Absalom Kibanda na Theophil Makunga waibwaga serikali kesi ya uchochezi

Absalom Kibanda na Theophil Makunga waibwaga serikali kesi ya uchochezi

Serikali huwa haishindi kesi kwasababu huwa inaendeshwa na emotion badala ya facts, Inaonekana hapa ofisi ya mwanansheria mkuu haikumshauri DPP vizuri na hii ni upotezaji wa muda kwa kumshataki mtu kwa hisia badala ya vidhibiti.

haki imetendeka at last,kwenye dunia hii iliyojaa waongo,mabazazi,mahayawani,waliokosa utu,mkweli siku zote ataonekana adui,na inahitaji ujasiri wa ziada kuwa mtu huyo,shall truth only set us free!
 
Ilibidi hata gazeti la ----------- serikali ingeenda kushitaki mahakamani kuliko kufungia gazeti lisilokuwa na hatia.

haki imetendeka at last,kwenye dunia hii iliyojaa waongo,mabazazi,mahayawani,waliokosa utu,mkweli siku zote ataonekana adui,na inahitaji ujasiri wa ziada kuwa mtu huyo,shall truth only set us free!
 
‪Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru Mhariri Mtendaji wa kampuni ya New Habari, Absalom Kibanda, Meneja Uendelezaji Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communication Limited Theophil Makunga na mwandishi Samson Mwigamba.

Akisoma hukumu yao ya kesi ya uchochezi leo Jijini Dar es Salaam, Hakimu Mkazi Warialwande Lema amesema washtakiwa hao walishtakiwa kwa hisia tu na hisia haziwezi kuwa na mashiko hata zikiwa na nguvu ya aina gani na kuongeza kuwa ushahidi uliowasilishwa dhidi yao ulikuwa dhaifu source eatv.
 
Naona kama Kibanda alishapokea hukumu yake ya awali, kwa kung'olewa meno, jicho, kidole na kucha kutokana na kalamu yake!
 
hakimu waliarwande lema wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu, hivi punde amewaachiwa huru, mwenyekiti wa jukwaa la wahariri, absalom kibanda na mjumbe wa bodi ya jukwaa hilo, theophil makunda katika kesi ya jinai ya uchochezi iliyokuwa inawakabil.

Katika kesi hiyo pia salmson mwigamba alikuwa anashtakiwa kwa makala aliyoandika kwenye gazeti la tanzania daima, yenye kichwa cha habari "waraka maalumu kwa askari wote" iliyotafsiriwa kuwa ilikuwa ya kuwachochea wanajeshi.

Wakati huo, kibanda alikuwa mhariri mtendaji wa tanzania daima na makunda alikuwa kaimu mkurugenzi mtendaji wa mwananchi communications ltd iliyochapisha gazeti hili.

Hakimu amesema walishtakiwa kwa hisia, na kwamba hisia haziwezi kuwa na mashiko hataka kama zina nguvu kiasi gani.

hiyo kesi haina tofauti na madai ya usaliti wa zito kwa chadema....ni hisia tu ambazo 'wasiochanganya' na zao kichwani wamenasa, bahati mbaya hao ndio wengi ndani ya chama!!!
 
Ninachokiona mimi ni UTANZANIA DAIMA NA UCHADEMA.


KIBANDA =Alikuwa mhariri mtendaji wa freemedia.
SAMSON=Alikuwa sio mwandishi wa makala kali dhidi ya ccm tu ila UENYEKITI WA CHADEMA ndio uliwafikisha hapo walipofikia.

ILA LEO HII HAKUNA HATA MMOJA ANAEFUNGAMANA NA CHADEMA WALA FREEMEDIA.

habari ndio hiyo kwa kuachiwa huru na katika hao hakuna atakae kata rufaa.
 
mimi naanza kuwa na imani na mahakana zetu chini mahakimu mahiri na wenye elimu za kutosha wasio penda rushwa. nawaombea mungu majaji na mahakimu kama hawa. lakini kwa wale wasio na sifa na wapenda rushwa igeni heshima kwa wenzenu hawa na muone aibu kwani mnachafua sifa ya mahakama tukufu
 
Mkuu righteye, usiwe na mhemko wa kisiasa unaokosa weledi wa kuchuja mambo. Kesi iliyokuwa inamkabili Samson Mwigamba ni ya kuandika makala iliyokuwa inadaiwa na Jamhuri kuwa ni ya kichochezi. Kesi hiyo ndiyo imekwisha leo na Samson Mwigamba ameonekana hana hatia na Mahakama.

Hilo suala la uhaini pia ni kama mmelishwa -----. Uhaini (treason) ni kosa linalofanywa tu dhidi ya dola (state). You can not commit treason against a political party. Tafuta kesi ya Hamis Ali Machano na wenzake dhidi ya Jamhuri ambapo Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ilisema wazi kuwa uhaini ni kosa ambalo hufanywa dhidi ya dola na kwa kuwa Zanzibar haikuwa dola basi uhaini usingeweza kufanywa na wakata rufaa huko Zanzibar.

Msomi mwenzagu Tundu Antipas Mughwa Lissu alipotoka kimantiki na kisheria alipokuwa akiutangazia umma kuwa Samson Mwigamba na Kitila Mkumbo ni wahaini. I repeat, you can not commit treason against a political party, never!!!

Ahahahaha.........unanikumbusha Montevideo Convection mkuu
 
Ah! Nadhani wakati wa mwanasheria mkuu na ofisi ya DPP kutubue dhambi zao! Kazi ya mwananchi yeyote ni kuliamsha na kulitenda kundi linaloonewa. Mwigamba alijaribu kulitetea kundi ambalo bado linakandamizwa ili nalo likandamize wananchi. Bila ya hili kundi kujitambua na kuendesha kesi za kisiasa, basi tutaendelea kusikia tena fulani ni mchochezi. Lakini sijui kwa nini mwandishi azuiwe kuwa mchochezi? Maanake kama moto wa kuni unatakazima lazima uongeze kuni ili nalo liwake. CCM alishawafanya watu wasinzie fofofoooooooooooo, kwa hiyo wanapoona mtua anaamsha, moto unachochewa watu wasijisahau ili wajitambue na kuiondoa madarakani, basi hoja itakayotoka, oh wanachochea ili kuvuruga amani! Aksante hakimu Lema Mungu akupe nguvu na mahakimu wengine wenye kutetea haki
 
Hongereni Makamanda. Mpaka mwisho wa mwaka huu, watashitakiwa wengi kwa utaratibu huu.
 
Lengo la kesi lilikuwa kugeuza msimamo wa Mwigamba na Kibanda dhidi ya CCM na Serikali yake. Kesi iliisha kitambo mara tu baada ya kesi hiyo kufanikiwa kuwafanya kuwa mawakala wa magamba! Hiyo ndiyo Tanzania!
 
Bravo..and arutta continua. You cant shoe a running horse you Mr government!
 
Back
Top Bottom