Absalom Kibanda na Theophil Makunga waibwaga serikali kesi ya uchochezi

Absalom Kibanda na Theophil Makunga waibwaga serikali kesi ya uchochezi

Samsoni Mwigamba ameshinda kesi ya uchochezi ilyokuwa ikimkabili yeye na wenzake Absalom Kibanda na Makunga. Kesi hiyo ilifunguliwa na Jamhuri baada ya Mwigamba kuandika Makala katika gazeti la Tanzania Daima iliyokuwa na wito kwa askari wote kutokutii amri ambazo si halali zinazotoka kwa wakubwa zao hasa zile zilizokuwa na lengo la kuua raia hususani kwenye mikutano ya CHADEMA.
 
Hakimu Waliarwande Lema wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, hivi punde amewaachiwa huru, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda na Mjumbe wa Bodi ya Jukwaa hilo, Theophil Makunda katika kesi ya jinai ya uchochezi iliyokuwa inawakabil.

Katika kesi hiyo pia Salmson Mwigamba alikuwa anashtakiwa kwa makala aliyoandika kwenye gazeti la Tanzania Daima, yenye kichwa cha habari "Waraka Maalumu kwa askari wote" iliyotafsiriwa kuwa ilikuwa ya kuwachochea wanajeshi.

Wakati huo, Kibanda alikuwa Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima na Makunda alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd iliyochapisha gazeti hili.

Hakimu amesema walishtakiwa kwa hisia, na kwamba hisia haziwezi kuwa na mashiko hataka kama zina nguvu kiasi gani.
Kumbe kesi za uchochezi zipo toka kitambo?
 
Back
Top Bottom