Hofu ya Al Qaeda Ukerewe
JUMATANO, FEBRUARI 20, 2013 05:04 NA MWANDISHI WETU
*Wananchi wakihusisha chuo na ugaidi
*Mbunge ataharuki, aandaa hoja binafsi
*Mkuu wa Mkoa, DC wakwepa kunena
HOFU ya kuwapo kwa magaidi wa mtandao wa Al- Qaeda, imetanda katika Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, baada ya kuvuja kwa taarifa za kuanzishwa kwa chuo kimoja cha kidini kinachohofiwa kutoa mafunzo yenye mwelekeo wa kigaidi visiwani humo.
Taarifa hizo zimeeleza kuwa chuo hicho kinajulikana kwa jina la Markaz, Aljazeera na kimeanzishwa kwa ufadhili wa raia wa kigeni ambao ni waumini wa dini ya Kiislamu.
Makundi yanayotajwa kufadhili uendeshaji wa chuo hicho ni Al-Qaeda na Al shabab yanayoaminika kuwa na mtandao mkubwa wa ugaidi duniani.
Uchunguzi uliofanywa na Mtanzania Jumatano wilayani Ukerewe, umebaini kuwa chuo cha Markaz kinatoa mafunzo kwa watu wa rika mbalimbali yenye mwelekeo wa kujihami na kushambulia kama Karate na Kung-fu.
Aidha, taarifa nyingine za kiuchunguzi ambazo gazeti hili lilidokezwa na wakazi wa kisiwani humo walioonyesha wasiwasi wa kuwepo kwa chuo hicho, zilidai kuwa, aina nyingine ya mafunzo yanayotolewa katika chuo hicho na kushambuliana kwa silaha aina ya jambia.
Uchunguzi ulibaini zaidi kuwa, wanafunzi katika chuo hicho ni watoto wenye umri wa kati ya miaka saba hadi 10 na pia kuna wanafunzi vijana na watu wazima.
Baadhi ya wakazi wa wilayani humo waliopata kufanya kazi katika chuo hicho, waliliambia gazeti hili kuwa chuo hicho kimekuwa kikipokea mizigo ya aina mbalimbali, ikiwa imefungwa kwenye maboksi ambayo katika udadisi wao walibaini kuwa, baadhi ya bidhaa zinazokuwa kwenye shehena hizo ni kanzu, seti za televisheni, vitabu na silaha za aina mbalimbali.
Walidai kuwa, walianza kukitilia mashaka chuo hicho baada ya kubaini kinapokea silaha katika baadhi ya mizigo yake.
Mbali ya hilo, wakazi hao walilieleza gazeti hili kwamba aina ya wageni wanaoingia na kutoka visiwani humo kwa minajili ya kukitembelea chuo hicho, ni jambo jingine ambalo limekuwa likiwafanya wazidi kukitilia shaka chuo hicho.
Kwa mujibu wa wakazi hao, wageni hao wamekuwa wakiingia kisiwani kwa njia ya mitumbwi wakipita katika njia za panya nyakati za usiku.
Wageni hao kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo la Nansio ni wale wanaodaiwa na kuaminika kutoka katika nchi jirani za Kenya na Uganda ambazo mipaka ya ziwa Victoria inapita.
Wafanyabiashara wanaojihusisha na usafirishaji abiria waliozungumza na gazeti la Mtanzania Jumatano walieleza kuwa, wageni wanaowapakia kuwapeleka chuo cha Markaz au maeneo mengine ya kisiwa hicho huwalazimisha kuondoa misalaba waliyoivaa shingoni au waliyotundika katika magari na pia huwataka wazime redio katika magari yao.
Hofu hiyo ya wakazi wa Nansio ilisababisha gazeti hili kumtafuta Mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemli (Chadema) ambaye naye alikiri kulifahamu jambo hilo.
Akizungumza kupitia simu yake ya kiganjani, Machemli alisema chuo hicho kinatoa mafunzo ambayo wakazi wake wanayahusisha na matendo ya kigaidi.
Mbunge huyo alisema hofu zaidi kuhusu chuo hicho ni kuwapo kwa taarifa zinazodai kwamba, baadhi ya wanachuo ambao wamewahi kupata mafunzo chuoni wanatajwa kuwa wanachama wa makundi ya kigaidi ya Al Qaeda na Al-Shabab.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, miongoni mwa hatua ambazo amepata kuzichukua ili kutafuta majibu ya wasiwasi wa wananchi wa Ukerewe ni pamoja na kumsaka mmoja wa watu anayekijua chuo hicho.
Ni kweli tuna wasiwasi na hatuoni kazi ya umma kinachojihusisha nacho. Niliwahi kumuuliza Diwani wa Kata ya Nansio, Sheikh Ramadhani Mazige (CCM) kuhusu uhalali wa kuwapo kwa chuo hicho kwa sababu alikuwa akisimamia ujenzi wake na nikashauri juu ya umuhimu wa kubadili aina ya mafunzo yanayofundishwa chuoni hapo na jibu lake lilikuwa wenye chuo hawataki.
Alipoulizwa iwapo anawafahamu wamiliki wa chuo hicho, alikana kuwatambua kwa kueleza kuwa, jitihada zake za kuwafahamu hazikufanikiwa baada ya Diwani Mazege kukataa kuwataja.
Machemli alisema kuwa, amepanga kulifikisha suala hilo kama hoja binafsi kwenye Baraza la Madiwani ili kuomba kibali cha kutembelea chuo hicho kuona shughuli zinazofanyika na kwamba iwapo atakwamishwa, atalifikisha suala hilo katika ngazi za juu.
Akizungumza kuhusu raia wa kigeni wanaopitia njia za panya kwa usafiri wa mitumbwi nyakati za usiku kufika chuoni hapo, Machemli alisema hilo hawezi kulipinga.
Kwa mujibu wa Machemli, jiografia ya visiwa vya Ukerewe inavifanya viwe wazi kuhusu mipaka yake na kwamba jambo hilo alipata kulizungumza bungeni ingawa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha alimpuuza.
Nilizungumza katika mkutano uliopita wa Bunge kuhusu mipaka ya Ukerewe kuwa wazi sana, nililalamika kwamba, wanajeshi wa Kenya na Uganda wanakuja hadi katika kisiwa hicho kufanya mazoezi yake na kuondoka, lakini nashangaa waziri akanipuuza, alilalamika Machemli.
Alipotafutwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu kwa ajili ya kuzungumzia juu ya hofu hiyo, alisema anaomba apewe muda kwa sababu yeye ni mgeni mkoani humo na huu mwezi wa pili akiwa katika kituo chake kipya cha kazi, hivyo yapo mengi ambayo hayafahamu.
Hata hivyo, Mangu aliliahidi gazeti hili kufuatilia juu ya suala hilo na kulitolea ufafanuzi baadaye.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mary Tesha alikana kufahamu chochote na badala yake akahoji sababu za mwandishi kumtafuta wakati tayari suala hilo lilisharipotiwa katika gazeti hili hivi karibuni.
Kumekuwa na tetesi za kuwepo kwa vikundi vinavyojihusisha na utoaji mafunzo ya kigaidi hapa nchini, vikiwa vimejificha katika mwamvuli huku lengo halisi likiwa kuhatarisha amani ya kitaifa.
Tayari Rais Jakaya Kikwete amekwishaagiza kusakwa kwa makundi yenye mwelekeo huo yanayohisiwa kuhusika na machufuko na mauaji hapa nchini, wakati akitoa salamu za pole baada ya tukio la kuuawa kinyama kwa Padre wa Kanisa Katoliki Evaritus Mushi huko visiwani Zanzibar.
Maoni --
123
-
-1
#26 Chibwana 2013-02-23 12:24
Hili ni sakata jipya ambalo Gazeti hili linaanzisha kuchochea.
Matokeo yeyote ya hili ni lazima mmiliki na uongozi wa gazeti hili uwe "RESPONSIBLE". Nawasihi acheni kutumia vibaya uhuru muliopewa wa habari kwa kunadi amani ya nchi kupitia idara nyeti kabisa ya IMANI ZA WATU. Musitarajie kuwa uchochezi huu utaishia hapo. It's Shame kwa tasnia ya habari !!!!
Nukuu
-
-
-1
#25 ABUBAKARI KARATA 2013-02-23 04:50
Hivi kweli shule kufundisha Karate na Kumfuu ni Ugaidi, Kwa hiyo Wachina na wajapani ni magaidi, Ama kweli tumekosa hoja, na ni kweli kwamba abiria amuamuru mwenye chombo aondoe misalaba, Kweli? Na chuo kutembelewa na wageni ni kosa, mbona tunaona wazungu wanamiminika huku Arusha kutembelea Makanisa, au kwakuwa ni makanisa na hiyo Ni mali ya waislam. Tupime jamani Ni aibu kwagazeti kama hili kuandika mambo ambayo hayana hoja na hayana mashiko kana kwamba waandishi ni mambumbumbu wa kupima mambo.
Nukuu
-
-
-1
#24 chorobi 2013-02-23 02:41
NASAHA KWA WASOMAJI HEBU TUANGALIE VYOMBO HIVI VYA HABARI AMBAVYO VINATOA HABARI ZA UCHOCHEZI KWANI LITAKALOTEKEA HAKUNA ATAKWYE SALIMIKA MTANZANIA PAMOJA NA WAANDISHI WAKE WATATUANGAMIZA NDANIN YA NCHI HII KINACHONITIA SHAKA KATIKA HABARI KAMA HIZI JINA LA MWANDISHI HAWALIWEKI HII NI KUONYESHA KUWA HABARI ZAO HAZINA UHAKIKA NA HAWAJIAMINI PIA SI ZA UKWELI KWANINI WAWEKE NA MWANDISHI WETU?INAMAANA HABARI HIYO MWANDISHI WAKE HANA JINA KUNA KILA JITIHADA ZA WASOMAJI KUFAHAMU KUWA MTANZANIA HAITAKII MEMA NCHI HII NA TAMBUENI KUWA UISLAM NA UGAIDI NI TOFAUTI KABISA NI SAWA NA MASHARIKI NA MAGHARIBI HIVYO TAMBUENI KUWA WAISLAM HAWAHUSIKI NA UGAIDI HATA SIKU MOJA KWANI DINI YAO IMEWAELEZA KILA KITU JINSI YA KUISHI NA NDUGU ZAO KATIKA ADAMU TAHADHARINI SAAAANA WASOMA JI WA GAZETI HILI TUTANGAMIA KUTOKANA NA KALAMU HIZI ZA WAANDISHI AMBAO HAWAITAKII MEMA TANZANIA HIII
Nukuu
-
-
-1
#23 chorobi 2013-02-23 02:32
Hakuna asiyefahamu kuwa gazeti la mtanzania ni gazeti ambalo lina agenda za siri na waislam kwa maana habari zake zote zinazotoka za kiislam ni dhahiri za kiuchochezi baina ya serikali kuna habari nyingi saana ukifuatilia hazina maaana yoyote nashukuru kuna chombo kimoja cha habari(RADIO IMAN)Waliweza kuwatafuta viongozi wote wa ukerewe ambao mwandishi wa habari hizo alisema walimpa ushahidi na kulifahamu tukio hilo na wao viongozi kukataa na kuonyesha kuwa chuo hicho kinatoa mafunzo yanayohusu dini pekee na hakuna mwananchi ambaye alishalalamika kuhusu chuo hicho TAHADHARI KWA WAISLAM KWANZANI KULISUSIA GAZETI HILI LA MTANZANIA KWANI HALINA MAANA KWETU NA NI WACHOCHEZI SANA
Nukuu
-
-
0
#22 Raia Mwema 2013-02-22 11:28
Bwana Mohamed Hamad, kwa nini unahamaki sana na kuhukumu kuwa mtanzania ni waongo. Wewe umetoa wapi huo ukweli mara hii? Nilitaraji ungeamua kufanya na wewe utafiti kama alioufanya mwandishi wa Mtanzania, then uje na matokeo tofauti yatusaidie. Lakini unaposhuka na nyundo bila altenative tukueleweje hapo. Kwamba na wewe ni mmoja wao?
Nukuu
-
-
0
#21 hayaland 2013-02-22 06:34
lisemwalo lipo kama halipo basi tujiandae .uislam ni ugaidi na hilo kamwe halipingiki.una jua hakuna mtu ambaye atakaa kimya kwa ujinga na uharamia.unajua wakristo wanatumia sana busara lakini inafika hatua kamwe uvumilivu unafikia kikomo na atakayeamuru ugonvi aidha jeshi la wananchi au viongozi wa dini zote mbili.tunatangu liza busara lakini busara ina mwisho wake.
Nukuu
-
-
+1
#20 Mohammed Hamad 2013-02-22 06:30
Mtanzania linajulikana kwa kuandika habari za kichochezi na zenye chuki, ni gaazeti linalotumikia watu wenye maslahi yao binafsi nasema hivi kwa kuwa hakuna asiejua walichomfanyia mzee Salim Ahmed Salim wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005! Hawa ndio Mtanzania sijui watfaidika na nini ikiwa machapisho yao yatasababisha uvunjifu wa amani nchi. Wewe mwandishi unadhani utaandika tena? Unajiita "Mwandishi Wetu" kwanini usiweke jina lako bayana? wewe ni mwoga na woga unao kwa kuwa unajua habari uliyoandika ni majungu. Tumeishi na kuzaana na wakristo wa madhehebu mbalimbali. Nina marafiki wengi niliosoma nao ambao ni wakristo na wengine wamekuwa kama ndugu! Habari zenu kama hizi haziwezi kuwafanya wanione adui kwa sababu ya dini yangu sana sana watawaona wapumbavu! Acheni fitina andikeni habari zenye kuleta tija kwenye taifa hili njaa zitawaua.
Nukuu
-
-
0
#19 mamamaaa 2013-02-20 18:09
ndugu zetu waislamu nao wamezidi kufanya fujo zisizoza maana. kwa mfano kuua kama yaliyotokea huko zanzibar, kuchoma makanisa. si ajabu mkihisiwa kuwa mwashirikiana na al shabab au makundi mengine yoyote ni kutokana na yale yanayotokea kwenye jamii yanayofanywa na wafuasi wa dini hii. jifunzeni kusamehe na siyo kulipa visasi. Yesu anawapenda!
Nukuu
-
-
+1
#18 jane joseph 2013-02-20 18:02
WATANZANIA TUMEFUNDISHWA UPENDO NA UMOJA. TUSIKUBALI KUINGIZIWA ELIMU MPYA YA CHUKI NA UVUNJIFU WA AMANI KWA MASLAHI YA WENGINE.
Nukuu
-
-
+2
#17 jane joseph 2013-02-20 18:00
HABARI KWA KWELI INATISHA - INATISHIA AMANI YA NCHI NZIMA BILA KUJALI DINI GANI. CHA MUHIMU NDUGU ZETU WAANDISHI WA HABARI JITAHIDINI KUFANYA UCHUNGUZI WAKUTOSHA KABLA HAMJATOA HABARI WA WANANCHI ILI KUEPUKA MKANGANYIKO AU UVUNJIFU WA AMANI. NAWASHAURI MTOE TAARIFA ZINAZOHAMASIHA UMOJA NA AMANI, CHOKOCHOKO HAZITATUFIKISHA POPOTE.
Nukuu
-
123
Rekebisha orodha ya maoni
RSS feed for comments to this post
Toa Maoni yako kwa habari hii
Jina (linahitajika)
Barua Pepe (Inahitajika, lakini hatutaionyesha)
1000 symbols left
Nijulishe juu ya maoni yanayoendelea
Huisha
Tuma
JComments