Hii ni kudhihirisha tu kwamba wananchi hatuko salama kabisa. Kama wananchi wanavamiwa, wanapigwa, wanajeruhiwa na wengine kuuwawa kila mara na serikali kupitia vfyombo vyake vya dola wameshindwa kabisa kudhibiti hali hiyo ni dhahiri kwamba kama taifa tunahitaji kujipanga na kuchukua mwelekeo mpya kwa ajili ya usalama wetu.
Hii inadhihirisha pasipo shaka yoyote kwamba usalama wa taifa pamoja na jeshi la polisi wameshindwa kabisa kutekeleza majukumu yao ya msingi kwa raia wa nchi hii, na kimsingi hatuoni umuhimu wa kuwa na usalama wa taifa tulio nao kwa sasa kwakuwa wameshindwa kabisa kazi waliyotumwa kuifanya.
Na kwahali hii tunalazimika kuhitaji overhaul ya idara hii nyeti kwa ustawi, usalama na maendeleo ya watanzania. Major overhaul kwa TISS ni kitu kisichoepukika kwa sasa.