Kama kawaida, kwa kupitia jf, be the first to know, kuwa hivi sasa, juhudi zinafanywa kumhamisha Kibanda kwenda nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi. Juhudi hizi zinaratibiwa na Jukwaa la Wahariri kwa ushirikiano wa karibu na baadhi ya wadau watakao gharimia safari hiyo!.
Japo ni kawaida kwa serikali kupeleka baadhi ya wagonjwa nje ya nchi, preference ya kwanza ya serikali ni kupeleka wagonjwa India kwa sababu its cheaper kuliko Afrika Kusini ambapo gharama ziko juu!.
Hili la Kibanda kupelekwa A. Kusini, linazidi kumshabihianisha Kibanda na Dr. Dr. Ulimboka, wote walivamiwa usiku na watu wasiojulikana, wote walifanyiwa jinai ya kudhuru mwili, wote walihudumiwa kwanza MOI, na baadae kupelekwa nchini Afrika Kusini, juhudi za kwanza ni kusafirishwa kwa michango ya wadau na baadae serikali ikatumbukiza mkono wake.
Mara ya mwisho kukaa na Kibanda ni mwezi Desemba, mara tuu baada ya kuhama Tanzania Daima, tulikutanishwa mahali na mwana jf Omar Ilyas, na miongoni kwa swali kubwa langu kwa Kibanda, nilidadisi ni kwa nini amehama Tanzania Daima kuelekea Mtanzania, alichonijibu nilibaki tuu kushangaa bila kumuamini. Kwa vile jibu lile lilikuwa off the record, lakini maadam haya yamentokea, naanza to connect the dots!.
Kwa sasa, tuendelee kwanza kumtakia uponyaji wa haraka na mengine yatafuatia!.
We keep on wishing him a speedy recovery and get well soon!.
Pasco