Absalom Kibanda (Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri) avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa

Absalom Kibanda (Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri) avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa

Tusiwe wepesi wa kuchora mstali na kuhitimisha kwenye jambo linalohitaji fikra pevu na uchunguzi mpana.
Cha kufanya ni kumtakia heri huku uchunguzi ukiendelea.

Hivi mapalala maana yake ni maganda au magamba?
 
katika wanaokwenda kumpa pole wahusika wamo pia!!!!
 
Duh! Hili tena ni jambo zito. Tuombe Mungu isijekuwa ni mwendelezo wa yale ya Dr Ulimboka. Kijan mahiri kwenye kazi yake naona hatakiwi. Watabaki akina nani jamani???????????????
 
Watu kama nyie ni sumu kubwa kwa taifa hili. Ungekuwa ni mtu mwenye busara, ungeacha vyombo vya usalama ambavyo ndio wataalamu wa uchunguzi wa matukio kama haya vikafanya kazi yake badala ya ku-jump on conclusions zinazoongozwa na hisia hasi na za kishetani kama zako.

Kwa hivyo mtu ye yote anayehama chama na kujiunga au kuunga mkono chama kingine akiugua, akafanyiwa vitendo vya kihalifu, akapata ajali, ama akafariki - basi conclusion ni amefanyiwa na watu wa chama alikotoka! Kweli tutafika kwa uwendawazimu kama huu.

mbona umecopy kipande tu? na hao wanaohitimisha kwa kuhusisha tukio hilo na mipango ya vyombo vya dola kuwateketeza wanaopinga serikali unawashauri nini
 
Akili yako imejaa kamasi kama unamtegemea Pasco kukupa vivid evidence, ungekuwa na akili ungeanza kuomba Invisible asitishe ban ya Ritz ili aje kufafanuwa ile kauli ya Waislamu anowajuwa yeye kuhusu gazeti la Mtanzania.

CC: chama
Invisible tunaomba muilift ban ya Ritz kuna kila ushahidi anajuwa mipango hii tangu awali na ushahidi upo humu humu JF. achaneni na porojo za Pasco.

Kama yangu imejaa kamasi wewe imejaa maji.
 
tangia mtanzania lilipoamua kuweka pua kwenye habari hii iliyopostiwa kwenye hii post nilijua kibanda anajihatarishia maisha yake.




Mnakumbuka kuwa siku mbili tu baada ya hii habari, radio imaan iliiripoti na mtanzania, hasa mhariri wake akalaumiwa sana? Kwa mliobahatika kusikiliza yale matangazo ya radio imaan na waliokuwa wanaongea, mtajua kuwa kibanda alikuwa ameuweka usalama wake mashakani.
malaria sugu alileta thread aliyohitimisha kwa kusema aljaazira center inawataka mtanzania wakanushe habari hiyo ndani ya siku saba



[kwa bahati mbaya] baada ya ile habari, mtanzania inasemekana waliendelea kuchunguza kuhusu kile chuo, na punde wangekuja na more detailed report.

Pole sana kibanda...

mashaka yangu yapo kwa chadema kuwa wanahusika ktk tukio hili.
 
nadhani mkasa huu unaenda sambamba na article waliyoiandika gazeti lake la mtanzania kuhusu chuo kilichojengwa ukerewe alichodai kinaendesha mafunzo ya kigaidi.yeye akiwa ni mhariri mkuu wa gazeti hili.bila shaka kile alichoandika hakijawapendeza wasomaji hasa walioguswa na habari ile.

hakuna kitu kama hicho...............chadema ichunguzwe ktk hili.
 
serikali ya awamu ya liwalo na liwe

Hayo maneno ya mfa maji, mlifikiri mkifanya hivyo serikali itaonekana ndiyo imehusika wakati mambo yote yanajulikana
kuwa ni mgogoro wa Tanzania Daima na yeye ndo umemfikisha hapo. Pole yake jamani
 
Polisi waanze uchunguzi na gazeti la tanzania daima na chadema. kwani hatuelewi ni kwanini alikimbia huko alipokuwa mhariri wa hilo gazeti la mwenyekiti wa chama.
Umbeya mtupu; serikali inayoshindwa kulinda usalama wa watu wake haina maana. Elimu mmeshindwa..... Kilimo mmeshindwa........ Umeme mmeshindwa...... Afya mmeshindwa...... Hata usalama wa watu na mali zao umeshindwa? Aibu kuubwa
 
Watanzania tuna uoga sio amani tunadanganywa. Damu yako iwe chachu ya ukombozi kibanda. Wanahabari kuweni chonjo na magamba!
 
tofauti yake nini? tume ngapi zimeundwa na zimeishia wapi Tume ya Dr Ulimboka ilipewa muda gani?na nini kinachoendelea? ya mwangosi je? ya Kubenea kumwagiwa tindikali?kwanza bora hata kule kusikokuwa na amani kasisa kuliko hii ya hapa kusiojulikana amani ipo au haipo tunasikia tuu katekwa na kunyofolewa kucha mara meno na vitendo vinginevyo? kumbuka wanaopewa madaraka na huyu mlala hoi na kumlipa pia na ulinzi kwa huyo mkubwa ni huyu huyu anayeteswa ndiyo anafanya yote haya.TUTALINDA USALAMA WA NCHI NA WATU WAKE DAH?
 
hii nchi inalaana yaani ubinadamu umeshaisha kabisa yaani afadhari kukutana na mnyama na si binadamu
 
Back
Top Bottom