Absalom Kibanda na Theophil Makunga waibwaga serikali kesi ya uchochezi

Absalom Kibanda na Theophil Makunga waibwaga serikali kesi ya uchochezi

Miruko

Senior Member
Joined
Feb 8, 2008
Posts
173
Reaction score
46
Hakimu Waliarwande Lema wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, hivi punde amewaachiwa huru, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda na Mjumbe wa Bodi ya Jukwaa hilo, Theophil Makunda katika kesi ya jinai ya uchochezi iliyokuwa inawakabil.

Katika kesi hiyo pia Salmson Mwigamba alikuwa anashtakiwa kwa makala aliyoandika kwenye gazeti la Tanzania Daima, yenye kichwa cha habari "Waraka Maalumu kwa askari wote" iliyotafsiriwa kuwa ilikuwa ya kuwachochea wanajeshi.

Wakati huo, Kibanda alikuwa Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima na Makunda alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd iliyochapisha gazeti hili.

Hakimu amesema walishtakiwa kwa hisia, na kwamba hisia haziwezi kuwa na mashiko hataka kama zina nguvu kiasi gani.
 
Mahakama ya kisutu imewaachia huru Kibanda na Makunga na Mwigamba waliokuwa wanashtakiwa kwa uchochezi.

Mahakama imesema serikali imeahindwa kuthibitisha makosa dhidi yao.
 
Sasa huyo alietoa kibali kwa hao watu kushtakiwa ndo alipe gharama za kesi yote hii.. Maana toka mwanzo ilikuwa ni kichekesho ambacho mwisho wake ulikuwa unajulikana.. Imefika wakati sasa kila mtu kuwajibika katika eneo lake la kazi..
 
Nakala kwa Juma Nkamia (Mzee asiyeongea na Mbwa bali mwenye mbwa) atakata rufaa!
 
Kibanda rudi sasa kwenye mapambano, achana na hao watu watakuua
 
The prosecution case was so weak making any reasonable lawyer to come to the conclusion that acquittal will be the end result of the case.

Thanks to God that I (in cooperation with the other defense counsel) defended my very long time friend Samson Maingu Mwigamba with all my abilities and integrity. The family must be happy today hearing that their father and husband (Mama Brenda) is now free. Justice has not only been done but seen to be done.
 
haya serikali yetu lipeni hela ya usumbufu kama kawaida yenu!!
 
Asante sana hakimu kwa kutenda haki, usitishiwe nyau na siasa za maji taka.
 
hivi kesi ya yule mhaini mwigamba inaendeleaje?

Mkuu righteye, usiwe na mhemko wa kisiasa unaokosa weledi wa kuchuja mambo. Kesi iliyokuwa inamkabili Samson Mwigamba ni ya kuandika makala iliyokuwa inadaiwa na Jamhuri kuwa ni ya kichochezi. Kesi hiyo ndiyo imekwisha leo na Samson Mwigamba ameonekana hana hatia na Mahakama.

Hilo suala la uhaini pia ni kama mmelishwa -----. Uhaini (treason) ni kosa linalofanywa tu dhidi ya dola (state). You can not commit treason against a political party. Tafuta kesi ya Hamis Ali Machano na wenzake dhidi ya Jamhuri ambapo Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ilisema wazi kuwa uhaini ni kosa ambalo hufanywa dhidi ya dola na kwa kuwa Zanzibar haikuwa dola basi uhaini usingeweza kufanywa na wakata rufaa huko Zanzibar.

Msomi mwenzagu Tundu Antipas Mughwa Lissu alipotoka kimantiki na kisheria alipokuwa akiutangazia umma kuwa Samson Mwigamba na Kitila Mkumbo ni wahaini. I repeat, you can not commit treason against a political party, never!!!
 
Serikali huwa haishindi kesi kwasababu huwa inaendeshwa na emotion badala ya facts, Inaonekana hapa ofisi ya mwanansheria mkuu haikumshauri DPP vizuri na hii ni upotezaji wa muda kwa kumshataki mtu kwa hisia badala ya vidhibiti.
 
Kazi kwenu maccm, mliezoea kupakazia watu kesi kisa wameongea ukweli, endeleeni mzidi kuumbuka, maana mmgeuza mahakama za ccm hizo, mmempoteza mpaka Zitto, siku hizi anafanyia siasa mahakamani, wenzie waruka na chopa kutafuta ukombozi, yeye anawaza mahakama, kazi kweli kweli.
 
Sasa huyo alietoa kibali kwa hao watu kushtakiwa ndo alipe gharama za kesi yote hii.. Maana toka mwanzo ilikuwa ni kichekesho ambacho mwisho wake ulikuwa unajulikana.. Imefika wakati sasa kila mtu kuwajibika katika eneo lake la kazi..

walijua hawatashinda ndio maana wakaamua kumtoboa jicho.....
 
Back
Top Bottom