini inaweza kabisa isijulikane. Mungu amponye haraka.
Tina , asante kwa taarifa,
Kibanda we wish you a speedy recovery and get well soon!.
Pasco.
Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Absalom Kibanda amevamiwa na watu wanaodaiwa ni majambazi akiwa anaingia nyumbani kwake. Amejeruhiwa vibaya ikiwa ni pamoja na kutobolewa jicho na sasa anatibiwa hospital ya Taifa Muhimbili (icu)
Wabaya wake wemetimiza dhamira yao
Kama uko duniani huwezi kosa mbaya, siyo jambo la kushangaza., kwani wabaya wake walikuwa akina nani?
Inawezekana ni sababu za kisiasa.
Haya mambo yanatokea sana system inapokuwa imefeli.hapa itaundwa tume! Waandishi mjifunze ili msimamie haki maana huwezi jua kesho ni nani!
Chama tawala kimefeli muda mrefu!
hivi unaweza kuwa mwanahabari wa new habari corporation halafu ukawa na uhasama na serikali ya ccm?
Ukitaka kuishi kwa amani tanzania nilazima uwe mtu wa kupundisha ukweli na kuubadilisha kuwa uongo. by the way you cat off
Hofu ya Al Qaeda Ukerewe
*Wananchi wakihusisha chuo na ugaidi
*Mbunge ataharuki, aandaa hoja binafsi
*Mkuu wa Mkoa, DC wakwepa kunena
HOFU ya kuwapo kwa magaidi wa mtandao wa Al- Qaeda, imetanda katika Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, baada ya kuvuja kwa taarifa za kuanzishwa kwa chuo kimoja cha kidini kinachohofiwa kutoa mafunzo yenye mwelekeo wa kigaidi visiwani humo.
Taarifa hizo zimeeleza kuwa chuo hicho kinajulikana kwa jina la Markaz, Aljazeera na kimeanzishwa kwa ufadhili wa raia wa kigeni ambao ni waumini wa dini ya Kiislamu.
Makundi yanayotajwa kufadhili uendeshaji wa chuo hicho ni Al-Qaeda na Al shabab yanayoaminika kuwa na mtandao mkubwa wa ugaidi duniani.
Uchunguzi uliofanywa na Mtanzania Jumatano wilayani Ukerewe, umebaini kuwa chuo cha Markaz kinatoa mafunzo kwa watu wa rika mbalimbali yenye mwelekeo wa kujihami na kushambulia kama Karate na Kung-fu.
Aidha, taarifa nyingine za kiuchunguzi ambazo gazeti hili lilidokezwa na wakazi wa kisiwani humo walioonyesha wasiwasi wa kuwepo kwa chuo hicho, zilidai kuwa, aina nyingine ya mafunzo yanayotolewa katika chuo hicho na kushambuliana kwa silaha aina ya jambia.
Uchunguzi ulibaini zaidi kuwa, wanafunzi katika chuo hicho ni watoto wenye umri wa kati ya miaka saba hadi 10 na pia kuna wanafunzi vijana na watu wazima.
Baadhi ya wakazi wa wilayani humo waliopata kufanya kazi katika chuo hicho, waliliambia gazeti hili kuwa chuo hicho kimekuwa kikipokea mizigo ya aina mbalimbali, ikiwa imefungwa kwenye maboksi ambayo katika udadisi wao walibaini kuwa, baadhi ya bidhaa zinazokuwa kwenye shehena hizo ni kanzu, seti za televisheni, vitabu na silaha za aina mbalimbali.
Walidai kuwa, walianza kukitilia mashaka chuo hicho baada ya kubaini kinapokea silaha katika baadhi ya mizigo yake.
Mbali ya hilo, wakazi hao walilieleza gazeti hili kwamba aina ya wageni wanaoingia na kutoka visiwani humo kwa minajili ya kukitembelea chuo hicho, ni jambo jingine ambalo limekuwa likiwafanya wazidi kukitilia shaka chuo hicho.
Kwa mujibu wa wakazi hao, wageni hao wamekuwa wakiingia kisiwani kwa njia ya mitumbwi wakipita katika njia za panya nyakati za usiku.
Wageni hao kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo la Nansio ni wale wanaodaiwa na kuaminika kutoka katika nchi jirani za Kenya na Uganda ambazo mipaka ya ziwa Victoria inapita.
Wafanyabiashara wanaojihusisha na usafirishaji abiria waliozungumza na gazeti la Mtanzania Jumatano walieleza kuwa, wageni wanaowapakia kuwapeleka chuo cha Markaz au maeneo mengine ya kisiwa hicho huwalazimisha kuondoa misalaba waliyoivaa shingoni au waliyotundika katika magari na pia huwataka wazime redio katika magari yao.
Hofu hiyo ya wakazi wa Nansio ilisababisha gazeti hili kumtafuta Mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemli (Chadema) ambaye naye alikiri kulifahamu jambo hilo.
Akizungumza kupitia simu yake ya kiganjani, Machemli alisema chuo hicho kinatoa mafunzo ambayo wakazi wake wanayahusisha na matendo ya kigaidi.
Mbunge huyo alisema hofu zaidi kuhusu chuo hicho ni kuwapo kwa taarifa zinazodai kwamba, baadhi ya wanachuo ambao wamewahi kupata mafunzo chuoni wanatajwa kuwa wanachama wa makundi ya kigaidi ya Al Qaeda na Al-Shabab.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, miongoni mwa hatua ambazo amepata kuzichukua ili kutafuta majibu ya wasiwasi wa wananchi wa Ukerewe ni pamoja na kumsaka mmoja wa watu anayekijua chuo hicho.
Ni kweli tuna wasiwasi na hatuoni kazi ya umma kinachojihusisha nacho. Niliwahi kumuuliza Diwani wa Kata ya Nansio, Sheikh Ramadhani Mazige (CCM) kuhusu uhalali wa kuwapo kwa chuo hicho kwa sababu alikuwa akisimamia ujenzi wake na nikashauri juu ya umuhimu wa kubadili aina ya mafunzo yanayofundishwa chuoni hapo na jibu lake lilikuwa wenye chuo hawataki.
Alipoulizwa iwapo anawafahamu wamiliki wa chuo hicho, alikana kuwatambua kwa kueleza kuwa, jitihada zake za kuwafahamu hazikufanikiwa baada ya Diwani Mazege kukataa kuwataja.
Machemli alisema kuwa, amepanga kulifikisha suala hilo kama hoja binafsi kwenye Baraza la Madiwani ili kuomba kibali cha kutembelea chuo hicho kuona shughuli zinazofanyika na kwamba iwapo atakwamishwa, atalifikisha suala hilo katika ngazi za juu.
Akizungumza kuhusu raia wa kigeni wanaopitia njia za panya kwa usafiri wa mitumbwi nyakati za usiku kufika chuoni hapo, Machemli alisema hilo hawezi kulipinga.
Kwa mujibu wa Machemli, jiografia ya visiwa vya Ukerewe inavifanya viwe wazi kuhusu mipaka yake na kwamba jambo hilo alipata kulizungumza bungeni ingawa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha alimpuuza.
Nilizungumza katika mkutano uliopita wa Bunge kuhusu mipaka ya Ukerewe kuwa wazi sana, nililalamika kwamba, wanajeshi wa Kenya na Uganda wanakuja hadi katika kisiwa hicho kufanya mazoezi yake na kuondoka, lakini nashangaa waziri akanipuuza, alilalamika Machemli.
Alipotafutwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu kwa ajili ya kuzungumzia juu ya hofu hiyo, alisema anaomba apewe muda kwa sababu yeye ni mgeni mkoani humo na huu mwezi wa pili akiwa katika kituo chake kipya cha kazi, hivyo yapo mengi ambayo hayafahamu.
Hata hivyo, Mangu aliliahidi gazeti hili kufuatilia juu ya suala hilo na kulitolea ufafanuzi baadaye.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mary Tesha alikana kufahamu chochote na badala yake akahoji sababu za mwandishi kumtafuta wakati tayari suala hilo lilisharipotiwa katika gazeti hili hivi karibuni.
Kumekuwa na tetesi za kuwepo kwa vikundi vinavyojihusisha na utoaji mafunzo ya kigaidi hapa nchini, vikiwa vimejificha katika mwamvuli huku lengo halisi likiwa kuhatarisha amani ya kitaifa.
Tayari Rais Jakaya Kikwete amekwishaagiza kusakwa kwa makundi yenye mwelekeo huo yanayohisiwa kuhusika na machufuko na mauaji hapa nchini, wakati akitoa salamu za pole baada ya tukio la kuuawa kinyama kwa Padre wa Kanisa Katoliki Evaritus Mushi huko visiwani Zanzibar.
CHANZO: Mtanzania | Feb 20, 2013
Salvatory Naruyaga: mbunge wa ukerewe kupitia chadema amekanusha vikali habari kupitia gazeti la mtanzania kwamba yeye aliongea na gazeti hilo kuhusu Taasisi ya Islamic Center kuhusika na Ugaidi.
Amesema yeye hajawahi na wala hajui kwanini gazeti hilo limeandika taarifa hiyo huku ikumnukuu yeye.
Amesema yeye kama Mbunge hajui wapi gazeti hilo limetoa taarifa hiyo na kudai pengine ni njama za gazeti hilo la kutaka kumgombanisha na jamii ya kiislam hapa nchini. amesema hakuna mwananchi wa eneo lake aliwahi kupeleka malalamiko hayo kwake.
SOURCE: Mahojiano ya mbunge huyo na REDIO IMAAN.
PIA TAASISI YA ALJAZIRA ISLAMIC CENTRE UKEREWE WATOA SIKU 7 KWA GAZETI LA MTANZANIA KUKANUSHA KWA MAANDISHI MAKUBWA TAARIFA ILIZOTOA LA SIVYO ITACHUKUA HATUA ZA KISHERIA.
yes tisha toto style ya uongozi - hata mzee ukiona huna hela mfukoni na weekend ndiyo inawadia cha kufanya ni kuwa mkali kwa kila jambo ili asijitokeze either ze-wife au watoto kuomba hela.Awamu ya nne ya utawala Tanzania imekuwa na style mpya kabisa ambayo haikupata kutokea huko nyuma.
Matukio haya wala sio ya kufanyia kebehi hata kidogo maana sasa kasi yake imepamba moto. Tusimame kwa umoja wetu na kuyakataa haya