Absalom Kibanda (Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri) avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa


Wewe ni mmoja wao eeenh? Subiri FBI wakimaliza kazi zenj kisha watakuja uwaeleze vizuri.
 
Kwa mchezo huu tukifika 2015 wengi tu watakuwa wameuawa au kujeruhiwa sana. Utasikia ni vyombo vya usalama vya nchi jirani vimefanya mambo.
 
Waache wafe tuu hatuoni mchango wao zaid ya fitna hasa kwetu sisi waznz
 
Tanzania Daima gazeti la Mbowe,Lilian Mke wa Mbowe na Mmiliki wa Chadema ni Mbowe! Bado huoni Connection?
In so saying, CCM na Kikwete wameshindwa kuongoza nchi kwa kuwa wameshindwa kuwahakikishia raia haki yao ya kuishi, ambayo ni haki ya msingi, kutokana na kushindwa kudhibiti ujambazi na ughaidi kama huu. Kama ndani ya nchi kuna chama au mtu au kikundi cha watu kinachoweza kupanga na kutekeleza umafia kama huu ni dhahiri serikali haipo au kama ipo basi ni taabani.
 
Nchi ya mambo ya ajabu ajabu,bado kitekwa JK mwenyewe.!
 
nimekupata mkuu. You hv realy thought aloud. Wanatafuta pa kutokea.

mbona uchunguzi unafanywa na polisi iweje mnaaza kujitetea wkt bado hamjaitwa kujieleza.Kwa akili ya kawaida tuwaeleje
 
Haihitaji uwe wakili ili kuweza kufahamu kwamba tukio hili halikufanywa na CHADEMA!

KUSHAMBULIWA KWA KIBANDA-NIMUHANGA WA ALICHOKIANDIKA..? Connected dots…!
Jana usiku limetokea tukio baya la kuvamiwa na kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari Corporation, Ndugu Abdalom Kibanda.
Tukio hilo ambalo limesababisha sintofahamu kubwa miongoni mwa watanzania wanahabari, wapenda uwazi na ukweli na wale wenye kusimamia misingi ya Amani na utulivu katika nchi hii.
Aina ya tukio lenyewe na upekee wa utokeaji wake umegubikwa na utata mkubwa kiasi kwamba akili yangu ikanituma kutafakari kwa kina na kuyaandika haya, ikiwa ni miongoni mwa YAWEZEKANAYO kuwa ndiyo yaliyosababisha tukio ilo la kusikitisha kutokea kwa Mtanzania mwenzetu huyu kipenzi cha wanahabari.
•Mengi yanahusuanishwa na tukio hili, lakini wengi wakihusianisha tukio hili na kazi ya mhusika ya Uandishi, ambapo tukio hili linamkuta katika kipindi ambacho mtindo wa uandishi wake umebadilika na mfumo wa hoja zake umekuwa wa mlengwa wa kati. Lakini pia wapo wachache wanaohusianisha tukio hilo na ujambazi ama unyang’anyi, hisia ambazo binafsi nazipinga kwani Watu waliomvamia na kumtoa katika gari kisha wakampiga kabla ya kumtupa na kumtelekeza umbali mdogo na nyumbani kwake hawakuchukua kitu chochote katika vitu ambavyo Mhariri huyo anavimiliki kuanzia gari, simu na pesa.
•Hivyo, nalihusianisha tukio hili na aina ya kazi ambayo mhanga anaifanya, kazi ya UHARIRI WA HABARI katika vyombo vya habari, na hisia zangu zimenipeleka huko baada ya kuzingatia kwa umakini mkubwa matukio yafuatayo.
a)14th November 2012, Baada ya kuundwa kwa sekretarieti mpya ya chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Kibanda akiwa ni Mhariri wa Gazeti la Tanzania Daima ambalo linafahamika wazi kuwa ni chombo cha propaganda cha Chadema chini ya Mbowe, aliandika makala ambayo ilikuwa ikisifu safu hiyo mpya ya uongozi ya CCM,
huku akinukuu kauli mbalimbali za viongozi wa upinzani akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Znz, Mhe. Maalim Seif Sharif. Baada ya tukio hili wakuu wa gazeti hilo walimuita na kumuonya juu ya makala yake hiyo.
Lakini katibu Mkuu wa Chadema hakuishia na kuridhishwa kwa kuonywa kwa Kibanda bali alienda mbele zaidi na kumjibu; ambapo tarehe 16th November 2012, sehemu ya nukuu yake alipokuwa akimjibu Kibanda inapatikana katika link hii; http://www.habarimasai.com/en/ziliz...i-mpya-ya-ccm-asema-wapo-kwenye-kashfa-ya-epa

Na link nyingine ndani ya Tanzania Daima la ijumaa ya tarehe 16 th Nov 2012 ni hii;

http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=42529

b)Lakini mara tu ya jibu hilo la Slaa kwa Kibanda, Mhariri huyo kwa ufundi mkubwa aliandika makala nyingine ambayo ilikuwa ikimsifu zaidi Katibu Mkuu mpya wa CCM, ndugu Abdulrahaman Kinana, ambae Slaa alimkosoa katika majibu yake dhidi ya Kibanda. Mhariri huyo makini alieleza bayana kuwa kuiponda sekreatieti mpya ya CCM ni sawa na kukosa akili, akaendelea kufafanua na kutaja wasifu wa kila kiongozi kwa kadri alivyowafahamu yeye, akielekeza nguvu zaidi kwa Katibu Mkuu Kinana na kuelezea umahiri wa kinana kama strategist tangu akiwa jeshini, lakini akataja uzoefu wake ndani ya chama na pia kutaja alivyoshiriki katika chaguzi mbalimbali na kuwawezesha wagombea urais wa Awamu ya tatu na Nne kushinda kwa kishindo.
Baada ya Makala hiyo ya pili, ulizaliwa mgogoro wa haja ndani ya kampuni hiyo ya freemedia uliomuhusisha Kibanda na wamiliki wa kampuni na Chama kinacholitumia gazeti hilo. Mgogoro ambao ulipelekea Kibanda kuihama Freemedia na kuhamia katika New Habari Corporation ambayo kimsingi ni ya wadau wa Chama Cha Mapinduzi na kampuni ambayo kwa namna moja ama nyingine inaruhusu kuandikwa habari katika mandhari na tafsir ya HABARI bila propaganda wala upendeleo. Kwa maana nyingine ni kuwa Ndugu Kibanda alikuwa akihariri habari ambazo zinasema ukweli wa mazuri ya chama cha Mapinduzi na kuimwagia sifa kwa mipango yake ya kuiletea nchi Maendeleo lakini pia kwa kasi ya utekelezaji wa Ilani ya chama.
Baada ya Uamuzi huo wa Kibanda kuhamia New Habari Corporation na kuiandika habari zenye mlengwa wa Kati, wakuu wa Free media walimuita ili kufanya nae mazungumzo ya kumtaka kurejea katika kampuni yao, hasa baada ya Gazeti lao la Tanzania Daima kuanza kupoteza dira na kuandika habari ambazo hazina mvuto hivyo kulifanya kushuka kimauzo na kipropaganda dhidi ya Chama Cha Mapinduzi. Lakini Kibanda aliendelea kukataa kurudi na kuwa pamoja na viongozi hao wasiojua nini maana ya kuwa kiongozi, hawaheshimu taaluma wala hawataki kuruhusu fikra huru kuchukua nafasi katika chama na Kampuni zao.
Kulingana na ukweli huo wa kuwepo kwa uhasama baina ya Mhariri Huyu makini na mabosi wake wa kampuni aliyokuwa akiifanyia kazi hapo awali, hisia zangu zinanipelekea kuamini kuwa yawezekana kabisa mpango huu wa kumvamia, kumshambulia na kuhatarisha maisha yake umeratibiwa na viongozi hao ambao hali nao sahani moja, na ndiyo asili ya swali JE, KIBANDA ni muhanga wa alichokiandika..?
 
yule mkenya amerudi cjui sasa hivi ataenda kutubu kanisa gani ili wamkamate
 
Hofu ya Al Qaeda Ukerewe
JUMATANO, FEBRUARI 20, 2013 05:04 NA MWANDISHI WETU
*Wananchi wakihusisha chuo na ugaidi
*Mbunge ataharuki, aandaa hoja binafsi
*Mkuu wa Mkoa, DC wakwepa kunena
HOFU ya kuwapo kwa magaidi wa mtandao wa Al- Qaeda, imetanda katika Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, baada ya kuvuja kwa taarifa za kuanzishwa kwa chuo kimoja cha kidini kinachohofiwa kutoa mafunzo yenye mwelekeo wa kigaidi visiwani humo.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa chuo hicho kinajulikana kwa jina la Markaz, Aljazeera na kimeanzishwa kwa ufadhili wa raia wa kigeni ambao ni waumini wa dini ya Kiislamu.

Makundi yanayotajwa kufadhili uendeshaji wa chuo hicho ni Al-Qaeda na Al shabab yanayoaminika kuwa na mtandao mkubwa wa ugaidi duniani.

Uchunguzi uliofanywa na Mtanzania Jumatano wilayani Ukerewe, umebaini kuwa chuo cha Markaz kinatoa mafunzo kwa watu wa rika mbalimbali yenye mwelekeo wa kujihami na kushambulia kama Karate na Kung-fu.

Aidha, taarifa nyingine za kiuchunguzi ambazo gazeti hili lilidokezwa na wakazi wa kisiwani humo walioonyesha wasiwasi wa kuwepo kwa chuo hicho, zilidai kuwa, aina nyingine ya mafunzo yanayotolewa katika chuo hicho na kushambuliana kwa silaha aina ya jambia.

Uchunguzi ulibaini zaidi kuwa, wanafunzi katika chuo hicho ni watoto wenye umri wa kati ya miaka saba hadi 10 na pia kuna wanafunzi vijana na watu wazima.

Baadhi ya wakazi wa wilayani humo waliopata kufanya kazi katika chuo hicho, waliliambia gazeti hili kuwa chuo hicho kimekuwa kikipokea mizigo ya aina mbalimbali, ikiwa imefungwa kwenye maboksi ambayo katika udadisi wao walibaini kuwa, baadhi ya bidhaa zinazokuwa kwenye shehena hizo ni kanzu, seti za televisheni, vitabu na silaha za aina mbalimbali.

Walidai kuwa, walianza kukitilia mashaka chuo hicho baada ya kubaini kinapokea silaha katika baadhi ya mizigo yake.

Mbali ya hilo, wakazi hao walilieleza gazeti hili kwamba aina ya wageni wanaoingia na kutoka visiwani humo kwa minajili ya kukitembelea chuo hicho, ni jambo jingine ambalo limekuwa likiwafanya wazidi kukitilia shaka chuo hicho.

Kwa mujibu wa wakazi hao, wageni hao wamekuwa wakiingia kisiwani kwa njia ya mitumbwi wakipita katika njia za panya nyakati za usiku.

Wageni hao kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo la Nansio ni wale wanaodaiwa na kuaminika kutoka katika nchi jirani za Kenya na Uganda ambazo mipaka ya ziwa Victoria inapita.

Wafanyabiashara wanaojihusisha na usafirishaji abiria waliozungumza na gazeti la Mtanzania Jumatano walieleza kuwa, wageni wanaowapakia kuwapeleka chuo cha Markaz au maeneo mengine ya kisiwa hicho huwalazimisha kuondoa misalaba waliyoivaa shingoni au waliyotundika katika magari na pia huwataka wazime redio katika magari yao.

Hofu hiyo ya wakazi wa Nansio ilisababisha gazeti hili kumtafuta Mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemli (Chadema) ambaye naye alikiri kulifahamu jambo hilo.

Akizungumza kupitia simu yake ya kiganjani, Machemli alisema chuo hicho kinatoa mafunzo ambayo wakazi wake wanayahusisha na matendo ya kigaidi.

Mbunge huyo alisema hofu zaidi kuhusu chuo hicho ni kuwapo kwa taarifa zinazodai kwamba, baadhi ya wanachuo ambao wamewahi kupata mafunzo chuoni wanatajwa kuwa wanachama wa makundi ya kigaidi ya Al Qaeda na Al-Shabab.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, miongoni mwa hatua ambazo amepata kuzichukua ili kutafuta majibu ya wasiwasi wa wananchi wa Ukerewe ni pamoja na kumsaka mmoja wa watu anayekijua chuo hicho.

“Ni kweli tuna wasiwasi na hatuoni kazi ya umma kinachojihusisha nacho. Niliwahi kumuuliza Diwani wa Kata ya Nansio, Sheikh Ramadhani Mazige (CCM) kuhusu uhalali wa kuwapo kwa chuo hicho kwa sababu alikuwa akisimamia ujenzi wake na nikashauri juu ya umuhimu wa kubadili aina ya mafunzo yanayofundishwa chuoni hapo na jibu lake lilikuwa wenye chuo hawataki.

Alipoulizwa iwapo anawafahamu wamiliki wa chuo hicho, alikana kuwatambua kwa kueleza kuwa, jitihada zake za kuwafahamu hazikufanikiwa baada ya Diwani Mazege kukataa kuwataja.

Machemli alisema kuwa, amepanga kulifikisha suala hilo kama hoja binafsi kwenye Baraza la Madiwani ili kuomba kibali cha kutembelea chuo hicho kuona shughuli zinazofanyika na kwamba iwapo atakwamishwa, atalifikisha suala hilo katika ngazi za juu.

Akizungumza kuhusu raia wa kigeni wanaopitia njia za panya kwa usafiri wa mitumbwi nyakati za usiku kufika chuoni hapo, Machemli alisema hilo hawezi kulipinga.

Kwa mujibu wa Machemli, jiografia ya visiwa vya Ukerewe inavifanya viwe wazi kuhusu mipaka yake na kwamba jambo hilo alipata kulizungumza bungeni ingawa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha alimpuuza.

“Nilizungumza katika mkutano uliopita wa Bunge kuhusu mipaka ya Ukerewe kuwa wazi sana, nililalamika kwamba, wanajeshi wa Kenya na Uganda wanakuja hadi katika kisiwa hicho kufanya mazoezi yake na kuondoka, lakini nashangaa waziri akanipuuza,” alilalamika Machemli.

Alipotafutwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu kwa ajili ya kuzungumzia juu ya hofu hiyo, alisema anaomba apewe muda kwa sababu yeye ni mgeni mkoani humo na huu mwezi wa pili akiwa katika kituo chake kipya cha kazi, hivyo yapo mengi ambayo hayafahamu.

Hata hivyo, Mangu aliliahidi gazeti hili kufuatilia juu ya suala hilo na kulitolea ufafanuzi baadaye.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mary Tesha alikana kufahamu chochote na badala yake akahoji sababu za mwandishi kumtafuta wakati tayari suala hilo lilisharipotiwa katika gazeti hili hivi karibuni.

Kumekuwa na tetesi za kuwepo kwa vikundi vinavyojihusisha na utoaji mafunzo ya kigaidi hapa nchini, vikiwa vimejificha katika mwamvuli huku lengo halisi likiwa kuhatarisha amani ya kitaifa.

Tayari Rais Jakaya Kikwete amekwishaagiza kusakwa kwa makundi yenye mwelekeo huo yanayohisiwa kuhusika na machufuko na mauaji hapa nchini, wakati akitoa salamu za pole baada ya tukio la kuuawa kinyama kwa Padre wa Kanisa Katoliki Evaritus Mushi huko visiwani Zanzibar.

Maoni --

123
-
-1 #26 Chibwana 2013-02-23 12:24
Hili ni sakata jipya ambalo Gazeti hili linaanzisha kuchochea.
Matokeo yeyote ya hili ni lazima mmiliki na uongozi wa gazeti hili uwe "RESPONSIBLE". Nawasihi acheni kutumia vibaya uhuru muliopewa wa habari kwa kunadi amani ya nchi kupitia idara nyeti kabisa ya IMANI ZA WATU. Musitarajie kuwa uchochezi huu utaishia hapo. It's Shame kwa tasnia ya habari !!!!
Nukuu
-
-
-1 #25 ABUBAKARI KARATA 2013-02-23 04:50
Hivi kweli shule kufundisha Karate na Kumfuu ni Ugaidi, Kwa hiyo Wachina na wajapani ni magaidi, Ama kweli tumekosa hoja, na ni kweli kwamba abiria amuamuru mwenye chombo aondoe misalaba, Kweli? Na chuo kutembelewa na wageni ni kosa, mbona tunaona wazungu wanamiminika huku Arusha kutembelea Makanisa, au kwakuwa ni makanisa na hiyo Ni mali ya waislam. Tupime jamani Ni aibu kwagazeti kama hili kuandika mambo ambayo hayana hoja na hayana mashiko kana kwamba waandishi ni mambumbumbu wa kupima mambo.
Nukuu
-
-
-1 #24 chorobi 2013-02-23 02:41
NASAHA KWA WASOMAJI HEBU TUANGALIE VYOMBO HIVI VYA HABARI AMBAVYO VINATOA HABARI ZA UCHOCHEZI KWANI LITAKALOTEKEA HAKUNA ATAKWYE SALIMIKA MTANZANIA PAMOJA NA WAANDISHI WAKE WATATUANGAMIZA NDANIN YA NCHI HII KINACHONITIA SHAKA KATIKA HABARI KAMA HIZI JINA LA MWANDISHI HAWALIWEKI HII NI KUONYESHA KUWA HABARI ZAO HAZINA UHAKIKA NA HAWAJIAMINI PIA SI ZA UKWELI KWANINI WAWEKE NA MWANDISHI WETU?INAMAANA HABARI HIYO MWANDISHI WAKE HANA JINA KUNA KILA JITIHADA ZA WASOMAJI KUFAHAMU KUWA MTANZANIA HAITAKII MEMA NCHI HII NA TAMBUENI KUWA UISLAM NA UGAIDI NI TOFAUTI KABISA NI SAWA NA MASHARIKI NA MAGHARIBI HIVYO TAMBUENI KUWA WAISLAM HAWAHUSIKI NA UGAIDI HATA SIKU MOJA KWANI DINI YAO IMEWAELEZA KILA KITU JINSI YA KUISHI NA NDUGU ZAO KATIKA ADAMU TAHADHARINI SAAAANA WASOMA JI WA GAZETI HILI TUTANGAMIA KUTOKANA NA KALAMU HIZI ZA WAANDISHI AMBAO HAWAITAKII MEMA TANZANIA HIII
Nukuu
-
-
-1 #23 chorobi 2013-02-23 02:32
Hakuna asiyefahamu kuwa gazeti la mtanzania ni gazeti ambalo lina agenda za siri na waislam kwa maana habari zake zote zinazotoka za kiislam ni dhahiri za kiuchochezi baina ya serikali kuna habari nyingi saana ukifuatilia hazina maaana yoyote nashukuru kuna chombo kimoja cha habari(RADIO IMAN)Waliweza kuwatafuta viongozi wote wa ukerewe ambao mwandishi wa habari hizo alisema walimpa ushahidi na kulifahamu tukio hilo na wao viongozi kukataa na kuonyesha kuwa chuo hicho kinatoa mafunzo yanayohusu dini pekee na hakuna mwananchi ambaye alishalalamika kuhusu chuo hicho TAHADHARI KWA WAISLAM KWANZANI KULISUSIA GAZETI HILI LA MTANZANIA KWANI HALINA MAANA KWETU NA NI WACHOCHEZI SANA
Nukuu
-
-
0 #22 Raia Mwema 2013-02-22 11:28
Bwana Mohamed Hamad, kwa nini unahamaki sana na kuhukumu kuwa mtanzania ni waongo. Wewe umetoa wapi huo ukweli mara hii? Nilitaraji ungeamua kufanya na wewe utafiti kama alioufanya mwandishi wa Mtanzania, then uje na matokeo tofauti yatusaidie. Lakini unaposhuka na nyundo bila altenative tukueleweje hapo. Kwamba na wewe ni mmoja wao?
Nukuu
-
-
0 #21 hayaland 2013-02-22 06:34
lisemwalo lipo kama halipo basi tujiandae .uislam ni ugaidi na hilo kamwe halipingiki.una jua hakuna mtu ambaye atakaa kimya kwa ujinga na uharamia.unajua wakristo wanatumia sana busara lakini inafika hatua kamwe uvumilivu unafikia kikomo na atakayeamuru ugonvi aidha jeshi la wananchi au viongozi wa dini zote mbili.tunatangu liza busara lakini busara ina mwisho wake.
Nukuu
-
-
+1 #20 Mohammed Hamad 2013-02-22 06:30
Mtanzania linajulikana kwa kuandika habari za kichochezi na zenye chuki, ni gaazeti linalotumikia watu wenye maslahi yao binafsi nasema hivi kwa kuwa hakuna asiejua walichomfanyia mzee Salim Ahmed Salim wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005! Hawa ndio Mtanzania sijui watfaidika na nini ikiwa machapisho yao yatasababisha uvunjifu wa amani nchi. Wewe mwandishi unadhani utaandika tena? Unajiita "Mwandishi Wetu" kwanini usiweke jina lako bayana? wewe ni mwoga na woga unao kwa kuwa unajua habari uliyoandika ni majungu. Tumeishi na kuzaana na wakristo wa madhehebu mbalimbali. Nina marafiki wengi niliosoma nao ambao ni wakristo na wengine wamekuwa kama ndugu! Habari zenu kama hizi haziwezi kuwafanya wanione adui kwa sababu ya dini yangu sana sana watawaona wapumbavu! Acheni fitina andikeni habari zenye kuleta tija kwenye taifa hili njaa zitawaua.
Nukuu
-
-
0 #19 mamamaaa 2013-02-20 18:09
ndugu zetu waislamu nao wamezidi kufanya fujo zisizoza maana. kwa mfano kuua kama yaliyotokea huko zanzibar, kuchoma makanisa. si ajabu mkihisiwa kuwa mwashirikiana na al shabab au makundi mengine yoyote ni kutokana na yale yanayotokea kwenye jamii yanayofanywa na wafuasi wa dini hii. jifunzeni kusamehe na siyo kulipa visasi. Yesu anawapenda!
Nukuu
-
-
+1 #18 jane joseph 2013-02-20 18:02
WATANZANIA TUMEFUNDISHWA UPENDO NA UMOJA. TUSIKUBALI KUINGIZIWA ELIMU MPYA YA CHUKI NA UVUNJIFU WA AMANI KWA MASLAHI YA WENGINE.
Nukuu
-
-
+2 #17 jane joseph 2013-02-20 18:00
HABARI KWA KWELI INATISHA - INATISHIA AMANI YA NCHI NZIMA BILA KUJALI DINI GANI. CHA MUHIMU NDUGU ZETU WAANDISHI WA HABARI JITAHIDINI KUFANYA UCHUNGUZI WAKUTOSHA KABLA HAMJATOA HABARI WA WANANCHI ILI KUEPUKA MKANGANYIKO AU UVUNJIFU WA AMANI. NAWASHAURI MTOE TAARIFA ZINAZOHAMASIHA UMOJA NA AMANI, CHOKOCHOKO HAZITATUFIKISHA POPOTE.
Nukuu
-
123
Rekebisha orodha ya maoni
RSS feed for comments to this post
Toa Maoni yako kwa habari hii

Jina (linahitajika)

Barua Pepe (Inahitajika, lakini hatutaionyesha)


1000 symbols left

Nijulishe juu ya maoni yanayoendelea


Huisha


Tuma
JComments
 

acha vituko
 
Polisi waanze uchunguzi na gazeti la tanzania daima na chadema. kwani hatuelewi ni kwanini alikimbia huko alipokuwa mhariri wa hilo gazeti la mwenyekiti wa chama.

Umekuwa polisi mkamataji mpelelezi mwendesha mashitaka na hakimu kwa wakati mmoja hutayaweza yote hayo.

 
Umejaribu kueleza mengi na kwa ustaadi mkubwa sana kama mtu ambaye amebobea katika propaganda. Lakini napata shaka kidogo katika hili. Je ni nini logic ya CHADEMA kumpiga Kibanda na kumwacha hai? Kama ugomvi wao ni juu ya kile alichokiandika, na kwamba amegoma kurudi kwenye kampuni ya Freemedia, si wangemuua kabisa? Walikuwa na sababu gani ya kumng'oa jicho, meno na kucha na kumpiga panga moja na kumwacha? Je mmemuuliza yeye amewaambia ni nini walichokuwa wanamdodosa wakati wanampiga?

Ninaamini kabisa hizi ni mbinu za kijasusi za CCM, ambazo zimepangwa mahususi ili kutafuta namna ya kuichafua CHADEMA. Sioni msingi wowote wa CHADEMA kufanya jambo la namna hii. Maana haileti maana kabisa kwa CHADEMA kufanya haya na kumwacha hai. Nilitarajia kwamba kama kwa hakika Kibanda ni tatizo kwao basi bila shaka angeuawa.

Lakini pia, tujiulize kama mtu, au kikundi cha watu kinao uwezo wa kupanga mashambulizi kama haya, tuendelee kuamini kwamba serikali yetu ina umakini wowote? Kama mtu popular kama kibanda mwenye attention kubwa ya vyombo vya habari anaweza kuvamiwa kirahisi namna hiyo, je ni watu wangapi wasio na influence katika nchi ambao wanakufa kila siku? Je serikali iliyopewa jukumu la kulinda katiba ya nchi ambayo haki ya kwanza ya raia ni kuishi na imeshindwa kuwahakikishia usalama wananchi kiasi cha mtu, watu au chama kuvamia, kushambulia na kuua, ina uhalali gani wa kuendelea kutawala nchi?

Kwa vyovyote vile, kwa level tuliyofikia, ambapo tunashuhudia padri akipigwa risasi kwenye gari, walimu wakipigwa risasi na polisi, wengine wakilipuliwa kwa mabomu na wengine kutekwa na kuteswa ni dhahiri kwamba Tanzania imekuwa si mahali salama pa kuishi tena. Chini ya utawala wa Kikwete, inafaa sasa tutangaze Tanzania kuwa ni nchi isiyo salama tena kwa maisha na mali za watu.
 
Ni Unyama tena !
Kwanza tupate Matukio ya kuvamiwa kwa kipindi kilichopita:
- Januari 5, 2008, Mhariri wa gazeti la Mwanahali, Saed Kubenea, alivamiwa na kujeruhiwa akiwa ofisini kwake Mwananyamala, Dar es Salaam.

- Septemba 2, 2012, Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Televisheno cha Channel Ten, Daudi Mwangosi alishsmbuliwa na kuuawa katika Kijiji cha Nyololo, Iringa katika vurugu zilizotokea wakati polisi walipokuwa wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliotaka kufanya mkutano na ufunguzi wa tawi.

- Desemba 5, 2012, Mwandishi wa Habari wa Tanzania Daima, Shaaban Matutu alivamiwa nyumbani kwake na polisi ambao walimjeruhi kwa risasi begani.

- Januari 8, 2013, Mwandishi wa Habari wa Radio Kwizera ya Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma, Issa Ngumba alikutwa amekufa msituni na kunyofolewa sehemu zake za siri.

- ………


Maoni…
"husisahau lile tukio la Ulimboka kule Mabwepande"
"My take: je ni nani atafuatia ? Na ni wakati gani ?"

Maelezo Muhimu
Alivyoumizwa;
· Ameng'olewa meno mawili
· Ametobolewa jicho la kushoto
· Amekatwa mara tatu kichwani
· Amepigwa na nondo mara tatu kichwani
· Amenyofolewa kucha mbili, mkono wa kushoto
· Ameumizwa mkononi na mguuni na kitu Kizito

Hatua zilizochukuliwa
· Amepelekwa Afrika Kusini
· IGP ateua timu ya wachunguzi
· Jukwaa, MOAT, watoa tamko
· Afanyiwa uchunguzi Muhimbili.
"Matukio ya kutekwa na kushambuli kwa waandishi wa habari yamekuwa yakishika kasi…, ni jambo la kusikitisha na hatuwezi kukaa kimya kwa hili."
-
Habari kamili
---------------------
Waandishi Wetu,
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda ametekwa na watu wasiofahamika na kisha kumjeruhi vibaya kwa nondo, mapanga na kisha kumng'oa meno, kucha na kumharibu jicho la kushoto.

Tukio hilo la kinyama linafanana kwa kiasi fulani na lile la alilofanyiwa Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania, Stephen Ulimboka.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea juzi usiku wakati Kibanda akirejea nyumbani kwake Goba Punguni, Kata ya Mbezi Juu, kutoka kazini.

Tayari mwandishi huyo mkongwe wa habari, amesafirishwa jana kwenda Afrika Kusini kwa matibabu zaidi. Aliondoka jana akisindikizwa na daktari kutoka Taasisi ya Mifupa Muhimu (Moi).

Mkasa wenyewe
Akizungumza kwa tabu alipokuwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), hospitalini Moi, Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006), alisema:

"Nilifika nyumbani kwangu kama saa sita usiku nikitokea kazini na nilipofika kwenye lango la kuingia ndani nilipiga honi ili mlinzi anifungulie. Lakini ghafla nilivamiwa na kundi la watu ambao walivunja kioo cha gari langu upande niliokuwa nimekaa. Nilitokea kupitia mlango wa abiria lakini sikuweza kuwakimbia watu wale kwani walinikamata na kuanza kunishambulia kwa vitu vizito."

"Baada ya kutoka kwenye gari, nahisi nilikanyaga sehemu mbaya, nikateleza na kuanguka wakanifuata...niliona kama watu watatu hivi wakaanza kunishambulia. Sikuwa nafahamu kilichojiri, lakini nilisikia mwingine akimwambia mwenzake afande ‘mshuti... mshuti' huyo alipoelekeza mtutu na kujaribu ‘kushuti' (kupiga risasi) ilikuwa kama vile imegoma.

"Nikiwa bado niko chini, wakanipiga kwa kitu cha ncha kali kwenye jicho la kushoto, wakaning'oa meno na kucha katika vidole vya mkono wa kulia, walinipiga sana na nilipata maumivu makali. Baada ya kunipiga na kunijeruhi waliniburuza hadi bembeni ya nyumba yangu na kunitupa na wakaondoka, baadaye majirani na wasamaria wema walikuja kuniokoa.

Mashuhuda baada ya tukio
Akizungumza jana, mzazi mwenzake, Angella Semaya alisema wakati Kibanda alipovamiwa hakusikia lolote: "Niliamshwa na kelele za majirani ndipo nami nikaenda eneo la tukio. Sikuamini kama alikuwa Kibanda kwani alikuwa ametapakaa damu huku akigugumia maumivu makali... kwanza sikumjua kama ni yeye kwa jinsi alivyokuwa."

"Nina wasiwasi na hawa watu kuwa wametumwa kwa kuwa hawakuchukua chochote zaidi ya kumdhuru mwili," alisema. Angella aliondoka jana na Kibanda pamoja na Mwandishi wa Habari, Eric Kabendera ili kumsindikiza Afrika Kusini atakapokuwa anapata matibabu.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Hussein Bashe alisema: "Tulikuwa na Kibanda hadi usiku kama 5:30 hivi, tukifuatilia matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Kenya na tulipoona hakuna kinachoendelea zaidi, tukaagana kurudi makwetu."

"Kwa kweli taarifa za kuvamiwa na kushambuliwa kwake zimetushtua, kwani ameumizwa sana hasa jicho. Daktari alishauri jicho liondolewe lakini nilikataa, jopo la madaktari bingwa wa macho wamemtazama na kuthibitisha kweli limeumia sana, tumewasiliana na mwajiri wetu ameamua kumpeleka Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.

"Nawashukuru madaktari kwa jinsi walivyompokea na kumshughulikia katika kiwango kinachotia moyo. Pia waandishi kwa umoja waliouonyesha kwa kujitokeza haraka na kumjulia hali."
Tasnia ya habari
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limeelezea kushtushwa na tukio la kutekwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa mwenyekiti wake.

Taarifa ya TEF iliyotolewa jana na Katibu wake, Neville Meena, imesema shambulio hilo ni uthibitisho kwamba mazingira ya kikazi ya waandishi wa habari Tanzania siyo salama tena... "Tunapaswa kuchukua hatua za kutathmini upya mazingira ya kazi zetu, ili kuhakikisha kwamba walau tunakuwa salama."

Alisema mwendelezo wa vitendo vya kuwashambulia waandishi wa habari ambavyo katika siku za karibuni vimeibuka, vinalifanya jukwaa liamini kwamba wanahabari sasa wanatishwa ili wasiweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

"Utesaji huu aliofanyiwa Kibanda unafanana na ule aliofanyiwa Dk Ulimboka. (Rejea vitendo vya kupigwa kichwani, kung'olewa kucha na meno).

Aidha, Meena alisema: "Tunaamini kwamba yaliyomkuta Kibanda hayawezi kutenganishwa na msimamo wake kikazi au kama mtu binafsi. Tunasema hivyo tukizingatia kwamba wahusika hawakuchukua chochote liwe, gari au vitu vilivyokuwamo ndani ya gari hilo vikiwamo laptop, ipad, simu za mkononi na vinginevyo."

"Tunaamini vyombo vya dola, vitachunguza na kuwatia mbaroni kisha kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wa tukio hili na mengine kadhaa ambayo sasa yamegeuka kuwa sehemu ya utamaduni katika nchi yetu."

Awali, Mjumbe wa Bodi ya TEF, Theophil Makunga alisema wakati huu wanahabari na wanafamilia wakisubiri uchunguzi juu ya tukio hilo, kitendo hicho hakina budi kulaaniwa.
"Hatuwezi kusema nini chanzo cha tukio hilo kwa sasa, lakini tunaamini limetokana na kazi yake. Tunalaani vikali kwani tunaweza kusema kazi yetu sasa si salama tena," alisema Makunga.

Mhariri Mtendaji wa Nipashe, Jesse Kwayu alisema tukio hilo halina uhusiano na ujambazi kutokana na mazingira ya jinsi lilivyotokea na kutaka hatua za haraka za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika.

Mhariri wa Habari wa Tanzania Daima, Edson Kamukara alisema: "Matukio ya kutekwa na kushambuliwa kwa waandishi wa habari yamekuwa yakishika kasi... ni jambo la kusikitisha na hatuwezi kukaa kimya kwa hili."

Baada ya tukio
Katika taarifa yake jana, Dk Nchimbi alisema Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema ameteua timu ya maofisa wa polisi wanne kutoka Makao Makuu ya Upelelezi kuungana na wapelelezi kutoka Kanda Maalumu ya Polisi Mkoa wa Kinondoni ili kuhakikisha waliohusika wanakamatwa.

Baadaye jana Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema ofisi yake imeunda jopo la maofisa wa polisi tisa ambao wameshaanza kazi ya upelelezi wa tukio hilo.

Kova alisema kitendo alichofanyiwa Kibanda si cha kihalifu, bali kukomoana na visasi kwa kuwa upelelezi wa awali umeonyesha kuwa waliomvamia hawakuchukua chochote.
Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene alisema Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia idara yake imepokea kwa mshtuko tukio la kupigwa na kutendewa ukatili.

Alisema kitendo kilichofanywa kwa mhariri huyo ni ukatili uliopitiliza na kwamba wanaliachia Jeshi la Polisi lifanye kazi yake.

Wamjulia hali
Kabla ya Kibanda kupelekwa Afrika Kusini, viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal walifika kumjulia hali. Wengine ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene na Yussuf Omar Chunda na Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk Reginald Mengi.

Mengi na Mbowe
Akizungumza tukio hilo, Dk Mengi mbali ya kulaani, aliwataka waandishi wa habari kuandika ukweli na kuhakikisha haki inapatikana kwa kuwa jambo hilo ni zito.
Alisema kuna haja ya polisi kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli halisi upatikane na wahusika wafikishwe katika vyombo vya sheria.

Mbowe alisema: "Tuungane katika kutetea uhuru wa vyombo vya habari. Uvamizi wa Kibanda ni doa kubwa katika tasnia ya habari bila kujali yuko chombo gani na yeye ndiye mkuu wa Jukwaa la Wahariri, ni wazi atakuwa amezungukwa na maadui wengi."
Imeandikwa na Joyce Mmasi, Aidan Mhando, Bakari Kiango, Salhim Shao, Beatrice Moses na Aziza Masoud.

Source: Mwananchi
 
Cjawahiona utawala legelege kama huu,ilikua Ulimboka sasa kibanda,tutaona mambo mengi zaidi ya kushangaza hadi uchaguzi upite 2015
 
Nina matumaini kwamba Absalom Kibanda ataendelea kupata matibabu yanayostahili ili atakapopata nafuu ya kuridhisha basi atatusimulia kisa hiki cha kusikitisha.

Halafu mkuu PM naona ulipolenga ndio mahala penyewe maana ukiunganisha hizo "data" utaona kwamba kuna mambo mawili.

Mtazamo wangu kwenye hili jambo utakuwa tofauti kidogo kwa kuzingatia uzito wa taarifa hii.

Kwanza, inawezekana gazeti la Mtanzania limeingilia kazi ya upelelezi uliokuwa ukifanywa na majasusi kwa kuzingatia kuwa kuingia kisiwani Nansio ni ngumu nyakati za mchana hivyo upelelezi wake uonekane unachukua muda mrefu.

Hapo namaanisha kwamba upepelezi wa jambo kama hilo la Ukerewe kwa wao majasusi na hasa wa nje ingeweza kuchukua miezi mingi sana hivyo kuharibu kazi ya uchunguzi huchukiza sana. Pia inawezekana kwamba kulitolewa onyo la kutovujisha habari yoyote inayohusiana na chuo hicho , hivyo kuonekana kwake kwenye gazeti labda kumeleta kuingiliana kikazi.

Hapa namaanisha kwamba wale waliomfanyia mbaya bwana Kibanda wametumia nafasi hiyo kufanya walichokifanya kwa kutaka kuchonganisha pande zote.

Pili, katika wasomaji waliotoa maoni utagundua baadhi yao ambao wanaonekana kulifuatilia gazeti hilo mwenendo wake kwa kuzingatia kwamba wanalionya juu ya uchochezi, uchonganishi kupitia dini na imani za watu na kulitahadhalisha gazeti hilo kuwa "responsible" na matoleo yake.

Pia mifano imetolewa kwamba hata Radio Iman waliwatafuta viongozi wa shule hiyo kisiwani humo kuzungumzia jambo la kuwepo shule ya namna hiyo lakini hakukuthibitishwa chochote.

Mimi nasema, uandishi wa mleta habari katika gazeti hilo haukuzingatia vigezo na mifano halisi kwamba kuna shule ambayo inafadhiliwa na watu wasiojulikana na kilichofanyika ni kuandika kwamba kila mara yanatumika maneno kama "uchunguzi uliofanywa" au "uchunguzi umebaini", lakini hakuna mifano hali kama picha kuonyesha maboksi na baada ya maboksi hayo kufunguliwa, santuri za DVD kama kuna ambae amepata nakala yoyote inayoonyesha mtiririko wa mafunzo hayo na mambo mengine.

Uandishi wa kuchungua unakwenda na vigezo na mifano halisi si vinginevyo na kwenye jambo zito kama hili hapo naona kama gazeti hili limetibua kitu.

Ugaidi upo na utaendelea kuwepo hasa barani Afrika baada ya kudhibitiwa katika nchi za walengwa, hivyo ni lazima taarifa zake ziwe zinaandikwa kwa umakini wa hali ya juu na waandishi waliobobea katika fani za upelelezi na uchunguzi, ili zisaidie walengwa wa siku zote na walengwa wapya.
 
Kuna tendency ya traumatic events kujirudia once started ... Ilianza na Dr Ulimboka and many more to come -if strong action against them not taken!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…